Kiranga hoja zako Kwa Upande Huu wa Leo zina udhaifu mkubwa katika kuelewa msingi wa haki na wajibu.
Nitafafanua kwa kutumia nadharia za kifalsafa, kijamii, na hata kisheria ili kukudhihirishia kasoro Zilizopo Ili Unielewe Zaidi..
kwanza Haki na Wajibu ni Pande Mbili za Sarafu Moja..
Wengi sana Tunaongea Kuhusu
Liberalism ila Hatuielewi kabisa
Nitamnukuu
John Stuart Mill, katika kitabu chake
On Liberty, anasema:
"The liberty of the individual must be thus far limited; he must not make himself a nuisance to other people."
Yaani "uhuru wa mtu binafsi lazima uwe na mipaka; hawezi kuwa kero kwa wengine."
Sasa Nikitoka Kuelezea Hoja Hiyo nitaenda Kukujibu swali lako uliloniuliza Mwanzoni Kuwa Nani kaweza Mipaka Hiyo..
So kama Nilivyosema Awali haki haipo peke yake bila wajibu. Kwa mfano, mtu ana haki ya kuishi anavyotaka, lakini wajibu wake ni kuhakikisha kuwa maisha yake hayavunji utulivu wa jamii (Ikiwemo Misingi ya Jamii na Tamaduni Iliyojiwekea na wala havunji haki za wengine)
Kwa hiyo, unaposema haki ya kuishi mtu anavyotaka haina mipaka, unakosea kwa sababu kila haki lazima iwe na uwiano wa wajibu ili kuwe na mshikamano wa kijamii.
Turudi Lilipokuja swa zima La wewe Kuleta Utata niliposema Mwanamke ana wajibu wa Kumtii Mumewe..
Kwanza Nadharia ya kijamii inatufundisha kuwa katika taasisi yoyote, iwe Ni Ya Kisiasa Kijamii kama ndoa, kuna mgawanyo wa majukumu ili kuwepo na utulivu.
nitamnukuu Mwanazuoni wa Socialogy na Anthropology anaitwa David Émile Durkheim anasema:
"Society is not a mere sum of individuals. Rather, the system formed by their association represents a specific reality that has its own characteristics."
(Jamii si mkusanyiko wa watu binafsi tu, bali ni mfumo wenye kanuni zake maalum.)
Sasa Kuolewa Sio Lazima Kama Ulivyosema Ila Kanuni za Kijamii Ambazo ndo msingi wa Haki zinaweka Misingi Ya Umuhimu Wa Mtu kuolewa Unless Usiwe Part ya Jamii hiyo so Kwa sasa Ndoa Imewkwa Kama Moja Ya Haki Na Jamii zetu..
So Katika ndoa, ili iweze kufanya kazi ipasavyo, kuna mgawanyo wa majukumu. Mwanamke na mwanaume wote wana haki na wajibu, na mojawapo ya wajibu wa mke ni kuheshimu mamlaka ya mumewe kama kiongozi wa familia, hasa pale ambapo majukumu yamegawanywa kwa makubaliano.
Aristotle, katika
Politics, alisema:
"
The rule of a household is a monarchy, for every house is under one head."
(
Yaani, uongozi wa familia ni wa kifalme, kwa maana kuwa kila familia ina kiongozi mmoja.)
Hii haimaanishi kuwa Badi mume Kwa Kuwa Ni monarchy awe Dictecta No, bali kwamba kuna mfumo wa uongozi wa asili unaohakikisha usawa wa majukumu. Na Ndivyo jamii zetu hasa Watanzania katika mifumo yetu ya ndoa ambapo heshima na wajibu wa kila mmoja ni muhimu.
Uliposema mwanamke hana wajibu wa kuolewa, ni kweli. Hakuna mtu anayelazimishwa kuingia kwenye ndoa,
ila Swala Linakuja Ukishaamua Kuingia Kwenyr Ndoa au kwenye Mahusiano anakuwa ameingia katika mfumo wenye haki na wajibu. (hawezi kujiamulia Kitu kwakuwa eti kuna Liberty)
Sijui kama Unanielewa???
Katika
Social Contract Theory ya Jean-Jacques Rousseau, anasema:
"Man is born free, and everywhere he is in chains."
(Yaani, binadamu huzaliwa huru, lakini kila mahali yuko katika minyororo ya jamii.)
Sasa Kiranga Unajua Hiyo Inamaanisha ninir kuwa tunapochagua kuishi ndani ya jamii au taasisi fulani (kama ndoa), tunakubali kufuata kanuni zake na Si vinginevyo..
Mwanamke akiamua kuolewa, anakuwa ameingia kwenye mkataba wa ndoa ambao unajumuisha haki na wajibu, ikiwa ni pamoja na kutii na kuheshimu mume wake kama sehemu ya mgawanyo wa majukumu.
Najua unaweza Ukasema naleta Ushamba and all staffs of Logical blah blah blah....
Namalizia Kwa Kumnukuu Hayati
Edward Said, katika
Orientalism, anaeleza kuwa:
"A society that ignores its foundational structures in pursuit of unchecked individualism risks self-destruction."
(Jamii inayopuuzia misingi yake katika harakati za kuendekeza uhuru wa mtu binafsi isiyo na mipaka inajihatarisha yenyewe.)
Kila Jamii ina Misingi yake na Kila Misingi ina Miiko yake Jamii yoyote Inayopuuza Misingi Hiyo Inahatari ys Kupotea na Kufata Misingi ya Jamii zinginr..
Extiction sio Lazima Iwe ni Upotevu wa Species tu hata Kupotea kwa Tabia, tamaduni na Miiko ya Jamii fulani Inayotambulisha Jamii Hiyo huitwa Societal extinction..
Asante!
CC:-
Manyanza