NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

MeinKempf

Mkuu kwa hili NMB wanastahili pongezi za hali ya juu.. Mimi sikutegemea NMB wanaweza kuwa watu wa kujali kiasi hiki cha kujitojeza jukwaani na kuomba radhi... Nadhani ninakila sababu sasa ya kujiunga na hii bank inayoonyesha kujali..
Asanteni NMB,as ante Jamii Forums

Mkuu bado wanastahili pongezi? Maana walifungua tu thread.lkn hamna majibu yeyote wanayotoa kwa wateja
 
Last edited by a moderator:
Nilijaza fomu ya kuweka pesa tsh 500000 nikakosea nikampa 1000000.Nilipotoka dirishani kabla hajaingia mteja mwingine nikashtuka kama nilichoweka sicho nilichojaza kwenye fomu nikarudi haraka.

Nilipomuuliza kiasi nilichompa na nilichoandika alizubaa tu hakunijibu mara akanipa pesa zangu zote 1m nikagawa zilizobak nikampa akazipokea kwa aibu bila kuhesabu mi nikaondoka.

Shida ni uaminifu mdogo kwa baadhi ya wahudumu.
 
nmb mmefuta mkataba na baadhi ya halmashauri kuwakopesha wafanyakazi wao lakini mnachoshangaza hamliweki wazi hili swala na mnaendelea kugawa miform yenu watu wapate usumbufu
 
Kuna hiki kitu kinaitwa "NMB MOBILE"...Unapotuma pesa au kutoa pesa kwenye account yako unatumiwa ujumbe kuwa umetuma au umetoa pesa lakini kinyume chake ;pale unapotumiwa pesa kwenye account yako hakuna ujumbe wowote kuonyesha kuwa kuna pesa imeingia kwenye account yako.

Hii itasidia ikitokea umetumiwa pesa unajua na mtu akizitoa pia unajua hata kama pesa zilitumwa kimakosa kwenye account na zikatolewa mwenye account anatakiwa ajue.Hii ikoje.?

Naomba mliangalie hili kwa jicho pevu na mtupatie majibu tafadhali.
 
Habari.
Mimi ni mteja mpya wa benk yenu na tayari nimeshapata account number yangu kutoka katika bank yenu.

Ni kiasi cha wiki zaidi ya mbili hadi sasa nafuatilia Atm card yangu lakini mpaka sasa sijapatiwa card hiyo na tayari pesa yangu ishaingia kwenye account na nilipokwenda katika bank yenu niliambiwa kuwa batch zenu ziliharibika na hivyo nimeambiwa nirudi wiki ijayo au baada ya wiki 2.

Pia wiki moja ilopita niliambiwa hivyo hivyo ni rudi baada ya wiki na niliporudi nilipewa taarifa kuwa batch zimeharika na kwenda kutengenezwa upya.
Swali langu ni : VIPI NITAWEZA KUTOA HELA ILOINGIA KATIKA ACCOUNT YANGU WAKATI HAMJANIPA CARD NA HADI SASA HIVI NAMAHITAJI MAKUBWA NA KIASI HICHO CHA PESA ?

Pia napenda kujua kama utaratibu wa kutoa hela dirishani upo au hapo ?
Na vipi suala la kucheleweshewa card,uongozi wa bank umnauchukuliaje au ndile biashara ya kupata wateja wengi ndio mwanzo wa kuharibu biashara ?

Na vipi zikipita two weeks bila ya kupata card yangu,ni chukue hatua gani ?
mimi mteja wenu.
 
Kuna tawi moja la Nmb lipo mkoa wa kilimanjaro ukitaka mkopo hata kama ushakamilisha kujaza fomu zao mpaka upige magoti!Tofauti na CRDB na benki nyingine zilizopo hapa.Natamani kuhamisha mshahara wangu!
 
NMB bonus account, je nayo ni yenu pia, maana nakaribia kumaliza mwaka sijapata Bonus card, hadi fomu yakufungulia akaunti imechakaa! Jamani NMB!
 
Me nina tatizo moja tuuu,huduma ya NMB mobile 📱 sipati ijapokuwa nilisajili kwa simu,tatizo nni?
 
naomba nmb tupelekeni kwenye visa nashindwa kutumia feha zangu nje ya nch .
 
Daah jamani NmbN.mandela meneja huduma kwa wateja yule mkaka asee ni kichefuchefu hayuko polite hata kidogo pia kuna yule dada mweupe anavaa miwani pale mwanzoni sijui kwanini mmemuweka huduma kwa wateja anajibu utadhani hajisikii kuongea na wateja!

kuna macashier wawili jamani hata uwe umekasirika vp hasira inaisha walivyo na kauli paulina navyule dada mnene alikuaga fast track..badae akaenda bulk siku izi simuonagi tena maskini!

Jirekebishe nyie wengine jaman biashara ni kauli
 
Nawapongeza NMB kwa kuliona hilo.
Kwa lengo la kuendelea kufanya maboresho yafuatayo ni maoni yangu.
1. NMB Ngara kuna wateja wengi balaa. Fungua branch mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge. CRDB wakikamilisha branch yao Ngara mjini kiburi kitawapungua.

2. Customer service pale NMB house ni bonge la poor, kupanga mstari hata kuliza nina shida hii niende mlango gani!!?? Hili linaudhi wengi pale.
3. Wateja wenu tuna simama sana kuchukua fedha. Ongezeni timu au motisha kwa wafanyakazi wenu.

Hongera kuja hapa.
 
hiv mteja wa nmb asipotumia account yake kwa mda gani mnamfuta?
 
Nmb mnaniudhi pale mnapolazimisha mtu uwe account pale anapowaletea open cheque. Mnazungusha wee bila kueleza sababu zenu za kufanya hivo.
 
Kuna mtu ameajiriwa miezi mitatu iliyopita na tayari ana salary slip 2.
VIPI ANAWEZA AKAPATA MKOPO,,,????
 
NMB wafanyakazi wenu wengi wana nyodo na majibu yenye ukakasi na harufu mbaya. mnalijua hili ????
 
Back
Top Bottom