Niwape maua yenu Wasabato, mnajua kuimba nyimbo za dini

Niwape maua yenu Wasabato, mnajua kuimba nyimbo za dini

Kwanza kabisa mwanzo wa yote wacha niweke msimamo wangu kuwa mimi sio mtu wa dini yoyote(sina dini ).

Turudi kwenye dhumuni la uzi huu ambalo ni kuwapa pongezi zao Seventh Day Adventist(SDA) kwa namna ambavyo ni mafundi haswa wa kuimba nyimbo za dini mpaka mtu ana burudika haswa.

Mimi ni mpenzi sana wa muziki, napenda miziki ya aina mbalimbali ikiwemo bolingo, hip hop, bongo fleva, Afro beats, Mziki wa south, Gospel n.k

Katika gospel napenda sana ngoma za RC na SDA kwa sababu moja tu ni kwamba hawa ni wanaimba kwaya tofauti na wengine na kwaya ina mtiririko wa sauti kuanzia 1 mpaka 4.

Sasa hawa wasabato wanajua namna ya kutiririka katika sauti hizo nne kuanzia ya kwanza mpaka ya nne zote unazipata clear kabisa na kwa kuvutia.

Hawa jamaa huwa wana nifurahisha sana na kwaya zao wanajua haswa.

Wasabato wote mliomo humu chukueni maua[emoji253] yenu kwa niaba ya wenzenu toka kwangu aisee kwaya zenu zinajua haswa maana halisi ya nyimbo za gospel zinapaswa vipi kuwa.

View attachment 2743399

Tahadhari: Huu uzi sio wa mapambano ya kidini.

Hii Post imenibariki. We share a mutual feeling. SDA’s pokeeni Maua yenu
 
Wasabato wana program nzuri sana za uimbaji..

Pia hata mambo mengine ya kimaisha.. kanisani kwao ni kama shuleni...

Kila kitu kinafundishwa kwa upana.

Mimi ni KKKT ila napenda sana taratibu za kisabato. Maana nimekulia jirani na kanisa lao.. naona kila kinachoendelea.. na siku moja moja nimehudhuria ibada zao nikawajua zaidi
 
Nachojiuliza why waimbaji wa kisabato wanakimbizwa sana sokoni na kina Rose mhando, Bahati Bukuku, Martha mwaipaja, Edson Mwasabite, Flora Mbasha, Cristina shusho etc

Hata hawa kina zablon singers wanaosemwa ni wasabato ni kama wanabahatisha bahatisha..
Ukiwawekea mziki wa kina Rose mhando wanapigwa knock out
 
Sawa wasabato wanaimba vyema, ila ukizungumzia ufundi RC wanatia fora!!!
...unaifahamu organ vizuri kweli inavyokung'utwa na mafundi wa RC!?
Halafu ujue nyimbo wanazoimba RC ukimpa anayefundisha wasabato afundishe kitakachosikika mwishoni ni discord tu!
Sawa, RC wapo vizuri pia ndio maana nimewagusia kidogo kwenye uzi
 
Back
Top Bottom