Niulize chochote kuhusu mizimu

Niulize chochote kuhusu mizimu

YANI MISUKULE KWAKO NI WATU WALIO FUFUKA AU UNAMAANISHA NINI

KAMA UNAZUNGUMZIA MISUKULE INAYOPOTEZWA KIMAZINGIRA MNADHANI MNAZIKA MTU KUMBE NI MGOMBA WA NDIZI BASI NGOJA NIKUACHE KIDOGO MKUU
Kama unaamini hivyo basi hakuna tatizo

Ahsante
 
Tungelikuwa tunapewa options ya jinsi kuwa katika form, ningechagua kuwa MALAIKA.
 
Habari wakuu,

Nipo bariadi gamboshi masomoni nachukua digrii ya uchawi wenye faida.

Mizimu ni roho za watu waliokufa.

Kila mtu ana mizimu. Mizimu ya upande wa kwa baba na ya upande wa kwa mama (mababu na mabibi wote waliokufa)

Mizimu ipo mizuri na mizimu mibaya

Kuna aina zaidi ya >200 za mizimu.

Kama una swali lolote kuhusu mizimu kisayansi au kiroho niulize nitakujibu

Ahsante
Mizimu ina jinsia?
 
Je mizimu inaweza kukupa mali? Mfano huyo mtu alikua na mali sasa akazificha mahali maeneo ya kwake na alizizindika kiutalaamu na mganga! Na kwenye ile mali alinuia ije imkute mtoto wake hata kama yeye ameondoka.
Sasa imepita takriban 24 years mtoto wa kike kashakua mkubwa na kapata mtu kumuowa na katika pita pita kwa wataalamu yule mtu na mtoto wakaambiwa wamekutanishwa na mizimu na imewafungisha ndoa na inataka kuwapa mali.
Na huyo kijana kuna siku alipata ndoto ya kuijiwa na baba wa mke wake akaambiwa maneno na baba yupo vile vile japo hajawahi kumwona... na ile mali haijawahi kutolewa mpaka leo wengi walihangaika wameshindwa na anaweza kufa mtu pale wakifanya masihara na ile mali. Na wataalamu wanasema ile mali haiwezi toka pasipo yule mtoto kipenzi cha baba.

Hii scenario unaweza elezea vipi?
Hilo ni agano
 
Mizimu ya kichawi isikie tu kwa watu ni hatari sana yaana ni full package inavuruga kila kitu kuanzia nyota, kazi, ndoa mwili mpaka biashara na maradhi juu

Kujinasua nenda kanisani au watafute wazee wako wa ukoo
mimi sio Mkristo mimi ni Muislam na wazee wote wamesha fariki Ninao mzimu wa kichawi unaniliazimisha niwe mchawi lakini sitaki unaniharibia kila kitu na mpaka maradhi unanitia nitakuja huko Gamboshi nipambane nao mzimu wa kichawi.Nipate kuutoa usinifuate tena .
 
mimi sio Mkristo mimi ni Muislam na wazee wote wamesha fariki Ninao mzimu wa kichawi unaniliazimisha niwe mchawi lakini sitaki unaniharibia kila kitu na mpaka maradhi unanitia nitakuja huko Gamboshi nipambane nao mzimu wa kichawi.Nipate kuutoa usinifuate tena .
Wewe ni mkongwe hapa jukwaani unafahamika kwenye ekimu ya kiroho uoande wa tiba asili sidhani kama hilo tatizo hujui pa kulimaliza
 
Huyo Mungu kwa nini anamuacha ibilisi aite watu wafanye mabaya badala ya kumwangamiza?

Ibilisi kupewa muda mrefu kuishi hapa duniani, Sio tiketi ya yeye kutumia kuwaita binadamu wafanye mabaya.

Huyo Mungu kwa nini ampe ibilisi maisha marefu duniani ilhali alijua ibilisi huyo atatumia muda huo kuita watu wafanye mabaya?

Mungu mnayedai ni mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Anakupa mtihani ili ajue nini?

Ina maana huyo Mungu wakati anakuumba alikuwa hajui utafanya matendo gani mpaka akupime kwa kukupa mtihani?

Kama huyo Mungu ni mjuzi wa vyote tangu mwanzo na hata milele, Anakupima kwa kukupa mtihani ili nini?

Wakati tayari alijua na anajua matendo yako tangu mwanzo na hata milele.

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?

Kama huyo Mungu hapangiwi na yeyote, Kwa nini hapendi uovu na mabaya ilihali yeye ndiye muumbaji wa kila kitu?

Kama hapendi uovu na mabaya, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasio na uwezo wa kutenda mabaya?

Kwa nini huyo Mungu aumbe Dunia yenye uovu na binadamu wenye uwezo wa kutenda mabaya, Halafu aje alalamike kwamba kwa nini hatutendi mema?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Kwanza tambua kuwa MUNGU ana huruma sana na viumbe wake kuliko hasira/ghadhabu zake.

Ukiuliza kwanini Ibilis hakuangamwizwa hapo hapo alipokosea ni sawa na kusema kwanini Mungu amekuacha wewe uendelee kuishi ilihali ni mtenda dhambi.

Ibilis yeye hukumu yake ilishapita kitambo anajua kuwa yeye ni wa motoni hivyo anachofanya ni kulipa kisasi kwa Adam kwa kuhakikisha anaingia motoni na uzao wa Adam.

Mungu kashatuonya wanadamu kuwa tusimfanye ibilis kuwa ni rafiki yetu bali tumfanye kuwa ni adui. Yaani sisi na Ibilis ni maadui.

Hivyo ukipotea ni matokeo ya nafsi yako kumfanya ibilis kuwa ni rafiki yako badala ya kumfanya kuwa ni adui. Ni sawa uambiwe mbele yako kuna shimo kubwa ila bado ukakaza fuvu na kwenda kuingia kwenye shimo hilo.

Ibilis baada ya kuhukumiwa moto, alitumia nafasi hiyo kumuomba Mungu kwasababu anajua Mungu ni mwenye rehema sana, hivyo hakuomba toba bali aliomba maisha marefu.Mungu alimkubalia dua lake.
Ni hii ni kuonesha kuwa hata sisi wenye dhambi tukimuomba Mungu kwa dhati basi anapokea maombi yetu na kutujibu pia.

Mungu ni mjuzi wa yote anayajua yajayo na yaliyopita na ya sasa. Kutupa wanadamu mtihani sio kwamba alikuwa hajui tutakayoyatenda humu duniani. Ila alituacha tuishi ili siku ya mwisho tusije kuleta lawama kuwa hatukupewa muda wa kuyatenda mema. Ni kuwa mwisho wa siku kutakuwa hakuna excuse...! Nafasi wote tumepewa na tumechagua yale tuliyoyaridhia wenyewe.

Mungu hapendi maovu ndio maana akaleta mitume na manabii ili kubainisha haki . Alipomuumba mwanadamu alimpa akili na kumbainishia mazuri na mabaya kisha akampa na hiyari ya kuchagua mema au mabaya. Hivyo ukiyafanya mabaya ni matokeo ya chaguzi za nafsi yako mwenyewe
 
Mizimu ina nguvu kubwa kuliko majini ina uwezo wa kuishi hadi miaka elf sita.
Mizimu ni viongozi kama DC,RPC,RC.
Kazi yao kuu ni kusimamia ukoo, kabila,taifa,nchi,bara,nk ktk serikali ya shetani mizimu haitaki watu wawe na maendeleo wakiwa na maendeleo wataacha kuiabudu.
Hujui unachokiongea...Mizimu ni sawa na majini!
 
Habari wakuu,

Nipo bariadi gamboshi masomoni nachukua digrii ya uchawi wenye faida.

Mizimu ni roho za watu waliokufa.

Kila mtu ana mizimu. Mizimu ya upande wa kwa baba na ya upande wa kwa mama (mababu na mabibi wote waliokufa)

Mizimu ipo mizuri na mizimu mibaya

Kuna aina zaidi ya >200 za mizimu.

Kama una swali lolote kuhusu mizimu kisayansi au kiroho niulize nitakujibu

Ahsante
Mizimu Ina nguvu gani Kwa maisha ya watu walio hai?
 
Unaweza kutaja kozi angalau tano unazosoma kwenye hiyo degree yako ya uchawi?

Unaajiliwa na taasisi gani baada ya kuhitimu?
Chuo kinasajili wanafunzi wa ngapi kwa mwaka?
Ni kozi zipi zinazopendwa na wanafunzi wengi?
Kabla ya chuo kikuu je, kuna shule za msingi na sekondari ulizosoma za kichawi?

Chuo kipi maarufu hapa Africa mashariki?
Mna mahusiano na Satanist au freemason
 
Back
Top Bottom