Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wadada wenye uchumba sugu.
Kuna wadada wapo kwenye mahusiano zaidi ya miaka kadhaa, na wanatamani waolewe; lakini wanaume walionao bado wanawapiga dana dana.
Njia rahisi inayoweza kukusaidia, mwanaume wako afanye maamuzi ya haraka katika kukuoa, fanya hivi:-
Kuna wadada wapo kwenye mahusiano zaidi ya miaka kadhaa, na wanatamani waolewe; lakini wanaume walionao bado wanawapiga dana dana.
Njia rahisi inayoweza kukusaidia, mwanaume wako afanye maamuzi ya haraka katika kukuoa, fanya hivi:-
- Andaa bajeti ndogo ya laki mbili n.k
- Mtoe 'out' mpenzi wako
- Tafuta eneo tulivu, inaweza kuwa hotel yenye eneo kubwa, au sehemu yoyote wanazotoa huduma zote za chakula, vinywaji, malazi n.k
- Tafuta meza ya nje iliyojitenga, yaani muwe wenyewe tu au kuwe na umbali kufikia meza nyingine.
- Itakuwa vizuri zaidi kama itakuwa ni usiku
- Agiza vinywaji vingi ili muhudumu asiwe anakuja mara kwa mara kwenye meza yenu.
- Pia hakikisha umevaa nguo nzuri, inayomtamanisha mpenzi wako.
- Pigeni stori za kawaida, ila mkifika chupa ya nne anza kuongea kwa hisia kwa kumuonyesha umuhimu wa mpenzi wako katika maisha yako.
- Mpigie magoti huku ukitoa maneno ya mahaba ukiigiza kama unataka kulia, na kumuomba aweze kukusitiri katika ndoa.
- Mlilie mpaka yeye mwenyewe aanze kulengwa na machozi, na hatimaye yeye mwenyewe atakuinua na kukumbatia, na atakupa jibu lako.
- Baada ya kufanya hivyo, deka kama mtoto mdogo ikiwezekana uwe unamkalia kalia, huku mkiendelea kupata vinywaji.
- Mkimaliza hapo, nendeni chumbani mkapumzike.
- Kesho yake anza kutekeleza mlichoafikiana.
- Baada ya hapo nawatakia ndoa njema.