Njombe: Ajinyonga hadi kufa kwa kunyimwa unyumba na mkewe ambaye alidai mume hajaokoka

Njombe: Ajinyonga hadi kufa kwa kunyimwa unyumba na mkewe ambaye alidai mume hajaokoka

Hao Me shida yao wengi wakipitia hali fulani huwa hawajui kuhadithia na kuomba ushauri (wasiri) ili walau wapate ahueni.

Kazi yao wanayagugumia moyoni mwishowe wanajikuta kichwa kimejaa maudhi hapo ndo unakuta wanafanya maamuzi ambayo hata hayaelezeki saa ingine.

#Kuwashauri tu hao Me mambo yanapowazidia wajifunze kutafuta ushauri kwa wengine. Serikali ya kichwa kimoja peke yake kukijaza mambo kibao sana sana unakichosha tu.
Inasikitisha sana mpenzi
 
Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu, kufuatia madai ya mgogoro wa kifamilia.​
Tunakoelekea hatimaye watu watajinyongea kamasi kweli
 

Damas Mgaya (38), mkazi wa Mtaa wa Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe, amefariki dunia baada ya kukutwa amejinyonga ndani ya chumba chake kwa kutumia kamba ya kiatu, kufuatia madai ya mgogoro wa kifamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, ACP Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililoripotiwa jana, Oktoba 13, 2026, majira ya saa 12 asubuhi, akieleza kuwa marehemu alikutwa akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyofungwa kwenye nondo ya dirisha.

Kwa mujibu wa Kamanda Banga, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na kutokuelewana kati ya marehemu na mkewe kuhusu masuala ya ndoa na tendo la ndoa.

Inadaiwa kuwa mke wa marehemu alikataa kushiriki tendo la ndoa akieleza kuwa mumewe hajaokoka, hali ambayo inadaiwa kuchangia mgogoro huo wa kifamilia na kumsababishia marehemu msongo wa mawazo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Banga ametoa wito kwa viongozi wa dini kuhimiza mafundisho yanayojenga amani, maelewano na mshikamano katika familia na jamii, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua kwa vitendo vinavyokiuka sheria.
Nimesema ni upungufu wa akili na umaskini.
 
Back
Top Bottom