Niwape maua yenu Wasabato, mnajua kuimba nyimbo za dini

Niwape maua yenu Wasabato, mnajua kuimba nyimbo za dini

Hilo tatizo la kufutwa nyuzi hata mimi jana lilinikumba niliweka zikafutwa bila hata kuchangiwa sijui shida nini ?

Hizo nyimbo za SDA kwaya gani zimeimba ? Unaweza weka majina ya kwaya kama utaweza tafadhali
Angalia hapa..
Upendo na yundo imeimbwa na Pillars of faith
Hoziana _ ambassador
Mungu si binaadam na chungi amalo rongo central youth choir

Screenshot_20230908-192704~2.png
 
Kwanza kabisa mwanzo wa yote wacha niweke msimamo wangu kuwa mimi sio mtu wa dini yoyote(sina dini ).

Turudi kwenye dhumuni la uzi huu ambalo ni kuwapa pongezi zao Seventh Day Adventist(SDA) kwa namna ambavyo ni mafundi haswa wa kuimba nyimbo za dini mpaka mtu ana burudika haswa.

Mimi ni mpenzi sana wa muziki, napenda miziki ya aina mbalimbali ikiwemo bolingo, hip hop, bongo fleva, Afro beats, Mziki wa south, Gospel n.k

Katika gospel napenda sana ngoma za RC na SDA kwa sababu moja tu ni kwamba hawa ni wanaimba kwaya tofauti na wengine na kwaya ina mtiririko wa sauti kuanzia 1 mpaka 4.

Sasa hawa wasabato wanajua namna ya kutiririka katika sauti hizo nne kuanzia ya kwanza mpaka ya nne zote unazipata clear kabisa na kwa kuvutia.

Hawa jamaa huwa wana nifurahisha sana na kwaya zao wanajua haswa.

Wasabato wote mliomo humu chukueni maua[emoji253] yenu kwa niaba ya wenzenu toka kwangu aisee kwaya zenu zinajua haswa maana halisi ya nyimbo za gospel zinapaswa vipi kuwa.

View attachment 2743399

Tahadhari: Huu uzi sio wa mapambano ya kidini.

Sawa wasabato wanaimba vyema, ila ukizungumzia ufundi RC wanatia fora!!!
...unaifahamu organ vizuri kweli inavyokung'utwa na mafundi wa RC!?
Halafu ujue nyimbo wanazoimba RC ukimpa anayefundisha wasabato afundishe kitakachosikika mwishoni ni discord tu!
 
Back
Top Bottom