Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

Nje ya mawazo ya Mwanadamu Mungu hayupo, hajawahi kuwepo, na hatakuwepo

Kama ubaya ni matokea ya uasi maana yake ni kwamba wema ulikuepo kabla ya ubaya na kama tayari wote tumekubali kuongelea mambo ya creation basi wema ndio umetoka kwa Mungu
Fatilia mtiririko wa maswali yangu na majibu yako Kuna kitu utagundua..😃
 
JE MUNGU YUPO??

KAMA YUPO KWANINI WATU WANAPITIA KATIKA MAGUMU KAMA MAGONJWA, UMASKINI, LAAMA, MIKOSI N.K

#Jibu
Jamaa mmoja alikwenda saluni kunyolelwa.
Akiwa anaendelea kuhudumiwa (kunyolewa) akawa anapiga stor na kinyozi
Stori zao zilikuwa nzur na walizungumza mambo mengi sana bila kupishana kauli
Lakini pindi mteja alipogusia habari za neno la Mungu kinyozi akasema "hebu tuachane na hizo stori maana mimi siamini kama Mungu yupo"
"Kwanin unasema hivyo?" Mteja akauliza
Kinyozi akasema "kwa ushauri wangu ni bora uende huko nje na ukawatangazie watu ya kwamba Mungu hayupo"
Na akaendekea akisema "Hebu niambie
-kama mungu yupo kwann ukienda mahospitalini utakuta watu ni wangonjwa?
-Kama mungu yupo kwann ukienda huko mitaani unakuta kuna watoto omba omba?
-Kama mungu yupo kwann ukienda magerezani unakuta watu wamefungwa kwa kuonewa?
"Hivi unafikiri kama Mungu angekuwepo kweli angeruhusu mambo yote haya?"

Mteja akafikiria kidogo na kumuomba Roho Mtakatifu kimoyomoyo ili amfunulie kwani alikua ana Imani sana na alitaka kumsaidia yule kinyozi arudishe Imani yake kwa Mungu na amvute kwa Bwana ila hakuweza kujibu chochote maana hakuwa na Jibu la haraka kwa wakati ule na pia alihitaji busara ya Roho wa Bwana hivyo alikaa kimya kimya akisubiri Roho wa Mungu ampe jibu na hekima ya kumjibu
Na Kinyozi alipomaliza kumnyoa, Mteja akaenda zake akiwa anatafakari swali lile aliloulizwa.

Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake mteja akakutana na mtu mmoja akiwa na nywele ndefu, chafu huku ndevu zake zikiwa nyingi kupita kawaida kwa ujumla alikuwa ni mchafu.

Ndipo akagundua kwamba Roho wa Mungu alikua Kamjibu kwani kwa kupitia Mtu yule alipata hekima ya kumjibu vyema yule kinyozi aliyevunjika moyo na kupoteza imani yake.

Mteja akaamua kurudi saluni kwa mara nyingine na kusema "unajua nn? Vinyozi hawapo"

"Kwann unasema hivyo?" Kwa mshituko kinyozi akauliza "si mimi hapa kinyozi na muda si mrefu nimetoka kukunyoa"
“hapana!” mteja akasisitiza. "Vinyozi hawapo kwa sababu Kama wangekuwepo kusingekuwa na watu wenye nywele ndefu,chafu na ndevu nyingi kupita kawaida kama mmoja niliyemuona huko nje.”

Kinyozi akasema; “Ah, vinyozi tupo ila kinachotokea ni kwamba watu hawajataka kuja saluni ili tuwanyoe.”
“Sawa kabisa”- mteja akakazia;

“Hiyo ndo pointi niliyokuwa nikiisubiri.”

Mungu pia yupo;

Ila kinachotokea ni kwamba watu hawamfuati yeye na nyoyo zao bado hazijafunguka kwaajili ya kuutafuta utetezi na uponyaji wake.
Ila kama watu wakimtumainia yeye kwa roho na kweli huku wakimfanya kuwa ndiye mlinzi, mponyaji na mtetezi wao.
Amini watakuwa salama maana hakuna jambo gumu yeye asiloliweza.

Watu wengi tumeshindwa kujua majibu yetu halisi au kutambua ishara tunapojibiwa na Mungu kupitia Roho wake kutokana na uzito wa akili zetu kwani tumekua tukichanganywa na hisia za Milango yetu ya fahamu...

Mfano
-Unaweza kujiona upo tayari kuanza huduma lakini je Roho wa Mungu kakujibu au kakuruhusu kuanza hiyo huduma?
au unataka upande madhabahuni kuhubiri lakini je Roho wa Mungu kakuruhusu?
_________________________________
MAOMBI.
Kwa Jina la Yesu Kristo namuomba Roho wa Mungu Akupe hekima na Majibu sahihi pale unapojikuta katika wakati Mgumu wa kukosa Majibu na akaifanye akili yako iwe nyepesi kutambua ishara na hekima zake
Amina
____________________________________
Kama una amini kwamba Mungu yupo na una imani ipo siku atakushindia dhidi ya magonjwa,umaskini,laana ,kuonewa,kudharauliwa, na magumu yote unayopitia katika maisha yako Comment "AMEN"Kudhihirisha uwepo wake katika maisha Yako na Mungu wa Mbinguni atakujibu sawa sawa na Ukiri wako.
 
Hapana mkuu Mungu sio mbaya bali anatambua uwepo wa ubaya

Ubaya umekuwa dedicated kwa devil so mbali na uwepo wa Mungu usisahau kwamba shetani pia yupo

Pointi yangu ilikuwa hii hapa! namna pekee ya kuprove uwepo wa Mungu ni kutenda matendo mema na ndilo jibu jepesi unaweza toa kwa mtu ambaye sio beliver.

Tofauti na hapo ukianza kumsomesha vifungu vya vitabu vya kidini mtakesha make dini haina mpango wa kuaccommodate reasoning na sababu kubwa ni kuwa vile vitabu vinaeleza ukweli kwahiyo no room for reasoning instead we do believe, that is when faith take over.
Kutenda matendo mema hakuthibitishi uwepo wa Mungu, kunathibitisha ni jinsi gani ulivyopevuka kiakili au kustaarabika

Belivers na non believers wote wanauwezo wa kutenda mema au kutenda maovu, hii sio ushahidi wa misimamo yao

In fact, non believers wanaweza kuwa true zaidi kwa mema yao kwa sababu hawa expect zawadi yoyote ina return

Tajiri anayejenga msikiti akiamini atapata thawabu siku ya mwisho ni tofauti sana na Non believers anayetoa misaada ya chakula kwa wakimbizi, huyu hatarajii chochote in return

Buddhism ni imani kubwa na ya mda mrefu iliyojikita kwenye 'humanity' na hakuna concept ya Mungu

Pia the so called 'vitabu vya Mungu' haviruhusu questioning sio kwa sababu vimejaa obvious facts, ila ni kwamba havina fact

Thus why, mnasema mna amini Mungu yupo(faith), na sio mnajua mungu yupo (fact)

Please refer definition ya 'faith'

"Belief in absence of evidences(facts)
 
Sababu 10 Kuamini Mungu Yupo​

Mungu yupo na sababu za kuamini zipo.

Sababu zimeandikwa mbinguni na duniani kwa herufi kubwa kiasi kwamba kila aaminiye aweza kuzisoma; nimesema, kila aaminiye aweza kuzisoma.

Nikwambie mapema, sina ushahidi wa kumthibitishia asiyeamini uwepo wa Mungu hata asiweze kuutafsiri vinginevyo; kama vile nisivyoweza kumwaminisha asiyetaka kuniamini ninampenda hata asiweze kunichukulia tofauti. Katika mahusiano ya kuamini na kuaminia (iwe Mungu au mtu), imani hutangulia ushahidi jinsi msingi unavyoanza chini kabla ya nyumba kuja juu yake.

Pasipo msingi wa imani hakuna ushahidi unaosimama.

Katika ulimwengu wa asili zipo alama za mikono ya Mbunifu zinazoonesha uumbaji umebuniwa kwa kusudi na haukuibuka kwa bahati.

Unataka uzione? Kwa ufupi wa wakati na udogo wa nafasi, niruhusu nikuoneshe kumi tu.

Hizi hapa.

1. Kilichoanza huanzishwa na Muanzilishi

Kila kitu ulimwenguni kina mwanzo ulioanzishwa.

Aya hii ipo hapa kwa kuwa mwandishi alimwaga wino juu ya ukurasa huu.

Nani aliye hai ambaye hakupokea uhai toka kwa wazazi?

Ni mama yupi anayepasisha kwa wanawe uhai ambao hakuupokea kutoka kwa waliomtangulia?

Mwanzoni mwa mapokezano hayo ya uhai yupo nani kama si Yeye Aliye na uzima, uzima usio wa kupewa au kuazimwa?

Pasipo Mwenye-kitabu hakuna kitabu cha kuazimwa.

Tuna uhai wa kuazimwa kwa kuwa yupo Mwenye uhai aliyetuazima.

Yeye daima "hapatikani na mauti" (1Tim 6:16); na "ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu" (Matendo 17:28)

2. Mabadiliko huletwa na Mbadilishaji

Vitu vyote hubadilika: iwe mata (matter) au nguvu (energy), wakati (time) au nafasi (space).

Mwenye hekima mmoja alisema vizuri, ‘hakuna kisichobadilika isipokuwa badiliko lenyewe.”

Kwa kutazama kwa macho au darubini, vitu vina uwezekano wa kubadilika na si uwezo wa kubadilika.

Mchanga huhamishwa na upepo na ua ukaushwa na jua.

Uwezo wa kubadilika hutoka nje ya kitu husika.

Kwa kuwa ulimwengu katika ujumla wake unabadilika, basi yupo Mleta-mabadiliko nyuma yake.

Kama hayupo Mbadilishaji basi ulimwengu ungebakia ulivyokua daima. Mleta-Mabadiliko Mkuu wa ulimwengu yupo, yeye habadilishwi na habadiliki.

Biblia inamtaja huyo kama,"Baba wa mianga; [ambaye] kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka" (Yakobo 1:17; lingasha na Malaki 3:6; Waebrania 3:18; Zaburi 102:24-27)

3. Sanaa humtangaza Msanii

Ulimwengu ni sanaa iliyobuniwa.

Tupia macho nyota za angani au maua ya kondeni. Ni nini mbele yako? Si uzuri huo? Aidhaa uzuri huo umebuniwa na mbuni aliyejipanga au umeibuliwa na mlipuko usiokusudiwa (wanafizikia wauita, “big bang”).

Lakini, iweje mlipuko usiopangilika uzue maumbile yaliyopangilika?

Waweza kuamini herufi hizi usoni mwako ni matokeo ya wino uliojimwagikia badala ya binadamu aliyefikiria?

Daima, sanaa hubuniwa na kubakia mali halali ya msanii. Kufurahia uvumbuzi na kutomtambua mvumbuzi ni nini kama si ubakaji wa sanaa, ukatili kwa msanii, na ukiukwaji wa haki ya msanii kutambulika? “Kwa sababu mambo yake [Mungu]….yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru” (Warumi 1:20😉

4. Hali ya kutambua/ kutambulika yatoka kwa Mwasisi-Mtambuzi

Ulimwengu uliobuniwa unatambulika.

Kilimanjaro ya theluji au ngorongoro ya kijani yatambulika kwa macho.

Ijapokuwa tunautambua ulimwengu lakini wenyewe haujitambui.

Mata (matter) na nguvu (energy), mwamba na umeme, kompyuta na roboti havijitambui.

Havina utambuzi wa nafsi.

Haviwezi kutambua nafsini kwa kufikiri, kusikiliza, kukumbuka, kuongea, kuhisi, kuhiari, na hapo hapo kung’amua walichokitambua.

Mwanadamu anatoa wapi utambuzi huo?

Kama gesi iliyojilipukia (“big bang”) ilizua wanadamu wenye utambuzi, iweje chanzo kisichojitambua (mlipuko) kitofautiane na zao lake linalojitambua (mtu)?

Hakika, wanadamu wenye ufahamu wametoka kwa Muumba mwenye-ufahamu. Mtu anamtambua Muumba na Muumba anamtambua mtu—wawili wanafahamiana hata kama wachukua muda kujuana.

Mungu ndiye "akiisha kuwawekea walimwengu nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu." (Matendo 17:26b,27)

5. Wazo lenyewe linaakisi uhalisia wake

Wanadamu wote wanamuwazia Mungu. Waumini, wasioamini, au wanaodai hawajui kuwa Mungu yupo huwa wanachukua msimamo wao baada ya kuingiwa na kupambana na wazo lenyewe.

Lakini, wazo linatua kichwani likitokea wapi? Aidha wazo limetoka ndani ya mtu au nje. Tujuavyo, chanzo huwa kikuu kupita matokeo yake (Mjapani ni mkuu kuliko Toyota).

Kwa kuwa “Mungu” wa vichwani mwao hufikiriwa kuwa mkuu (katika wema, uweza na busara) kuliko yeyote wanayemjua (kuliko baba au mama), basi dhana ya uwepo wa Mungu ni akisi ya uhalisia uliopo nje ya vichwa vyao.

Dhana haikuibuka vichwani mwao kama uyoga.

Kutoka nje, Mungu ameweka, "milele ndani ya mioyo" yao.

Ndiyo maana, pamoja na mahangaiko ya kitambo na wakati uliopo, kwa kujua au kutokujua, watu wote huangaikia umilele, hatima yao baada ya maisha yao duniani (Mhubiri 3:11; Matendo 17:26,27).

6. Usemi ‘Mungu yupo’ hudai uwepo wa Mungu

Usemi wowote uletao maana hupangika kisarufi bila kugongana kimantiki. "Duara ni pembe tatu" Sarufi? Sawa. Maana? Hakuna. “Mungu hayupo” huangukia hukumu hiyo hiyo.

Vichwani mwetu, "Mungu" ni Yeye astahiliye kuabudiwa kwa kuwa ni Mkamilifu katika uweza na uadilifu. “Mungu” ataitwa Mungu kwa kuwa yupo. Mrembo aliyeko kwenye jeneza si mrembo, na “Mungu” asiyekuwepo si “Mungu.”

Kusema, ‘"Mungu” hayupo’ ni kumhesabu Aliye hai miongoni mwa wasio hai. Mtu huthubutu vipi kusema “Mungu hayupo” kama hajateleza ulimi pasipo kujitambua? (Zaburi 51:1-2;14:1-2).

“Duara ni nyuzi 360” na “Mungu yupo” ni tungo mbili sahii kwa muundo na maana zake.

7. Kufahamika kwa maadili hutangaza Mtunzi wake

Yapo maadili-msingi yanayotambuliwa na watu wa kila zama na kila mahali. Japo wanaishi mbele ya utisho wa kutoweka na kila huyo akipambana abakie, watu wote wanajua nafsini mwao kutunza uhai wa wengine ni muhimu kuliko kuupoteza, kuonesha huruma ni bora kuliko ukatili, urafiki kuliko usaliti.

Wanaafiki heshima yafaa kuliko dharau, ushujaa kuliko woga, bidii kuliko uvivu, ukweli kuliko uongo, kutakiana heri kuliko kuoneana wivu, na kuridhika kuliko kutamani. Kufahamika kwa maadili yanayofanana ulimwengu kote ni uthibitisho wa uwepo wa mtunzi wake mmoja.

Baba wa mema yote amewaachia wanadamu kanuni 10 za namna ya kuishi na akaziandika kwa wino usiofutika (Kutoka 20; Warumi 2:14,15). Maadili ya Bwana Mungu hutia mjinga hekima na kumpatia raha moyoni.

Sheria yake ni kweli na haki. Tena ni tamu kuliko asali na hutamanika kuliko dhahabu safi (Zaburi 19:7-14).

Kwa nini kizuri kisijitangaze?

8. Sauti ya dhamira inayohukumu ushuhudia hakimu anayehukumu

Tofauti na wanyama, mwanadamu mwenye ufahamu ana dhamira inayomsonda au "sauti ndogo" nafisini. Sauti hii hujuza mema ("fanya hivi") na mabaya ("usifanye hivyo"). Kama ladha ilivyo kwa vyakula ndivyo dhamira ilivyo kwa maadili.

Dhamira uhukumu: umtetea mtu na kumletea amani; pengine, umshutumu na kumletea huzuni. Hata isemaje, watu wote hukubali ni vema kutii dhamira yako. Lakini, dhamira imepata wapi mamlaka hayo ya kusikilizwa?

Kutoka maumbile yangu asilia? Iweje asili iliyo chini yangu inikalie? Iweje nihuzunike ninapoiasi ikiwa mimi ndiye niliyeitunga?

Kama imepewa mamlaka na jamii iliyonilea, iweje wana jamii walio sawa nami wawe juu yangu?

Ni nani aliye na sauti ya mwisho kunipeleleza niliye chini, halafu kuniruhusu au kunikataza kabla sijatenda, kunitetea au kunishtaki baada ya kutenda? Hakika, "pumzi [neshamah kiebrania, au roho, dhamira,] ya mwanadamu ni taa ya Bwana; hupeleleza yote yaliyomo ndani yake" (Mithali 20:27)

9. Tamaa ya asili hutimizwa na kitu halisi

Kila hitaji asilia hutimizwa na kitu halisia.

Njaa huzimwa na chakula. Upweke humalizwa na mpenzi.

Kwa kila haja ya kimambile lipo jibu nje ya maumbile husika.

Lakini ipo tamaa ya kibinadamu isiyoweza kutoshelezwa na mazingira ya mwanadamu.

Elimu ya kidunia na ajira mali na madaraka na mapenzi haviwezi kukidhi haja hiyo.

Nani asiyetamani kufurahia ua lisilonyauka, muziki usiochuja, na upendo usiopoa.

Nani hana hamu ya kukutana na rafiki pasipo kuagana, kucheka pasipo kulia, na kuzaliwa pasipo kufa? Nani asiyependa kuongea na kusikilizwa, kugusa na kuguswa, kujua na kujulikana, na kupenda na kupendwa.

Shauku ya kufaidi uzima katika ukamilifu wake ni kiu halisi ya ulimwengu huu na utimizo wake hupatikana katika uhalisia wake nje ya ulimwengu. Zaidi ya ulimwengu upo uhalisia, Mungu Baba halisi, utimilifu wa tamaa ya vizazi vyote.

"Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga,...” (Yakobo 1:17)

10. Uzoefu wa wengi ni ushuhuda wa nguvu

Historia na anthropolojia hushuhudia kuwa uzoefu wa dini ni wa kiulimwengu. Watu wa kila zama na tamaduni wamedai kuwa na uzoefu na "Uungu." Wamemkaribia “Mungu” kwa kusujudu, kuheshimu, kusifu, na kushukuru. Je! Yawezekana waabudu wote hao wanainama kiti kilicho tupu? Kwamba uzoefu wanaoujua sio halisia? Kweli, hapo kale walimwengu wengi walijua kimakosa kuwa jua linaizunguka dunia.

Lakini uzoefu wao ulikuwa sahii. Kwa uzoefu walijua bila kukosea kuwa jua lipo, dunia ipo na mzunguko upo.

Huenda waabudu wakakosea kujua Mungu yukoje, lakini haiwezekani wakakosea kujua yupo.

kiwa wengine hawajui uzoefu unaojulikana sana, huenda shida ni mishipa ya fahamu, mishipa iliyopoteza uwezo wake wa kuhisi na kujua. “Kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.” (Warumi 1:21)

Picture

Hauko mwenyewe kama ungali unasita kuamini Mungu yupo. Lakini ikiwa yupo, Mungu aliye na uwezo wote na wema wote, basi utajiumiza mwenyewe usipomwamini. Ukimkataa, utakuwa unakataa uzima na upendo.

Wapo waliotafuta kumjua Mungu na kumpata; wakawa na hekima na furaha. Wapo waliotafuta kumjua na kumkosa; wakaonekana wana “hekima” lakini hawana furaha. Na wapo wasiomtafuta na wamepungukiwa hekima na furaha. Kuamini ni kuchagua. Ikiwa utachagua kuamini Mungu yupo, uwezekano wa kupata maana ya maisha upo. Yesu Kristo amekwisha sema, “tafuteni, nanyi mtaona” (Mathayo 7:7).

Kama unataka kumjua Mungu binafsi, lakini unaona woga, waweza kuomba ombi hili: “Mungu, sijui kama unaishi au la, lakini kama upo, tafadhali jifunue kwangu jinsi ulivyo.”
 
Kutenda matendo mema hakuthibitishi uwepo wa Mungu, kunathibitisha ni jinsi gani ulivyopevuka kiakili au kustaarabika

Belivers na non believers wote wanauwezo wa kutenda mema au kutenda maovu, hii sio ushahidi wa misimamo yao

In fact, non believers wanaweza kuwa true zaidi kwa mema yao kwa sababu hawa expect zawadi yoyote ina return

Tajiri anayejenga msikiti akiamini atapata thawabu siku ya mwisho ni tofauti sana na Non believers anayetoa misaada ya chakula kwa wakimbizi, huyu hatarajii chochote in return

Buddhism ni imani kubwa na ya mda mrefu iliyojikita kwenye 'humanity' na hakuna concept ya Mungu

Pia the so called 'vitabu vya Mungu' haviruhusu questioning sio kwa sababu vimejaa obvious facts, ila ni kwamba havina fact

Thus why, mnasema mna amini Mungu yupo(faith), na sio mnajua mungu yupo (fact)

Please refer definition ya 'faith'

"Belief in absence of evidences(facts)
Mkuu nimekupata vizuri ila naomba niende break kidogo nikiwa na deni la kuja kujibu hizi hoja vizuri

Pili niseme kuwa bado ahadi yangu ni kuwa after two years I will be here with something tangible na ikitokea sijarudi basi tambua safari yangu itakuwa imeishia njiani.

Moreover, thank you and everyone for this debate.
 
Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama unaumwa na huponi au una shida milioni bado Mungu anabaki kuwa Mungu
 
JE MUNGU YUPO??

KAMA YUPO KWANINI WATU WANAPITIA KATIKA MAGUMU KAMA MAGONJWA, UMASKINI, LAAMA, MIKOSI N.K

#Jibu
Jamaa mmoja alikwenda saluni kunyolelwa.
Akiwa anaendelea kuhudumiwa (kunyolewa) akawa anapiga stor na kinyozi
Stori zao zilikuwa nzur na walizungumza mambo mengi sana bila kupishana kauli
Lakini pindi mteja alipogusia habari za neno la Mungu kinyozi akasema "hebu tuachane na hizo stori maana mimi siamini kama Mungu yupo"
"Kwanin unasema hivyo?" Mteja akauliza
Kinyozi akasema "kwa ushauri wangu ni bora uende huko nje na ukawatangazie watu ya kwamba Mungu hayupo"
Na akaendekea akisema "Hebu niambie
-kama mungu yupo kwann ukienda mahospitalini utakuta watu ni wangonjwa?
-Kama mungu yupo kwann ukienda huko mitaani unakuta kuna watoto omba omba?
-Kama mungu yupo kwann ukienda magerezani unakuta watu wamefungwa kwa kuonewa?
"Hivi unafikiri kama Mungu angekuwepo kweli angeruhusu mambo yote haya?"

Mteja akafikiria kidogo na kumuomba Roho Mtakatifu kimoyomoyo ili amfunulie kwani alikua ana Imani sana na alitaka kumsaidia yule kinyozi arudishe Imani yake kwa Mungu na amvute kwa Bwana ila hakuweza kujibu chochote maana hakuwa na Jibu la haraka kwa wakati ule na pia alihitaji busara ya Roho wa Bwana hivyo alikaa kimya kimya akisubiri Roho wa Mungu ampe jibu na hekima ya kumjibu
Na Kinyozi alipomaliza kumnyoa, Mteja akaenda zake akiwa anatafakari swali lile aliloulizwa.

Akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake mteja akakutana na mtu mmoja akiwa na nywele ndefu, chafu huku ndevu zake zikiwa nyingi kupita kawaida kwa ujumla alikuwa ni mchafu.

Ndipo akagundua kwamba Roho wa Mungu alikua Kamjibu kwani kwa kupitia Mtu yule alipata hekima ya kumjibu vyema yule kinyozi aliyevunjika moyo na kupoteza imani yake.

Mteja akaamua kurudi saluni kwa mara nyingine na kusema "unajua nn? Vinyozi hawapo"

"Kwann unasema hivyo?" Kwa mshituko kinyozi akauliza "si mimi hapa kinyozi na muda si mrefu nimetoka kukunyoa"
“hapana!” mteja akasisitiza. "Vinyozi hawapo kwa sababu Kama wangekuwepo kusingekuwa na watu wenye nywele ndefu,chafu na ndevu nyingi kupita kawaida kama mmoja niliyemuona huko nje.”

Kinyozi akasema; “Ah, vinyozi tupo ila kinachotokea ni kwamba watu hawajataka kuja saluni ili tuwanyoe.”
“Sawa kabisa”- mteja akakazia;

“Hiyo ndo pointi niliyokuwa nikiisubiri.”

Mungu pia yupo;

Ila kinachotokea ni kwamba watu hawamfuati yeye na nyoyo zao bado hazijafunguka kwaajili ya kuutafuta utetezi na uponyaji wake.
Ila kama watu wakimtumainia yeye kwa roho na kweli huku wakimfanya kuwa ndiye mlinzi, mponyaji na mtetezi wao.
Amini watakuwa salama maana hakuna jambo gumu yeye asiloliweza.

Watu wengi tumeshindwa kujua majibu yetu halisi au kutambua ishara tunapojibiwa na Mungu kupitia Roho wake kutokana na uzito wa akili zetu kwani tumekua tukichanganywa na hisia za Milango yetu ya fahamu...

Mfano
-Unaweza kujiona upo tayari kuanza huduma lakini je Roho wa Mungu kakujibu au kakuruhusu kuanza hiyo huduma?
au unataka upande madhabahuni kuhubiri lakini je Roho wa Mungu kakuruhusu?
_________________________________
MAOMBI.
Kwa Jina la Yesu Kristo namuomba Roho wa Mungu Akupe hekima na Majibu sahihi pale unapojikuta katika wakati Mgumu wa kukosa Majibu na akaifanye akili yako iwe nyepesi kutambua ishara na hekima zake
Amina
____________________________________
Kama una amini kwamba Mungu yupo na una imani ipo siku atakushindia dhidi ya magonjwa,umaskini,laana ,kuonewa,kudharauliwa, na magumu yote unayopitia katika maisha yako Comment "AMEN"Kudhihirisha uwepo wake katika maisha Yako na Mungu wa Mbinguni atakujibu sawa sawa na Ukiri wako.
Asante kwa kisa kizuri cha Kinyozi na mteja wake.

Hakuna mmoja kati yao (Kinyozi, au mteja. Rejea ya kisa chako) aliyeweza jenga hoja yake kwa ufasaha

Kinyozi alikua ana rejea 'Problem of Evil' kimakosa huku Mteja akitumia 'Argument from the free will' ambayo imemulika aspect moja tu tatizo

Kwa kinyozi, Fact kuwa kuna wagonjwa hospitali sio direct proof kuwa hakuna Mungu

Ni proof kuwa tunaishi kwenye dunia yenye pathogens
Dunia yenye magojwa

Hoja ilibidi iwe hivi, Kwanini Mungu aliumba Dunia iliyojaa backeria, viruses, na natural causes zote zinazo sababisha Magojwa

Kwanini Mungu aliumba Dunia yenye Tsunami au Matetemeko ya Ardhi

Hii haina mahusiano kabisa na 'Free will ya binadamu'
Tsunami haijali upo karibu na Mungu wako kiasi gani itapiga tu,

Kuna maovu mengi hayana mahusiano na free will ya binadamu

Hoja ya mteja imejikita kwenye aspect moja tu ya tatizo, kuna maovu yanayosababishwa na free will ya binadamu na kuna yapo natural

Swali ni kwanini Mungu mwenye upendo wote na uwezo wote na ujuzi wote aumbe ulimwengu wenye Ebola, Tusnami, Matetemeko ya Ardhi,Mbu wa malaria, etc
Hivi vyote havisababishwi na binadamu
 
USIWE NA WASIWASI NIKIPATA MUDA KESHO AU KESHO KUTWA JUMAPILI NITAKUJIBU

KWA SASA NAZIMA KOMPYUTA NAENDA KUPUMZIKA NA MKE WANGU NA FAMILIA YANGU, NAKUTAKIA WEEKEND NJEMA
 
USIWE NA WASIWASI NIKIPATA MUDA KESHO AU KESHO KUTWA JUMAPILI NITAKUJIBU

KWA SASA NAZIMA KOMPYUTA NAENDA KUPUMZIKA NA MKE WANGU NA FAMILIA YANGU, NAKUTAKIA WEEKEND NJEMA
Nawe pia Mkuu,
 
Nikupe heko kwanza kwa kugundua udhaifu wa kutumia vitabu vya dini ku prove uwepo wa Mungu
(Circular Argument)

Pia kabla huja prove uwepo wa Mungu, ni busara kama ukitoa tafsiri yako ya neno Mungu

Mungu sio neno lenye maana moja, ku avoid ambiguity, mmoja anapaswa kutoa tafsiri yake ya neno hilo

Nakupa mfano, Mwanasayansi Professor Albert Einstein, alipoulizwa na wanafunzi wake kama anaamini juu uwepo wa Mungu

Alijibu ndio,kuwa anaamini Mungu yupo

Mkristo au muislam, anaweza kufurahi juu ya kisa hiki kwa kugundua kuwa kumbe mwanadamu mashuhuri namna hii anaamini Mungu yupo, mimi ni mjinga kiasi gani nipinge?

Ila ukitafuta tafsiri ya neno Mungu kulingana na Einstein ni tofauti kabisa, kiufupi ni kinyume cha na maana ya neno Mungu kwa mujibu wa imani ya kikristo au kiislamu

Albert Einstein aliamini Mungu ni 'summation of all laws of physics'
Mungu ni mkusanyiko wa sheria zote za asili, kwa maana nyingine Mungu ni just concept tu, abstraction ya jinsi gani Ulimwengu unafanya kazi

Kwa mkristo anayeamini Mungu mwenye hisia, aliyeumba kila kitu kwa kusudi, yaani Personal God. Hii ni habari mbaya kwake

Umeona hapo, kundi la watu ambao mwanzoni tunaona wanakubaliana, kumbe kiuhalisia wanatofautiana kwa 100%

Pia kwenye hoja yako sioni premise inayo justify hitimisho lako juu ya uwepo wa Mungu kupitia wema na ubaya

Ukirejea 'Problem of evil' utaona hivyo vitu viwili (Good and Evil) ndio vinatumika kuthibitisha kuwa Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuwepo kwenye ulimwengu wenye kila aina ya maovu na natural calamities kama huu
Kwa sababu kwa upendo wote asingeruhusu mateso yatokee, kwa uwezo wote asingeshindwa, na kwa ujuzi wote angekuwa na njia bora zaidi ya kuuepuka

Mungu mwenye upendo wote kwa viumbe vyake hawezi kuumba 'Mbwa mwitu' wanaokula nyama ya Swala mjamzito akiwa hai... Huo ni mfano wa natural cruelty iliyopo kwenye animal kingdom
Unless uwe unaamini wanyama hawahisi maumivu Mungu bado watu wengi hawaelewi nini hasa maana ya Neno Mungu. Bahati mbaya kabisa vitabu vitakatifu havielezi Mungu ni nini.
 
Moja ya tabu ninayopata ni kuambiwa nisiamini holly books zilizoletwa na ndege na meli lakin niamini history waliondika watu miaka milliions iliyopita.
Hivi hizo history zina ushahidi wa kuaminika kweli? Au ilimradi tuchanganyane tu hapa dunian?
 
Mijadala yote kuhusu Mungu ambayo ninaiona humu huwa ni mabishano tu, ambayo yote si ya kitaaluma na weledi.

Hii ni kwa sababu huwezi kudai Mungu hayupo au yupo kama hujajibu swali: Mungu maana yake ni nini?

Tazama kwa mfano, madai ya mtoa hoja hapa, hakuna mahali popote alipofafanua Mungu ni nini, badala yake amesema ni mawazo ya binadamu.

Hata hayo mawazo anayoyasema pia hajayafafunua! Mathalani nini kinafanya mtu awe na mawazo hayo? Je, ni mapokeo? Au ni nini?
 
Wao wanatumia theory zao kupinga.. Mimi nikitumia Maandiko ya Vitabu vitukufu Wanakataa.

Utawasikia hivyo vitabu wameandika watu kama wewe.. kwani hizo theory walitunga wanyama kama fisi?

Mwingine anakuja na ID zaidi ya moja kupinga uwepo wa Mungu, lakini anasahau tone ya matamshi (mwandiko wake) ni ileile..

Ibilisi najua upo kazini, Lakini na Mungu naye yupo Hapahapa..

Tumia theory nitumie Neno, ukija kwa blah blah.. utapata blah blah.

LIHIMIDIWE JINA LAKO MUNGU WETU, ULIYEUMBA ULIMWENGU NA VYOTE VILIVYOMO.. AMINA.
 
Watu waliokufa Wana majibu yote, kama Kuna mtu alikufa akarudi atuelezee
 
Back
Top Bottom