NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mi Nauliza Ukichukua Mkopo Wa Sh.Milion 3.5 Kwa Marejesho Ya Miezi 48 Kwa Mtumishi Mwenye Basic Salary Laki Nne Na Sitini, Makato Yake Pamoja Na Riba Kwa Mwezi Ni Sh. Ngapi Kwa Muda Huo Wa Miezi 48??
 
Swali La Pili, Mkataba Sikupewa,nilipoenda Kutaka Kuuchukua Nikaambiwa Nilipie Elfu 30,000/= Ya Usumbufu Ili Anitafutie, Je Hy Ni Halali?
 
Nmb Mmefanya Unyama Sana Kupunguza Miaka Ya Mikopo Ya "Salaries Workers Loan" Kutoka Miaka5 Hadi3, Mkidai Kuwa Mnapata Hasara, Haya Ni Majibu Ya Nmb Tawi La Kilombero, Lakini Tumegundua Ukweli Ni Kwamba Pesa Mmewapa Serikali Ili Wafanyie Uchaguzi.

Umeacha Kuwapa Wafanyakazi Ambao Marejesho Yao Hayana Pingamizi. Huu Ni Utapeli. Watu Walipanga "Kutop Up" Mwezi Wa Kwanya Ili Kuwapeleka Watoto Mashuleni. Tunaomba Mrudishe Sisi Kama Wateja Halijatufurahisha
 
Nmb Hamfai Kabsa! Mmepunguza Muda Wa Mkopo Hata Kwa Mikopo Ya "Salaries Workers Loan"?? Watu Ambao Marejesho Yao Ni Ya Uhakika! Alafu Mnawapa Wafanyabiashara Na Wakulima Kama Wa Mpunga, Miwa Kwa Nmb Tawi La Kilombero Ambao Uwezekano Wa Kupata Hasara Nb Faida Ni 50%kwa50%?

Mmewafanya Wafanyakazi Wa Kampuni Ya Sukari Kilombero Kuingia Kwny Riba Za Mitaani Kwa Kushindwa Ku "Top Up" Ni Heri Saccos. Kwanini Tunarudi Nyuma Wakati Tulikwisha Piga Hatua? Mmepunguza Wateja, Tunaomba Mrudishe Huo Muda Miaka5
 
NMB, mmeamua kupunguza muda wa mkopo kutoka miaka5 hadi3, kwa sbb-:
1. pesa mmepeleka serikalini kwa ajili ya uchaguzi

2. pesa mmewakopesha walima mipunga, miwa hasa kilombero alafu wengi wao hawajavuna kitu

3. pesa mmewakopesha wafanyabiashara wameshindwa kurudisha

4. wengi wenu mmejichotea mapesa na kununua magari tumeona Nmb Tawi La Kilombero Meneja

Amesimamishwa Kazi. Hayo Yote Ya Kwenu Sisi Kama Wateja Hayatuhusu, Mmeshindwa Kuwakopesha Wafanyakazi Ambao Marejesho Yao Ni Ya Uhakika 100%.

Je, Mnampango Gani Ktk Hilo? Unapunguza Muda Wa Mkopo Wakati Kiwango Cha Kuchukua Kipo Palepale 40%?? Tunaomba Jibu Wana "JF"
 
kupunguza muda wa mkopo bila sababu wameharibu sana... sasa ivi kuna bank ingine wanatioa hadi 5yrs ... na riba nafuu zaidi
 
Nmb bank ya kipuuzi sana,mtu una shida ya muhimu ck ya jmapil unatoka mbali kote unakokaa halafu ATM zimezima!!!mfano mzuri ni branch ya wilaya ya Kibaha -PWANI
 
Utaalamu na utumiaji wa mashine katika kuhifadhi fedha umeongeza idadi ya waibiwaji hasa wanaoweka pesa zao benki.

maana mlima mihogo na digitali lini na wap, akiuliza mbona hela yangu imekatwa anajibiwa "aaah hiyo ni monthly tax charge installement with vat inclusive.

wizi mtupuuuuuuuuuuuu
 
Nmb

Kuna bankteller hapo NMB HSE ana mdomo mchafu,sana,mkanyeni mapema, sisi tunawaletea hela halafu nyie mnaleta dharau na kejeli,hii sio sawa, nimeulizia anaanza na herufI K nyingine malizieni wenyewe.
 
Watumishi wenu wanaomba sana rushwa na wanazima mashine za ATM ili folen ibore watu ili wahongwe wapewe huduma haraka! Bunda na Geita hizi branch kero sana!
 
Some time ukituma pesa kutoka NMB Account to M-pesa huwa inachelewa kiasi kwamba inaleta kero na usumbufu, jitahidini iwe fasta kiasi fulani. Mfano unasafiri unataka nauli halafu muamala unachelewa unakuta unakwama na hufanikishi mipango yako kwa wakati. Ila mnajitahidi kutoa huduma nzuri nimapungufu madogomadogo kama hayo.
 
Naomba kuuliza hivi naweza kuchukua mkopo hadi shilingi ngapi ikiwa nachukua mshahara basic 700,000/= na riba itakuwa ni sh ngapi na kwa marejesho ya miaka 3,
 
nimeomba mkopo tangu mwaka jana mwezi wa kumi na moja....nimeanza kukatwa lkn mkopo cjapata..nimeomba nmb tanga tawi la madaraka
 
kwanini mnakalia mishahara ya wafanyakazi ambao crdb inawaletea mishahara yao yaani imekuwa kero
 
Mimi account yangu ilikua dormant takribani mwaka sasa nazungushwa kama tiara
 
Nimewalipa mkopo wenu tangu januari bado
mnakata tu salio kwenye mshahara..kwanini?
 
Fixed account one million for six month mnanipa interest elfu tatu halali kweli hiyo?
 
Malalamiko: Nmejaza fom za mkopo tangu mwz wa 12 mwk 2014 lkn mpk sasa cjapata, hv mmefilisika au mna tatizo gn linawasibu ktk bank yenu?
 
Back
Top Bottom