Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kila Mwanamke ambaye huwa anampiga matukio mwanaume mwema sana kwenye jamii huwa anazitumia njia hizi zifuatazo, vilevile mwanamke mwema sana kwenye jamii huwa anajikuta kwenye mahusiano na mwanaume ambaye hapendeki.
ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO MWANAMKE AMBAYE HAPENDEKI HUWA ANAZITUMIA KUMPATA MWANAUME MWEMA SANA KWENYE JAMII
1.Kugeuka tatizo kwa mwanaume badala ya kuwa chanzo cha amani, furaha na utulivu kwa mwanaume.
mwanamke mwenye kiburi, majivuno, jeuri na dharau huwa anaijua njia hii na huwa anaifanyia kazi kisawasawa.Kwanza anakuwa na matatizo mengi sana ya kiuchumi,anataka pesa nyingi sana ndani ya muda mfupi,anakuwa na matatizo mengi sana ambayo yanahitaji pesa nyingi sana kutoka kwa mwanaume.Vilevile anakuwa haeleweki tabia wala msimamo kwa mfano anakuwa mwenye furaha sana,anaonyesha kumpenda sana Mwanaume,kumwita majina mazuri,kumsifia sana,kuonyesha nia ya kujenga naye familia kisha ghafla anabadilika anakuwa na hasira kupitiliza, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa na huzuni sana,anakuwa na upweke,anakuwa na kisirani, gubu, kununa, kususa,kutishia waachane mara kwa mara.
Hapa kwa mwanaume mstaarabu sana,mpole kupitiliza huwa anachanganyikiwa kisha huanza kuomba msamaha, kumbembeleza,kumpa ushauri,kununua zawadi za gharama kubwa sana kisha Mwanamke anaonekana kubadilika tabia kidogo kisha anakuwa na tabia za ajabu ajabu siku chache zinazokuja.
wanaume wenye tabia njema sana kwenye jamii huwa hawavutiwi kimapenzi na Mwanamke mwenye hulka ya upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa kwa sababu wao huwa wakiona Mwanamke ambaye anapenda starehe,anapenda makundi,anapenda maisha ya anasa,anapenda kunywa pombe,kwenda night club huwa wanataka kumbadilisha tabia wakiamini ndiyo atakuja kuwa Mwanamke wa ndoto zake.
Lakini inakuwa kinyume chake kwa sababu kadiri unavyotaka kubadilisha tabia ya Mwanamke ndivyo unavyozidi kumpenda na kushindwa kumuacha hata kama atafanya kosa kubwa kiasi gani unakuwa na matumaini ya kwamba atabadilika tabia aje kuwa mwema tofauti na alivyo kwa sasa.
2.KUWEKA MIPAKA NA MASHARTI MAGUMU SANA
Mwanamke ambaye huwa anampiga mwanaume matukio huwa anaijua mbinu hizi.Anasema ili niwe na wewe nataka kiasi XYX cha fedha kama hauna basi tuachane na kweli anakuwa mkali kupitiliza kama fedha hizo hajapewa na vilevile hata kama atapewa hasemi neno ahsante ili mwanaume apate hasira na aanze kujichukia, baada ya kuanza kujichukia mwanaume huanza kupoteza uwezo wa kujiamini akiwa mbele ya Mwanamke mwingine hivyo mwanaume mstaarabu sana huona mwanamke pekee ni yule ambaye haeleweki tabia.
kadiri mwanaume anavyozidi kuonekana MSTAARABU sana,anavyotaka kuonekana ni mwanaume mkamilifu, anavyozidi kutaka aonekane ni mwanaume wa ndoto za Mwanamke huyo ndivyo Mwanamke huyo anakuwa na nguvu za kumtawala mwanaume kimabavu tena inakuwa rahisi kumuacha ghafla bila kujali mwanaume anakuwa amejitoa mhanga kiasi gani kumfurahisha Mwanamke husika.
3.KUWA NA HASIRA KUPITILIZA
Mwanamke ambaye hapendeki huwa anaijua mbinu hii ya kutumia hasira kupitiliza mara kwa mara kuzuia kupishana kauli na mwanaume,endapo Mwanamke akasema nataka 1,2,3 anawahi kuonyesha uso wenye hasira kupitiliza kama ngao ya kuzuia mwanaume kupinga mawazo yake.
kwa sababu mwanaume mpole kupitiliza huwa hataki ugomvi wala migogoro ndani ya familia huwa anajikuta anakubali kwa shingo upande.Baada ya muda mwanamke huanza kuonyesha dharau waziwazi, atamsaliti kwa makusudi kisha atasema nimefanya kwa makusudi kabisa na hauna cha kufanya,haombi msamaha kwa sababu hana cha kupoteza kwani tangu mwanzo yeye ndiye alikuwa na kauli ya mwisho.
4.UCHOYO KUPITILIZA
Mwanamke ambaye hapendeki huwa anaijua njia hii,anakuwa mbinafsi sana,anakuwa mchoyo sana,anakuwa busy sana kuzuia kujenga ukaribu na mwanaume wake,simu hapokei, sms hajibu hapo mwanaume mpole kupitiliza huanza kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo,kutuma pesa kibao ili kumshawishi ampende,mwanaume anaweza kumfuata kazini au nyumbani kwao kisha atapiga magoti, kutishia kujiua,kuomba msamaha,
kumbembeleza sana hata kama hajafanya makosa yoyote.
5.KUWA "SINGLE" MUDA WOTE
Hapa mwanamke ambaye hapendeki huwa anaijua njia hii.Kwanza anakuwa na wanaume wengi sana ambao wanamfuatilia lakini anakuwa hana hisia kwa mwanaume yeyote hivyo anaangalia nani amekuwa msumbufu sana kwake ndiyo anamuomba fedha nyingi sana kwa kisingizio kwamba kama hana fedha aache kupiga simu mfululizo,au kutuma sms.
mwanaume muoga huwa anatuma fedha lakini mwanamke anakuwa hana mpango na mwanaume yeyote baina yao.
Màra kwa mara anakuwa anamkosoa, kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu mwanaume mara kwa mara ili kumfanya ashindwe kujiamini mbele yake.
sheria yake inakuwa hivi mpaka mwanaume aonyeshe kumhitaji sana kwa kutuma sms mfululizo, kupiga simu mfululizo, kutuma pesa kibao ili kumshawishi ampende,akiona mwanaume analalamika,anapitia huzuni sana kwa kunyimwa ushirikiano hapo anakubali kwa sababu anajua huyu mwanaume hana ujanja kwake,hawezi kumuacha,hawezi kuishi bila yeye.
atamjaribu mwanaume kwa kumkosea kwa makusudi kisha ataangalia kama mwanaume analalamika,kulia, kuomba msamaha kisha anajua kwamba mwanaume hawezi kumuacha.
6.KUSUBIRI MWANAUME MKAMILIFU
Mwanamke ASIEPENDEKA huwa anaweza kukaa hata miaka 36 bila mwanaume yoyote wa kueleweka.Hii inatokea kwa sababu muda mrefu anakuwa anatumia kuchagua mwanaume wa ndoto zake yaani kila siku anasema huyu mwanaume sio wa HADHI yake mpaka umri unakuwa mkubwa sana anaweza kuzalishwa na waume za watu au player boy au bad boy ambao wanampa ujauzito na kumtelekeza bila huduma zozote.
lakini akiwa na ujauzito au watoto hapo ataenda kwa mwanaume mstaarabu sana kwa ajili ya kupata faraja ya huzuni, majonzi, simanzi na upweke pamoja na mahitaji ya kifedha ili kumtunza mtoto au ujauzito ambao ametelekezwa nao.
MWANAUME AMBAYE HAJUI SIFA ZA MWANAMKE MWEMA HUWA ANATESEKA SANA MAISHA YAKE YOTE.
Zingatia kwamba kazi ya mwanaume mwema sana ni kumfariji, kumliwaza mwanamke ambaye hapendeki, mwanamke ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto.
Ikiwa wewe ni mwanaume mwema sana kabla ya kujipa majukumu ambayo kwako yatakugharimu pesa,muda na hisia, tafuta Mwanamke mwenye tabia ya upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu na kujitoa kwako endapo utashindwa kuvutiwa na Mwanamke mwenye sifa hizo basi jiandae kwenda kulia.