Nitumie mbinu gani kumuachisha kucheza e Football kijana huyu, linamlaza saa 10 alfajiri

Nitumie mbinu gani kumuachisha kucheza e Football kijana huyu, linamlaza saa 10 alfajiri

Wakati naanza ni mwaka jana mwezi wa pili

Kwenye efootball kuna makundi mawili kuna pay to win players wanatoa hela kununua wachezaji wakubwa


Na sisi wa Free to play team😃tunaoishi kwa free players na kudra za Allah kwenye kuspin


Kikosi changu mpaka hapo sijawai tumia hela kununua coins kwa ajili ya mchezaji View attachment 3638362
Mm nmeanza mwaka jana mwez wa 9 ila had leo sijafka 3200🤣sina bahat kbs na free chance deals ila mwez ujao nitafka naona
 
Ninaishi na Kijana wa ndugu yangu, alikuja kwangu miezi 5 iliyopita, ana umri wa miaka 17 kwa sasa ila amekuwa mraibu wa kucheza gemu la mpira linaitwa eFootball mpaka anakesha usiku mzima analala saa 10 alfajiri hivyo analazimika kuamka saa 7 mchana.

Nimeshaongea mno mpaka nimekata tamaa, kila nikimshauri ananijibu anaacha, ila anaendelea, hali hiyo imekuwa kero kubwa mno kwani hata akiamka huo mchana, atafanya kazi za nyumbani akona zimemalizika zile zinazomuhusu basi ataingia kwenye gemu hapo ukimuita au kusema chochote jibu lakke subiri kidogo nimalizie mechi nitafungwa.

Anakera sana kwani kawa kama mgonjwa wa akili muda wote yupo anacheza gemu, simu ikiisha chaji anaweka chaji anaendela kucheza gemu, sielewi nitumie mbinu gani tena nimuachishe kucheza gemu hili kwani tabia hii hakua nayo hapo awali kabla hajafundishwa kucheza gemu hili.

Alikuja kwa lengo la kuja kuanza VETA ila kuna vitu vikawa bado havijakaa sawa tukampa muda kidogo tujipange sasa muda huu ambao yupo nyumbani ni gemu masaa yote mpaka anatia hasira.

Nifanye nini kumnusuru na janga hili?
Wazazi wakina Junior, mnatengeneza kizazi cha kizembe, kibovu kisichokuwa na nidhamu. Wazee wetu anaongea mara moja tu, unatii juchanganye sasa ukifanye alicho kukataza.

Wewe mzazi mzembe na ukizembea mtoto atakutawala.
 
Nilivyoanza kucheza nilikuwa nacheza kwa siku hata masaa 10 na zaid napumzika tuu simu ikiwa chaji... Ila baada ya kulizoea naweza pitisha siku kama nimebanana sijacheza...

Kwahiyo ni starehe kama tu kuangalia movie au Series...


Pia kama ana uwezo anaweza komaa akaenda kushiriki kimataifa nina Jamaa yangu mmoja kawekeza nguvu zote huku amechaguliwa kwenda kimataifa kushindanaView attachment 3638363
Nampata uyu Song director, tiktok namjua na div nilishawah kukutana nae
 
Nilivyoanza kucheza nilikuwa nacheza kwa siku hata masaa 10 na zaid napumzika tuu simu ikiwa chaji... Ila baada ya kulizoea naweza pitisha siku kama nimebanana sijacheza...

Kwahiyo ni starehe kama tu kuangalia movie au Series...


Pia kama ana uwezo anaweza komaa akaenda kushiriki kimataifa nina Jamaa yangu mmoja kawekeza nguvu zote huku amechaguliwa kwenda kimataifa kushindanaView attachment 3638363
Kumbe linafaida yake siyo starehe tu na kupoteza muda. Mimi lilinishida nikaliondoa kwenye simu.
 
Back
Top Bottom