Ninaishi na Kijana wa ndugu yangu, alikuja kwangu miezi 5 iliyopita, ana umri wa miaka 17 kwa sasa ila amekuwa mraibu wa kucheza gemu la mpira linaitwa eFootball mpaka anakesha usiku mzima analala saa 10 alfajiri hivyo analazimika kuamka saa 7 mchana.
Nimeshaongea mno mpaka nimekata tamaa, kila nikimshauri ananijibu anaacha, ila anaendelea, hali hiyo imekuwa kero kubwa mno kwani hata akiamka huo mchana, atafanya kazi za nyumbani akona zimemalizika zile zinazomuhusu basi ataingia kwenye gemu hapo ukimuita au kusema chochote jibu lakke subiri kidogo nimalizie mechi nitafungwa.
Anakera sana kwani kawa kama mgonjwa wa akili muda wote yupo anacheza gemu, simu ikiisha chaji anaweka chaji anaendela kucheza gemu, sielewi nitumie mbinu gani tena nimuachishe kucheza gemu hili kwani tabia hii hakua nayo hapo awali kabla hajafundishwa kucheza gemu hili.
Alikuja kwa lengo la kuja kuanza VETA ila kuna vitu vikawa bado havijakaa sawa tukampa muda kidogo tujipange sasa muda huu ambao yupo nyumbani ni gemu masaa yote mpaka anatia hasira.
Nifanye nini kumnusuru na janga hili?