Huyo Mungu kwa nini anamuacha ibilisi aite watu wafanye mabaya badala ya kumwangamiza?
Ibilisi kupewa muda mrefu kuishi hapa duniani, Sio tiketi ya yeye kutumia kuwaita binadamu wafanye mabaya.
Huyo Mungu kwa nini ampe ibilisi maisha marefu duniani ilhali alijua ibilisi huyo atatumia muda huo kuita watu wafanye mabaya?
Mungu mnayedai ni mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Anakupa mtihani ili ajue nini?
Ina maana huyo Mungu wakati anakuumba alikuwa hajui utafanya matendo gani mpaka akupime kwa kukupa mtihani?
Kama huyo Mungu ni mjuzi wa vyote tangu mwanzo na hata milele, Anakupima kwa kukupa mtihani ili nini?
Wakati tayari alijua na anajua matendo yako tangu mwanzo na hata milele.
Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Kama huyo Mungu hapangiwi na yeyote, Kwa nini hapendi uovu na mabaya ilihali yeye ndiye muumbaji wa kila kitu?
Kama hapendi uovu na mabaya, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?
Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasio na uwezo wa kutenda mabaya?
Kwa nini huyo Mungu aumbe Dunia yenye uovu na binadamu wenye uwezo wa kutenda mabaya, Halafu aje alalamike kwamba kwa nini hatutendi mema?
Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?