Ukitaka kutumia theory (MIMI NAKURUHUSU), Mimi nitatumia Neno La Mungu (Na wewe niruhusu)..
Ukishindwa hiyo..
Tumia blah blah (MIMI NAKURUHUSU) na Mimi nitatumia blah blah (Niruhusu Tafadhali)... Hahahahah.
Ukitaka shiriki kwa faida ya ubongo wako, Usipotaka Susa ubaki na giza lako.
Kwa Yesu kuna amani ipitayo amani zote, Karibu mpendwa...
NB..
Nakuruhusu, Tumia kitabu chako cha dini ku prove uwepo wa Mungu wako
Lakini kabla ya yote, kuna Maelefu ya Dini na imani tofauti tofauti Duniani na kila imani ina mitume au watu wake wanaoaminiwa kuwa na 'highest authority' na pia kila imani ina some sort of holly scripture inayoheshimiwa na imani
Haya maswali ni muhimu kuya address kwenye hoja yako
1.Kati ya hizo thousands religions, na holly scriptures kwanini dini yako wewe (Ukristo) na kitabu chako cha dini (Biblia) ni sahihi kuliko nyingine (zisizo sahihi)
NB: Kwasababu Mungu lazima awe mmoja, na haiwezekani kwa Mungu mwenye nia ya kutaka binadamu wote wamfahamu na kumwabudu, aanzishe dini nyingi zinazopingana kwenye hoja za msingi
Assumption yetu ni kwamba, kama umeona ukristo ni dini sahihi, na biblia ndiyo kitabu kitakatifu pekee na Mungu wa kwenye biblia (Agano jipya na kale) ndiye Mungu sahihi
Basi ni lazima utupe justifications kwanza kwanini Ukristo na Biblia na sio Uislam au Quran au dini nyingine elfu
Hapa napenda kukazia kitu muhimu, kwa kuwa utaamua kutumia kitabu chako cha dini basi hata tafsiri ya neno Mungu kwako inapaswa kuwa Strict
Mfano Generally, kwa dini za uyahudi, ukristo na uislamu
Mungu anajulikana kama mwenye nguvu zote, upendo wote na ujuzi zote
Hizi ndio sifa kuu za Mungu, ambazo hata moja ikiondoka kati ya hizo sio Mungu tena
Sasa unapotumia Biblia kuthibitisha uwepo wa Mungu wako, kutumia hio tafsiri haitoshi kwa sababu haito tenganisha Mungu wako 'Jehovah ' na 'Allah' Mungu wa imani ya kiislamu
Wote wana share tafsiri moja ya hapo juu, wote wana nguvu zote, ujuzi wote na maarifa yote
Hivyo hawawezi kutokea kwa pamoja, ni either Jehovah yupo na Allah hayupo au Allah yupo na Jehovah hayupo
Au aidha Ukristo ni imani sahihi na uislamu sio sahihi au vice versa
Na usiseme Allah na Jehovah ni kitu kimoja, tofauti yao ni misconception tu ya hizi dini mbili
Hapana, Jehovah na Allah ni miungu miwili tofauti kwa mujibu wa Biblia na Quran
Jehovah ana nafsi tatu za uungu, Allah ana nafsi moja pekee
Jehovah hamtambui mtume Muhammad ila Allah anamtambua
Jehovah anaitambua israel kama taifa teule ila Allah halitambui
Sasa utapotumia kutabu chako cha dini kuthibitisha uwepo wa Mungu wako lazima upite kwanza hii Filter..
Kwanini Ukristo, Bibilia na Jehovah ndiyo vitu pekee sahihi kuliko imani zote zilizopo, Vitabu vyote vilivyopo na Miungu yote iliyopo?
2.Vitabu vya dini vinaaminiwa kuwa inerrant
Havina hata nukta ya kosa kwasababu viliandikwa chini ya uongozi wa Mungu mjuzi wa yote, kwa case ya dini yako 'Roho mtakatifu'
Lakini ukifanya cross examination ya biblia utagundua ina makosa mengi ya msingi ambaye yasingewezekana chini ya uongozi wa Mungu mjuzi wa yote
Galileo alifungwa kifungo cha ndani maisha kwa kosa la kukosao biblia ilipodai kuwa Dunia ndio 'center' ya mfumo wa jua, na vingine vyote kwanzia Jua lenyewe,Sayari na nyota vinaizunguka Dunia
Na hio 'Geocentric Model' ndiyo inayo hubiriwa na Biblia mpaka leo
Baada ya Galileo kuonekana sahihi, kanisa katoliki likamuomba msamaha juzi juzi miaka mingi baada ya kifo chake
Na hio ni moja kati ya mara nyingi, Biblia iliyokumbatia false theories
In fact, naweza kukupa list ya scientific errors zilizo jaa kwenye biblia
Sasa unapotaka kutumia biblia kama evidence, lazima upite pia kwenye hii Filter ya pili
Je biblia haina scientific error yoyote ukilinganisha na vitabu vingine?
Ukiacha Scientific inaccuracies zilizopo, pia kuna Internal inaccuracies
Kitu ambacho hakiwezekani chini ya supervision ya roho mtakatifu
Vitabu vikuu vitatu vya injili, Luka, Mathayo, na Marko havikubaliani na kitabu cha Yohana kuwa Yesu alikufa kabla ya Pasaka au baada ya Pasaka
Na hivyo vitatu vyenyewe bado havikubaliani kulikua na wanawake wangapi kaburini (kwa yesu)
Naweza kukupa list ya internal inaccuracies nyingi za kwenye biblia
Hio ndiyo reason ya baadhi ya watu kusema njia rahisi ya kuwa Atheist ni kusoma biblia
Kabla hajatumia biblia kuthibitisha uwepo wa Mungu wako twambie kwanza
Je biblia haina internal inconsistencies ulinganisha ni vitabu vingine vya dini
Ukitoka hapo, twambie dhehebu lako, issue sio kuwa mkristo tu
Hizo internal inconsistencies na confusions zinazotengenezwa na biblia zimezalisha madhehebu kibao yanayopingana mpaka kwenye hoja za Msingi
Wasabato hawali bata na nguruwe na wanasali jumamosi
Madhehebu mengine ya kilokole wanakula Nguruwe na bata na wana sali Jumapili
Wote hawa wanatumia version moja ya Biblia
Papa,kiongozi mkuu wa dhehebu la kikatoliki (dhehebu kubwa katika ukristo), in fact kama wingi wa waumini unashabihiana na ukweli, hili lipo karibu na ukweli
Yet Papa, hana shida kabisa na ndoa za jinsia moja
Na ana nukuu biblia hio hio
Jehovah witnesses hawaamini uungu wa Yesu kristo, na yet wanatumia same version ya biblia kuwa support
So twambie kwanza
Wewe ni dhehebu gani na kwanini la kwako ni sahihi kuliko madhehebu mengine ya kikristo
Uki address hizo issues zote basi utakua qualified kutumia biblia kama prove yako
Ukishindwa ku address hizo issue, just stick tu kwenye General definition ya neno Mungu na yet kuna hoja nyingi za kuipinga
Kuthibitisha usahihi wa dhehebu au dini yako sio rahisi kama kuhubri kanisani Mchungaji
Huko hutopata mtu wa kukuuliza maswali ya msingi, ila huku wapo
Karibu