Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Mimi ni mtaalamu wa afya ya kinywa na meno napatikana Magomeni - Dar es Salaam na Kibaha -pwani
Kama una swali au changamoto yoyote kuhusu kinywa na meno niandikie hapa chini nitajitahidi kujibu kadri ya uwezo wangu.
  • Katika vituo hivyo vya kazi pia natoa huduma zifuatazo kwa gharama rafiki kabisa .
  • Elimu ya kinywa na meno
  • Kuziba meno yaliyotoboka
  • Kusafisha meno na kung'arisha meno
  • Kupanga meno (braces)
  • Kuweka meno bandia (partial/full denture )
  • Huduma ya mzizi wa jino (root canal treatment)
  • Urembo wa meno
  • Veneers, bleaching, crowns and bridges
Kinywa chenye afya, mwili wenyhudu
Huduma ya kupanga meno (brace's) inacost bei gani na inapanga kwa muda gani mkuu?
 
Ceramics crowns zinadumu zaidi ya miaka 25. Karibu sana
Okay kumbe poa sana,kuna jino moja kubwa gego limeanza kuniuma kwa vipindi,halipo serious ila smtm linauma kidogo kisha hiyo hali inapotea,bahati mbaya sipo dar now lkn nimefaidika na ushauri wa kutibu mzizi wa jino na kuondoa uwezekano wa kung'oa jino

Nitakapo rudi dar nitakutafuta katika swala zima la afya ya kinywa
 
Nini kinafanya toses (mafindofindo)kuuma bila kuwa kidonda. tofauti na kunywa maji ya baridi baadhi ya watu
 
Unajua kilimi? Nimeshauriwa nikakatwe kwakuwa nakohoa bila kupona, nmeenda hospital wakasema kilimi akikatwagwi..
Nini maoni yako mutahalamu
 
IMG_20241005_093645_811.jpg
Meno ya Kahawia (Fluorosis) hutokea mtoto anapopata kiwango kikubwa cha fluoride akiwa tumboni au katika miaka ya mwanzo ya maisha.

Meno huanza kutengenezwa kati ya wiki ya 3 hadi 6 ya ujauzito.

Ikiwa mama anapata maji au vyakula vyenye fluoride nyingi, meno ya mtoto yanayokua yanaweza kuathirika, na kusababisha madoa meupe au rangi ya kahawia kwenye meno baada ya kutokeza.

Matibabu ya meno ya kahawia

1. Kupiga mswaki na polishing – Kusafisha sehemu za juu za meno ili kupunguza madoa mepesi.

2. Bleaching – Njia ya kusafisha kitaalam kwa kutumia kemikali ili kupunguza rangi ya meno.

3. Veneers– Viboreshaji vidogo vya porcelaini au composite vinawekwa kufunika meno yaliyoathirika.

4. Crowns – Kofia za meno zinavaliwa kwenye meno yaliyoathirika sana ili kuboresha muonekano na uimara.

Kujua matibabu yapi hutegemea kiwango cha fluorosis. Kwa taarifa zaidi fika offisini kwetu ,Uweze kupata Elimu , Matibabu

Kibaha - Pwani, Magomeni- Dar es Salaam
kama una tatizo hili karibia PM tuweze kulitatua na ufafanuzi zaidi.
 
Huu ni uzwazwa tu binadamu walijibunia, ikazoeleka… na mabumunda ya kiafrika yakaiga kutoka kwa hao mashetani wa huko ughaibuni 😄
Je ni kweli kwamba kwenye kinywa cha binadamu kuna sehemu zenye nyenge ndio maana watu hupigana denda?

Ukweli ni upi mpaka watu wapende kupigana denda?
 
Mimi ni mtaalamu wa afya ya kinywa na meno napatikana Magomeni - Dar es Salaam na Kibaha -pwani
Kama una swali au changamoto yoyote kuhusu kinywa na meno niandikie hapa chini nitajitahidi kujibu kadri ya uwezo wangu.
  • Katika vituo hivyo vya kazi pia natoa huduma zifuatazo kwa gharama rafiki kabisa .
  • Elimu ya kinywa na meno
  • Kuziba meno yaliyotoboka
  • Kusafisha meno na kung'arisha meno
  • Kupanga meno (braces)
  • Kuweka meno bandia (partial/full denture )
  • Huduma ya mzizi wa jino (root canal treatment)
  • Urembo wa meno
  • Veneers, bleaching, crowns and bridges
Kinywa chenye afya, mwili wenye furaha.

View attachment 3117272
Kwanini watu wengi wanasumbuliwa na tonsilolith?
Je ni vizuri kuondoa tonsils kwa Operation au dawa?
 
Huduma ya kupanga meno (brace's) inacost bei gani na inapanga kwa muda gani mkuu?
Inategemea na hali ya meno ilivyo minimum miezi sita maximum miaka miwili. Kuhusu gharama za kufunga naomba tuwasiliane PM itakuwa bora zaidi . Mana zinatofautiana kulingana na cases
 
Ni kweli meno husababisha mdomo kutoa harufu mbaya kama chemba ya choo? Kama ndio kwanini? Kama sio nini kisababishi?
Sababu za kinywa kuoa harufu mbaya ni
.Meno yaliyotoboka bila kutibiwa
.Matumizi ya baadhi ya dawa
.Magonjwa ya fizi
.kinywa kikavu
Ukiona una hilo tatizo tuwasiliane PM uweze kupata tiba kwa tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni. Nitafurahi nikikuhudumia
 
Km meno ni mabovu unakua na uwekano mkubwa wakutoa almost yote au uzibe maana img’arishaji wanatumia ngumu sana hovyo kuumiza fizi alternative utumie dawa zakung’arisha badala ya kusafisha Kwa vifaa vya maabara.
Hizi dawa unatumia kusukutua wkt wakupiga mswaki pekee.
Kingine kunywa maji ya kutosha,usile Kwa vingi vyakula vya sukari kwakua ni adui mkubwa wa meno kuoza.
 
Unajua kilimi? Nimeshauriwa nikakatwe kwakuwa nakohoa bila kupona, nmeenda hospital wakasema kilimi akikatwagwi..
Nini maoni yako mutahalamu
Fata ushauri wa wataalamu.
 
Okay kumbe poa sana,kuna jino moja kubwa gego limeanza kuniuma kwa vipindi,halipo serious ila smtm linauma kidogo kisha hiyo hali inapotea,bahati mbaya sipo dar now lkn nimefaidika na ushauri wa kutibu mzizi wa jino na kuondoa uwezekano wa kung'oa jino

Nitakapo rudi dar nitakutafuta katika swala zima la afya ya kinywa
Shukrani sana karibu ,namba ipo hapo unaweza save kabisa
 
Hivi meno ya bandia ufanyaji wake kazi wake ni sawa na meno halisi au meno bandia kuna linakuwa na limit ya baadhi ya mambo

Au kwenye meno bandia kunakuwa na madaraja ya viwango katika efficiency.

Kwasababu wakati niko skul nilikuwa namuona teacher wetu wakati wakula msosi anayatoa meno yake ya mbele ya bandia ili aweze kula.

Sasa swali langu, hakuna meno bandia ambayo yatakuwa na efficiency ile ile ambayo meno halisi huwanayo?
 
Halafu kingine

Kung'arisha meno kunaweza kufanyika kwa jitihada za mswaki kupitia dawa maalumu?

Yani naulizia kama kuna dawa ambayo mtu akiwa anaitumia hiyo instead of Colgate.

Au haiwezekani mpaka aje clinic afanyiwe special cleaning ya kuhusisha chemicals kama ambavyo umetaja?
 
Back
Top Bottom