Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

Njia gani nzuri ya kutatua changamoto kama hii kazini kwangu?

Me pia Boss wangu ni kama freemason, ananikosesha Amani daily. Anapenda sana dharau. Wiki iliyopita alinifokea bila sababu ya msingi nikamuambia akiendelea nitamuua. Hatusalimiana tangu alhamis
Nilimfanyia hivyo yule Mjinga Muhindi wa pale USARIVER mpaka akataka anipeleke mahakamani.

Yaani nchini kwangu aje mzungu kunihangaisha na kuninyanyasa? Ananiogipaga hadi leo tukionana hapa Arusha.
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Ni private au Gavoo?
 
Kuna kenge flani mhindi alikuaga na tabia hiyo kunifokea bila sababu,nikaja nikamlia timing siku akajichanganya akanifokea then akanitusi ,nilichofanya nilimsogelea nikamwambia unasemaje wewe,nikampiga mtama pale pale akanyanyuka hajakaa sawa nikamrukia nikampiga teke la mbavu hajakaa sawa nikampiga ngumi za mfululizo kama 10 hivi halafu nikachikichia zangu,police hata hakwenda instead boss mkuu akaitisha kikao cha suruhu mimi nikamwambia siko tayari tena kufanya kazi mazingira yale, na ikawa ndio mwisho wangu kufanya kazi private sector.
 
  • Kwa kuwa upo sekta binafsi, ni sawa na jina lako kuandikwa kwa penseli, muda wowote linaweza kufutwa.​
  • Kama huna taasisi nyingine ya kufanya kazi, nakushauri vumilia kwanza na chukulia malalamiko yake kama fursa ya kukujenga.​
  • Mfanye awe rafiki yako,muombe akuelekeze kazi ata kama unajua zaidi.​
  • Pia usiwe siriazi sana kazini, jitahidi uwe ni mtu wa kuwafanya wengine wawe na furaha pale wakuonapo.​
Point yako yako mwisho siiungi mkono.
 
Point yako yako mwisho siiungi mkono.
Dunia ya sasa ukiwa mjuaji, utalala njaa; ndio maana kuna watu na elimu zao wamegeuka kuwa chawa.
Kwa sasa kazi ni chache, na wanaohitaji kazi ni wengi; muhimu kuishi kwa akili huku ukifanikisha ndoto zako.​
 
Mi ni jinsia ya kiume (ME) na boss wangu ni jinsia ya kiume ( Me)
Hamjachukuliana demu?

Kama kuna mamlaka mengine juu yake lifikishe huko pia.

Ama lah mwambie mheshimiane wote hapo ni waajiriwa kama kampuni si yake. Mchane, ajue unamaindi mambo yake yakiboya.

Vinginevyo asije kukulaumu siku yakikushinda.

Kama kunauwezekano anaona hataki kufanya kazi na wewe akusaidie pia uende idara nyingine. Ila usumkimbie kama naye ni mwajiriwa.
 
Usiwe kama kondoo wewe uyo boss wako ukimshindwa kavu shtua kidgo unamchna live,Mi kuna jamaa yupo ivo ivo nilikuwa nafanya nae kazi kwanza anamatusi kitu kidgo tusi zito alafu anapenda kukuumua mbele za watu yule ni mdengereko nawajuwa tabia zao, ss siku moja ivo ivo watu wapo wengi nilikuwa nshastua namgojea tu aingie geji,
Kweli akajaa akanza kufoka nikastop nikamwita jina lake fulani hivi wewe unaakili timamu kweli? Muda wote we ni kpayuka tu unanyge za mdomo au dipression imezid unachmba sana ka malaya aliekopwa au unafikiri nina shida kuliko wewe watu kimyaa tangia siku iyo akuweza niharas tena
 
1. Bosi wangu ananifokea Sana kwamba sijui kazi ilihali ni kitu nilichosomea na najitahidi kuonesha juhudi

2. Bosi wangu ananifokea Sana hata kwa makosa ambayo kayafanya yeye mwenyewe kwa uzembe

3. Natumia kila njia ili niwe mfanyakazi mzuri na kumfurahisha bosi wangu lakini Bado anakuwa mkali kwangu

NB: Leo boss wangu kanifokea ilikuwa kidogo tuu niombe kuacha kazi na ilikuwa mbele za watu hadharani.
Ni taasisi binafsi

Je nifanyaje kwenye Hali Kama hii?
Pole sanaa mkuu kwa changamoto, ni hali ya kawaida kukutana na hali hiyo ukiwa mwajiriwa, pia hata kwenye mahusiano n.k

Lakini kabla ya kulaumu, fanya utafiti wakina kujua sababu zinazokufanya ukumbane na changamoto hiyo, Pia angalie wafanyakazi wenzako wanavyoishi then relate mahusiano yao na Boss wako. Hii itakusaidia kujua boss wako ni mtu wa aina gani,anapenda kipi/hapendi kipi, anapenda/hapendi watu wa aina fulani.

Pia kumbuka hakuna boss anaependa aonekane kuwa chini ya wafanyakazi wake, kama umemzidi elimu,akili,muonekano(smart) au kama unakubalika sanaa na wafanyakazi wako kuliko yeye atatafuta sababu ya kukushusha hadhi yako. NB: sio wote wana roho hiyo ya kuchukia wafanyakazi,pia Wapo maboss wanaopenda wafanyakazi wanaokuwa smart kwenye kazi (Kuna kabila/jamii huwa wanatabia hiyo.. wakipanda cheo lazima mtaona chamoto, ni nature yao kwahiyo ishi nao kwa akili)

Lakini kunasababu zinazoweza kusababisha boss kukuchukia:

●Kutotimiza wajibu wako. Hakuna boss anayependa kuwa na mfanyakazi ambaye hatimizi wajibu wake, Yaani kilakitu lazima uambiwe,ukumbushwe kila kitu unakuwa wa mwisho. Kama una hiyo tabia acha mara moja.

●Kuwa na uwezo mdogo wa kujenga hoja. Fahamu deeply taaluma yako, pata ujuzi mpya kila siku, ikitokea kuna tatizo ofisini usikae kimya toa msaada wa mawazo ya kuimarisha ofisi.

●Kuto jali muda. Hakuna kitu muhimu kwenye taasisi yoyote kama muda, Jali muda wa kuingia kazini na kutoka, muda wa kuanza kazi na kumaliza, Jali muda mkihaidiana mfano kikao,kutoa repoti,n.k

●Kutoshirikiana na wafanyakazi wenzako. Kuna muda wa kazi, na muda wa kupumzika, hivyo kuwa social, zungumza na wenzako usijitenge sanaa, na usiwazoee sanaa.

●Acha mazoea na boss wako kwenye mambo ya kipuuzi, hapa kuna kuna seheme tofauti kama kwenye media,whatsapp the way unavyochat na watu wanakuchukulia boya tu, so yanakushusha hadhi, acha upuuzi.

●Usiwe mropokaji wa ovyo ovyo, Yaani Chochote unacho zungumza kiwe na manufaa,Kama wenzako wanajadili upuuzi usitoe maoni stay cool,Sometimes to be silent is better

●Epuka kutoa siri za maisha yako kwa kila mtu, watu wasijue kilakitu ulichonacho, au unachokipitia au tabia zako nje ya kazi. Kama unapiga gambe sanaa punguza.

●Kuwa Ruler 📏 kama YES iwe YES, NO iwe NO. Usiwe mtu wa kuyumbishwa tu na watu, Watu wajue unamsimamo. Hata boss akijua una msimamo ata kuheshimu, hawezi kuja kichwakichwa.

Maisha hayana njia moja, sio lazima njia uliyonayo ndiyo utakayo tokea.

● Mwisho : Usiache imani ya Mungu wako. Kwenye ofisi zetu za kibongo kuna mambo mengi sana kama ushirikina,waenda kwa waganga kukupiga tukio n.k (Hii wanaita kukupaka mavi ,kama kuna mtu kakufanyia hilo, hapo hutoboi hadi utafukuzwa kazi) namna ya kutoka fuata kanunu za kiimani, asubuhi kabla ya job Pray, ukiwa kazini Pray, ukitoka Pray, eneo la kazi Pray, Pray daily. Then urudi utupe mrejesho.

Asante
 
Dunia ya sasa ukiwa mjuaji, utalala njaa; ndio maana kuna watu na elimu zao wamegeuka kuwa chawa.
Kwa sasa kazi ni chache, na wanaohitaji kazi ni wengi; muhimu kuishi kwa akili huku ukifanikisha ndoto zako.​
Kuishigani kwa akili, hali kwamba unateseka, huna amani, unanyanyaswa bila sababu. Soma sababu nilizopost labda utaokota kitu.
 
Back
Top Bottom