Niulize chochote kuhusu mizimu

Nimekuelewa vema
 
Ustaaz Salamaleko.
 
Mizimu ni Mapepo au Majini yanayofutilia ukoo fulani.
Hakuna Mizimu mizuri kwa mfano utakuta ukoo una watu masikini sana na wana Mizimu inayo shindwa kuwakwamua kiuchumi.
Mizimu inapenda kuabudiwa na ina vilinge vya kuiabudu.

Kitu inachopenda kwenye familia ni uganga uchawi tu.
Utasikia mikoba ya babu irithishwe kwa mjukuu ilimrani iendelee kuabudiwa na ukoo husika.
Mizimu ikiona inapotezewa kuabudiwa inaanza kuleta mikosi kwenye ukoo husika kama magonjwa na taabu mbali mbali.
Inaleta taabu Hadi ukoo au familia au mtu husike afanye tambiko (ibada ya Mizimu) ndio apate nafuu.
Ibada halisi ya Mungu ndio njia pekee ya kuiondoa Mizimu katika Koo, Familia, au mtu husika.
 
MIZIMU HAINA AKILI NI MAJINI YANAYOCHUKUA SURA ZA WATU WALIO KUFA... HAKIKA KUMJUA YESU NDIO CHANZO CHA MAARIFA
 
HAKUNAGA MAJINI WAZURI MAJINI WALISHAPOTEZA SIFA NIA YAO NI OVU DAIMA HAWANA JEMA WANALO WAZA
 
Mizimu ni roho za watu (ndugu) waliokwisha kuiacha miili yao, na roho zao zimeibaki kutangatanga huku hatma yake ikiwa ni kuzimu...

Iweje wewe mwanadamu mwenye uhai na utashi kamili utake kuongozwa na roho za wafu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…