Njia gani ni bora kwa mtumishi kuhama kutoka halmashauri (local government) kwenda Taasisi zingine?

Umri unaruhusu kapige masters nje viza ukiwa mtumishi ni rahisi kupata,nauli unakopa bank.
Huku unasoma ukiwa unachek michongo mingine nje mambo yakikaa sawa unawaforwadia email ya 24hrs juu kwa juu.Ngoma ikigoma unarudi bongo na elimu yako unalipwa mshahara wa masters Sio Haba Serikalini.
Ukikomaa nje unatunza pesa ukija bongo unanunua nyumba,unarudi nje hivyo hivyo
Au unajenga apartment,hotel, viwanja hizi ndizo pension zako,ukiwa Mzee.
 
Serikali ina mkono mrefu, usijichanganye kamwe.

Kuhama Taasisi nyingine ni jambo linawezekana wala halihitaji hata kusoma tena degree ya pili hapa ni connection na uthubutu wako.


USIJICHANGANYE KUACHA KAZI UKAENDA KUSOMEA JAMBO JINGINE BILA KUFUATA TARATIBU.

UKISHAINGIA KWENYE SYSTEM YA GVT HATA UKIACHA KAZI YAKO UKAENDA KUSOMEA KITU KINGINE KUAJILIWA TENA NI NGUMU KWENYE MFUMO HUWA INASOMEKA KUWA VYETI HIVI VIMESHAAJILIWA SEHEMU FULANI.


Njia sahihi kwa 100% soma degree nyingine ukiwa kazini hlf omba kubadilishiwa kazi au cheo RECATEGORIZATION hii inafanya kazi bila shida.


Mambo siyo rahisi kama unavyowaza kuhamia Taasisi ni rahisi lakini kuna taratibu zake siyo kukurupuka na kwenda haraka kama unavyotaka wewe.

Unaweza kuanzia halmashauri ukahamia Taasisi.

Siwezi kueleza mengi hapa JF ila ukiweza fanya tuongee live nina mengi ninayoyajuwa kuhusu hii michakato coz mimi pia ni mhanga wa mishe hizi,

Taasisi kuna maisha kuliko serikali za mitaa so kutokana na kuhaso sana nilijifunza mengi kwa vitendo.

Yaani mimi nililianzisha kweli kweli mpaka NIKAFIKA KWA DE (Director of Estblishment) Huyu ndiyo anacontrol watumishi wote nchini ukitaka kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kumuona tu ni issue ofisini kwake.

Akitoka Waziri wa UTUMISHI, ANAFUATIA KATIBU KIUENDAJI NA BAADA YA KATIBU ANAFUATIA HUYO ED.

Huyo akisema hamia pale unakwenda akisema NO hata katibu mkuu anamsikilizia huyu kiutumishi.

Kwanza kujishusha ni lazima kuna inabidi uwe mpole ili jambo liende zaidi ya hapo labda uwe na ndugu vigogo serikalini.
 

Aisee.
 
Hizo taasisi zingine kuhamia ni pesa na connection.
Mchakato unaanzia juu.
Andaa mfuko mnene lakini kwa watu sahihi.
Maana maombi ya kuhamia huko yamejaa tele bila fitina utoboi.
Unachoongea ni ukweli 100%, hebu tujadili Hapo issue ya kusoma nje, vipi kuhusu scholarship? Nchi gani ambayo ni nzuri kwa kwenda kusoma? Shida ya huku ualimu masters ni added advantage haibadilishi kitu kwenye muundo wa mshahara.
 
Dah hii issue naona inakua ngumu sana kwangu mzee, kwa experience yako course ipi ambayo naweza kusoma nikiwa kazini? Maana ruhusa imekua ngumu kwangu, nimekutana na Mwalimu kwenye seminar ya walimu wa science alikua na master's ya mambo ya finance Lakini Bado ni Mwalimu na umri umeshaenda saana, Sasa endapo na Mimi nikienda kusoma Kichwa Kichwa bila kua na mtu nadhani nitaishia hukohuko.
 
1. Baki kazini, kasome Masters, rudi kazini na utulie kwa kama miaka 3 hivi kisha halafu ukasoke tena PHD.
Au 2. fanya mpango uhamie ktk miji mikubwa yenye vyuo vikuu vilivyo bora, na huko ukasomee fani unayoitaka ktk evening programs
 
Njia ni uombe nafasi kwenye taasisi unayotaka kwenda kama nafasi ipo watakubali uhamie huko au usubiri wakitoa nafasi huwa zinatangazwa ufatilie uombe kuhamia maana uwezi kubamishwa kutoka halmashauri kwenda taasisi kwa ninavyo jua mimi lakini kwa ushauri wangu usipanc nenda taratibu subiri ruhusa ya kusoma ukipata kasome degree nyingine japo huwa wanabania kusoma degree nje ya kada ulioajiriwa.
 
1. Baki kazini, kasome Masters, rudi kazini na utulie kwa kama miaka 3 hivi kisha halafu ukasoke tena PHD.
Au 2. fanya mpango uhamie ktk miji mikubwa yenye vyuo vikuu vilivyo bora, na huko ukasomee fani unayoitaka ktk evening programs
Hapo kwenye kuhamia kwenye miji mikubwa napo ni changamoto SI unajua tumetoka vijijini hatuna watu wowote waliotangulia huko juu, nimetenga mpaka laki 8-1Milion nipate connection ya kwenda kibaha tu au mkuranga nimekosa, matapeli kibao.
 
Ndio wanabana sana, ningeenda mwaka huu Lakini wanatoa ruhusa ya miezi 18 tu masters nje ya Hapo nakua mtoro kazini nimehairisha kwanza, sitaki kusoma master's ya education au utawala maana najua nitakua kama nilivyo tu bila mabadiliko yoyote, Morogoro Kuna Mwalimu ana PhD na ni Mwalimu wa secondary.
 

Kuandika barua na kutuma.
 
Unachoongea ni ukweli 100%, hebu tujadili Hapo issue ya kusoma nje, vipi kuhusu scholarship? Nchi gani ambayo ni nzuri kwa kwenda kusoma? Shida ya huku ualimu masters ni added advantage haibadilishi kitu kwenye muundo wa mshahara.
Canada, USA, Scandinavian,kazi zipo nyingi kule kuendesha malori,kazi za ujenzi,nk
 
Umri unaruhusu endelea kuomba majeshini pia kwa graduate mwisho miaka 28 ukipata unakula Kona.
Serikali inatambua masters siku hizi unavuta milion na laki saba
 
Mkuu kuwa Makini na utoaji wa taarifa zako humu,Kikubwa nakushauri eleza mambo Kwa ufupi ufupi...
Lakini kingine nakushauri tafuta Taasisi yoyote ile yenye nafasi halafu omba kuhamia....
Lakini kama ikiwa ngumu nenda kasome masters kwanza Huku ukifuatilia mipango yako
 
Issue Yako Iko kama Mimi. Kusema ukweli tamisemi hapana jamani. Yaani huku tunapauka mpaka basi. Mm nilisoma course ambayo nililetwa huku lakn ikaonekana kazi za kufanya hamna. Tuliomaliza kipindi Cha kikwete ilikuwa unaweza pelekwa sehemu utajua mwenyewe huko huko. Nina degree nilirud kusoma certificate ili nifit kwenye mfumo but sikufanikiwa kumaliza. Hapa ni kwamba nilianza biashara na kunogewa na kujikuta muda wa kurud kazini umeisha. Mwaka huu nimeomba kwenda kusoma masters nimepambana mpaka ruhusa nimepata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…