au tuseme mechanical engineering. Kwamba hata nikirudi halmashauri wanifanyie recategorization then niombe kwenda Taasisi nyingine huku nikiwa nimeshafanyiwa?
Mkuu samahani kwa kukuweka kidogo kuhusu hizi hoja zako. Sasa tuanze na hii.
Incase ukasomea mechanical engineering, ukimaliza pale halmadhauri watakubadilishia cheo cha muundo (recategorisation) kutoka divisheni ya elimu sekondari kwenda divisheni ya miundombinu na maendeleo ya mitaa/vijiji. (Zamani hizi divisheni zilikuwa zinaitwa idara, na ndilo neno lililozoeleka kwa wengi). Kumbuka mpaka uruhusiwe kwenda kusoma kada tofauti kubadilishwa muundo sio issue tena.
Sasa kwenye hii divisheni ya miundombinu na maendeleo mitaa/vijijini kuna vitengo/sekta tatu; yaani;
1. Sekta ya majengo
2. Sekta ya barabara
3. Sekta ya mitambo na umeme.
Sasa wewe kama mechanical engineer utakuwa hii sekta ya mitambo, ukihusika na kukagua na kusimamia matengenezo yote ya magari ya halmashauri. Wadau wako watakuwa ni TEMESA kwani ndio taasisi ya serikali yenye wajibu wa kutengeneza magari yote ya serikali. Na huko ndio utajenga link ya kuhamia TEMESA au taasisi nyingine moja kwa moja kutoka LGA
mfano Nikisoma mambo ya meteorology ndani ya halmashauri Kuna ofisi zinazoshugulikia hayo mambo ya Hali ya hewa?...
So far, masuala ya hali ya hewa hayana uzito huo kwenye LGAs, mara nyingi yanaratibiwa na TMA wenyewe. Japo kwa baadhi ya maeneo TMA huwa wanaweka partnership na LGAs especially masuala ya kuchukua takwimu kwenye mitambo yao wanayoweka wanakohitaji.
Sasa, kutokuwepo na divisheni mahsusi kwenye halmashauri hakukuzuii kusomea hilo suala. Kumbuka huu ni mchongo unafanya, HR akiwa upande wako anakuruhusu ukasome. Ukitoka masomoni unapeleka vyeti, yeye anakuongezea ujuzi kwenye database.
Sasa profile yako ikishakuwa updated, unatafuta chance huko TMA ukipata utaandika barua kigezo kuwa hapa kwenye halmashauri uko underutilized, maana taaluma yako mpya haitumiki. Simple but inahitaji kujitoa kimwili, kiroho na kiuchumi.
Mfumo wa malipo wa Lawson upoje? Nimeambiwa kwamba mfano nikienda kusoma hata nikiajiriwa sehemu nyingine utazingua kwenye malipo kwa sababu Mimi tayari ni muajiriwa sehemu nyingine, au Ndio tunarudi kule kwa Afsa utumishi kunifanyia re-categorization?.
Kwa kifupi ni kwamba, hakuna double employment kwenye mamlaka za umma. Nikisema mamlaka za umma namaanisha ile mihimi mitatu ya nchi, Yaani Serikali, Bunge na mahakama. Sababu ni moja tu, fedha zote zinatoka hazina kuuu. Kwa hiyo haiwezekani kwa mfano mtu aajiriwe serikalini af aache aombe mahakama au bunge. Mfumo utamkataa maana taarifa zote hizi zina link kwa mfumo huo wa lawson. Yaani ukishapewa cheque number huwezi kupewa nyingine, wakiingiza credentials zako zinagoma kabisa.
Na nikisema serikali ujue inajumuisha serikali kuu, serikali za mitaa, taasisi zote za umma, mashirika yote ya umma, na asasi zote za kiserikali.
Sasa kinachofanyika hapa sio kuomba ajira upya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, bali ni kuomba kuhamia sehemu unayotaka yenye sifa ulizonazo. Halafu kule unakokwenda wanakulipa mshahara kutokana na viwango vyao vya mishahara.
Ndio maana ukiona ajira za umma kwa waombaji wapya age limit huwa ni 45 years, lakini wale wanaohama sehemu moja kwenda nyingine huwa hakuna age limit, maana wewe huajiriwi ila unahamia.
Kwa hiyo wewe mkuu usijaribu kuomba ajira upya, (labda uombe private), omba kuhamia.
Kila la kheri mkuu