Niulize kuhusu mgogoro wa vita wowote duniani nitakujibu papo papo!

Niulize kuhusu mgogoro wa vita wowote duniani nitakujibu papo papo!

Vita vya marekani na urusi vitaanza mwaka gani?
Vita ya marekani na Russia ni ngumu sana kutokea na inawezekana isiwepo kabisa.
Russia siyo threat/Adui mkubwa sasa kwa US kama ilivokua kipindi cha miaka ya 1922-1991….. ya muungano wa kisoviet.

Marekani ilifanikisha kuisambaratisha USSR na kufanya isiwe tishio kwa marekani.

Urusi haina uwezo wa kupigana na marekani katika vita ya kawaida kwa sababu haina uchumi. Uchumi wa marekani ni mara 24 zaidi ya russia.
Vita yyte inategemea uchumi.
Urusi inanguvu inapokuja swala la silaha za nyuklia ambazo hamna nchi inataka kuzitumia isipokua tu pale inapovamiwa.

Aidha kinachoendelea ni proxy war au vita ya mbali mbali kupitia nchi nyingine
Na nchi hiyo ni Ukraine.
Hapa ndipo vinapopiganwa vita hivi lakini lengo kubwa la marekani ni kuinyong’onyeza urusi na kuipunguza nguvu kiuchumi pia kisilaha . Bahati mbaya kama mpango unaenda ndivo sivyo

Kwa kifupi Vita ya moja kwa moja ya marekani haipo na uwezekano wa kuwepo ni mdogo.
Kama tu itatokea vita ya tatu ya dunia bas marekan na Russia zinaweza kuwa pande tofauti hapo ndipo zinaweza zikapigana na nchi wanachama wengine

Adui mkubwa wa marekani ni China.
 
Napenda kufuatilia sana migogoro na vita zinazoendelea duniani.

Mambo ya geopolitics.
Nipo hapa kukujibu maswali yako yote kuhusu migogoro mbalimbali duniani.


swalii lolote
Uko vizuri Sana mkuu pia hongera kwa kuyajibu maswali ya kejeli kwa akili kiasi yasiharibu Uzi wako.

Mkuu uwepo wa waislam wenye msimamo mkali kunahatarisha amani ya dunia kwa kiwango gani na Nini kinaweza kusaidia kuondoa tatizo hilo@Mr Chromium
 
Uko vizuri Sana mkuu pia hongera kwa kuyajibu maswali ya kejeli kwa akili kiasi yasiharibu Uzi wako.

Mkuu uwepo wa waislam wenye msimamo mkali kunahatarisha amani ya dunia kwa kiwango gani na Nini kinaweza kusaidia kuondoa tatizo hilo@Mr Chromium
Mkuu dunia inahatarishwa na mambo mengi lakini kubwa zaidi si dini kama dini ila ni watu wanaotumia hiyo dini kutimiza malengo yao.
mfano mdogo:
Taliban waliweza kusurvive kwa kuuza heroine na biashara za magendo ndio zilikua vyanzo vya mapato.

Al shabab huwa wanahusika kuteka na kupora,kuuza mihadarati ilimradi tu kundi lisikose fund
Hapo utaona si Dini maana dini hiyo hyo inakataza mihadarati.

Kifupi sehemu yyte yenye ugadi
Kuna ujinga,umasikini, elimu hamna, na vitu kama hivo.
Katika maeneo haya ni rahisi kulubuniwa watu kujiunga na hayo makundi maana commone sense ya watu kufikiri na kutafakari inakua ndogo.

Suluhuhisho lipo katika kuboresha maisha ya sehemu masikini ambazo dini ndio imetawala na hamna elimu,kuboresha maisha na vipato vya vijana ambao ndio huwa wahanga.

Waislam wenye itikadi kali kupambana nao na kuwamaliza ni kitu kigumu kwasababu itikadi ni idea kama ni idea bas kuwepo kwa center kwa ajili ya re education kama ilivo rehabilitation .
Kublock funding na financial transfer.
Kuboresha ulinzi na usalama kama kuwa na strong ant terrorism unit.

Kikubwa ni kuboresha maisha ya jamii na elimu.
Ukiangalia sehemu kama somalia,kenya msumbiji,nigeria, mali bukinafaso,iraq ,yemeni,pakistan,syria zote hzo kuna shida ya umasikini,elimu dunia ndogo,serikali dhaifu, ni tofauti sehemu kama Uturuki,malaysia, indonesia,algeria, Egypt
 
Umejibu vizuri sana mkuu
Pia naomba kuelewesha hivi mapinduzi ya nchi huwa yanafanikishwa vipi? Na ni point gani muhimu mtu akizishikilia tayari anakuwa amefanikisha mapinduzi yake

Na UN wananguvu kiasi gani katika kuamua mustakabali wa nchi.
Mr Chromium
 
Umejibu vizuri sana mkuu
Pia naomba kuelewesha hivi mapinduzi ya nchi huwa yanafanikishwa vipi? Na ni point gani muhimu mtu akizishikilia tayari anakuwa amefanikisha mapinduzi yake

Na UN wananguvu kiasi gani katika kuamua mustakabali wa nchi.
Mr Chromium
Mapinduzi ili yafanikiwe inabidi kuwe na saport ya jeshi, kushika chombo cha habar cha taifa, ikulu nk.
Ukimaliza vyombo vya ulinzi nchi unakua ushaichukua na upo huru kujitangaza kuwa ww ndo unashikilia nchi
 
Katika kampeni zake za urais, Trump aliahidi kumaliza mgogoro wa Urusi vs Ukreni ndani ya saa 24. Je, amefanya hivyo? Ameshapiga simu kule Kiev na Mosko? Kama bado anangoja nini? Amekutana na vikwazo vyovyote?
 
Katika kampeni zake za urais, Trump aliahidi kumaliza mgogoro wa Urusi vs Ukreni ndani ya saa 24. Je, amefanya hivyo? Ameshapiga simu kule Kiev na Mosko? Kama bado anangoja nini? Amekutana na vikwazo vyovyote?
Bado hajafika ofisini
 
Ukraine na russia —— Nato aggression au kujaribu kuizunguka russia by USA.
Russia ye ndo kaanza

Irael Vs Hamas
Huu n mgogoro wa muda mrefu
Chanzo chake ni kutokubaliana kwa waarabu na mgawanyo wa ardhi ya palestine territor
Lakini chanzo cha Octobar 7 inasadikika ulikua n mpango wa iran ili kuzuia mkataba kati ya israel na Saudi arabia.

Machafuko ya kongo
-Hizi ni coporation za ulaya na marekani ambazo zinataka kupora madini hivo zinawatumia nchi vibaraka rwanda na Uganda kuchochea machafuko ya na kutorosha madini

Machafuko ya sudan
Haya yanaanza na dikteta Al bashir ambae alitaka kuigeuza sudan kuwa nchi ya kiislam bila kuzingatia utofauti wa jamii ya sudan
Ikasababisha kujigawa kwa sudan kusini

Lakini kubagaguliwa kwa watu weusi na waarabu wa kasiskazin mwa Sudan kukafanya kuanza upinzani wa maeneo ya kodofan na dafur.
Kupambana nao akawapa silaha kundi la kabila la kiarabu la janjaweed kuvamia na kuwaua raia weusi wa sudan.

Kundi hili ndio linalokuja kujibrand kama RSF.
Kwakua al bashir alitawala kwa mkono wa chuma maandamani ya wasudan yanakua hayaishi hivo mageneral wanaamua kumpindua akisalitiwa na general pia wa kundi lake ambalo ljmekua likimlinda la rsf.

kwa uchu wa kumiliki nchi magenge au makundi haya mawili yanatofautiana kati ya rsf na jeshi la sudan wanaanza kupigana kutaka kila mtu kuchukua nchi.
Katika vita yyte bas wapambe huingia ambao huwa wanatka kufaidi nchi katika upande utaoshinda

UAE ambae alikua akiuziwa madini na RSF inatumia nafasi hii kulisapoti kundi la rsf kwa kuingiza silaha na pesa kupitia bandari za somalia

wakat huo jeshi la sudan nalo likisaidiwa na iran.

Utaka ujue kwanini RSF inakua na nguvu.

Siri ni kua inatumia vifaa vikali kutoa US ambavyo viliuzwa kwa UAE.
UAE inatumia silaha hizi kufadhili vita ya sudan.
Mkuu upo vizuri sana; naomba unieleweshe kidogo kuhusu Congo again and sorry kwa kukuchosha. Wakubwa wa dunia wanamtumia PK na Rwanda yake ili kupora madini ya Congo as you said; swali langu..., kwanini wali opt njia ya vita ambayo of course wanapata madini kwa kiasi kidogo sana, why hawakupenda option ya amani halafu waishinikize serikali ya Congo isaini mikataba ya ujenzi wa mitambo ya kisasa ili wachimbe madini hayo in a large quantity kama walivo fanya Tanzania, Botswana, Mali, South Africa, Ghana nk? Hili jambo linaisumbuaga sana akili yangu
 
Back
Top Bottom