Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

Njoo uifahamu Taxi Mtandao BOLT/UBER

Inafaa ndio unachotakiwa kufanya ni kujisajili Kisha unawafundisha watu wa huko wajiunge...mkiwa wengi mambo yanafunguka huko huko mkoani....ila bei za hii mitandao ni za chini kama umezoea kutaja bei kubwa huu mtandao utauchukia 🙆
Mkuu kwani bei unataja wewe au wanakupangia watu wa Uber?
 
Nadhani nimekujibu inbox gari inakimbiza japo haitofautiani sana na bajaji...ila gari IPO juu kwasababu imekaa kishua Zaidi maana Kuna maboss hata iweje awawezi kupanda bajaji hua wanajiona kama wanazalilika wakionekana wameshuka kwenye bajaji...harafu Kuna waiting lounge airport Kwa wenye Uber hata bolt hapo unasubiri abiria bila kutumia nguvu airport...sasa watu walioshuka kwenye ndege ni nadra sana kupanda bajaji🙆🤣🙆🤣
Hv kuna waiting lounge siku hizi, kuna kipindi nilisikia wenye taxi za pale airport wakikujua km ww ni uber/Bolt aisee lzm itakua shida hebu fafanua hili
 
Hv kuna waiting lounge siku hizi, kuna kipindi nilisikia wenye taxi za pale airport wakikujua km ww ni uber/Bolt aisee lzm itakua shida hebu fafanua hili
Kwenye app zao wameiweka sasa Sina uhakika kama pale airport Kuna nafasi ya TAXI mtandao
Screenshot_20231007-140716.jpg
japo nahisi TU kutakuwa na nafasi hiyo...maana Kwa dereva yeyote lazima ikuelekeze pale
 
Asante Prince Mhando kwa maelekezo mazuri,,
1: Ningependa kufahamu kuhusu aina ya gari ambayo itavutia zaidi wateja (hii pengine inaweza kukupa wateja private nje ya mtandao)
2: Kwa Uba nasikia wanakuweka online kwa masaa 12 tu, je, ni wakati gani naweza kugawanya huo muda ili nipate request nyingi,,? yaani muda mzuri kuanza kazi na kufunga,,
 
Gari yoyote yenye cc ndogo 1300 kushuka chini best recommended IST, VITZ n.k .

Ndio masaa ni 12 ila sio kwamba ukiwasha TU yanaanza kuhesabu Bali masaa hayo yanahesabu ukiwa na abiria. Ukiwa huna abiria yanastop. Muda mzuri ni saa 11 alfajili Hadi saa 3 asubuhi Kisha saa 8 mchana 2 usiku. Kisha saa 2 usiku Hadi saa 8 {usiku wa manane wanauita.}

Usiku Kuna lipa Zaidi kwasababu request ni nyingi mno.
 
Back
Top Bottom