Endelea kupiga zumari ila tambua wanawake wengi mmejikuta mnaingia kwenye mkumbo wa kuomba mabaya kwa wanaume kisha hamkuolewa nao kwa mahusiano ya bahati mbaya. Ndoa ni safari haitokei ghafla tu kisa tu unajua kuzaa basi unaolewa.
Wanaume hawaio wanaojua kuzaa tu, kuna ziada mbali na kuzaa. Mbuzi nao wanazaa vilevile nao waolewe kisa tu wanajua kuzaa kama wewe.
Jengeni mahusiano yenye kuwapeleka kwenye ndoa, msijenge mahusiano ya kimalaya kisha mkayalazimisha kuwa ndoa hata mkifanikiwa kuolewa HAMTODUMU NDOANI.