NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzaniamnamo mwezi wa may,2014 nilikatwa kimakosa fedha zangu jumla ya kiasi cha shilingi.......kupitia account yangu namba...........cha kushangaza nimefuatilia mara kwa mara bila mafaniko na sasa umeingia mwaka mwingine sina matumaini ya kurudishiwa fedha zangu.


Tafadhali nawaomba mshughulikie suala hili, nitawasiliana na nyinyi for more details
 
Last edited by a moderator:
mm nilishaapa kutofungua a/c n.m.b huduma hovyo kabisa unakuta dilisha 7 labda linalofany kazi ni moja tu tena taraaatiiibuuu dada wa watu mara ajibu msg za cm mara atokeee duu kwer bank y makabwera mwanza r/d
 
Vile vidirisha vyenu vya ATM vingi ni mapambo tu hasa tar za mwisho wa mwezi foleni watu 300 vidirisha viwili na kinachofanya kazi kimoja huku kingine kikisomeka hivi MASHINE HII HAITUMIKI KWA SASA yaani nyie nmb ni shid mtu katoka kjjn anapiga kambi siku tatu akisubiri pesa ukienda ndani wahudumu wanakurudisha nje kama mavi

Halafu Yale maneno yenu yanayosomeka pale bank kuwa
ATM 24 HOURS ni bora muyafute na kuandika
ATM 12 HOURS Kwani ndo muda ambao zinafanya kazi

Nmb mobile nayo ukichukua Leo SMS ya pesa utaletewa keshokutwa hii nayo majanga tu mpaka tunaiogopa

Mikopo kwa watumishi nayo hata kama una kila kitu
Mfano unachukua milion 7 bila kuwa na refa au kumwachia afisa mikopo wa benki laki 5 hujapata mkopo la sivyo utarudi unaambiwa fomu ilipotea jaza nyingine na hiyo nayo baadaye utaambiwa hivyo kumbe ttzo tu hukutoa kamlungula....acheni hizo nmb mnatubore mtakosa Wateja......
Mteja wenu. Some where in Tanzania.
 
Castomer care ni tatizo kubwa ndani ya benki hii. Wapeni wafanyakazi wenu mafunzo ya mara kwa mara!
 
nimetoka NMB magu mwanza, naitaji mkopo nimeambiwa wamesitisha huduma iyo kwann? na tena hawatoi mkopo wa miaka 5 kama ilivyo nyuma, badala yake mkopo wa mda mrefu mwisho miaka 3, cjajua ni kwann! afu hakuna buku 5 kwenye ATM, wala ela chini ya buku ten, sielewi kwann! na kutoa ela shart AC yako ibak na buku 5, naomba mwongozo
 
Mi nahisi hawalipi vizuri wafanyakazi wao ndo maana hawajali wateja
 
NMB inalalamikiwa kwa kuwaibia wateja pesa hasa wale wanokopa.

Nadhani serikali imeibeba sana hii benki kwa kuwalazimisha watumishi wengi kupitishia mishahara yao kwenye benki hii. Vinginevyo hii benki ingekuwa imeshapotelea mbali na kubaki kama SACCOS tu mana haina huduma nzuri.

Huduma mbovu NMB inatokana na kuajiri watu wengi wenye vyeti feki na kujuana. Nendeni mkaone wasomi waliotulia CRDB na vyeti vyao halisi.
NMB badilikeni.
 
Naomba kufahamishwa miezi ya mkopo.nilienda nmb sgd nikaambiwa mda wa marejesho ni miezi 36. Ya miezi 60 imesitishwa.habari hiyo ina ukweli?
 
Huduma zenu mbovu sana hasa huku Mikoani ,mi Nipo mtwara mjini lakini nashangaa kwa mji kama mtwara unaoendelea kwa kasi wana tawi moja mashine za kutolea pesa kiujumla zipo nne hizo nne zenyewe tiamajitiamaji ukiingia benki sasa hao customer care hawazidi watano tunawaomba mlifikirie hili kwa kina
 
Namba yao ya simu ukipiga wanakuwekea matangazo dakika karibia kumi huku pesa kwenye simu inakatika tu yaani huduma zao ni hovyo kweli
 
kwanini bank yenu imekuwa sio mahari salama pa kutunzia hela maana ukiacha tu salio kuanzia sh 10000 mwisho wa mwezi hukuti hata sh 1 wafanya kazi wenu kwanza niwababe na hawana lugha nzuri kwa wateja.hasa tawi la mbozi mkoa wa mbeya kunamadudu baraa
 
NMB inalalamikiwa kwa kuwaibia wateja pesa hasa wale wanokopa.
Nadhani serikali imeibeba sana hii benki kwa kuwalazimisha watumishi wengi kupitishia mishahara yao kwenye benki hii. Vinginevyo hii benki ingekuwa imeshapotelea mbali na kubaki kama SACCOS tu mana haina huduma nzuri.

Huduma mbovu NMB inatokana na kuajiri watu wengi wenye vyeti feki na kujuana. Nendeni mkaone wasomi waliotulia CRDB na vyeti vyao halisi.
NMB badilikeni.

kweli kabisa maana mfanyakazu ukiacha hata 7000/= kwenye account mwezi unao fuata haukuti hata sh 1 huu ni wizi wa kweupe
 
be more aggresive and try to stop and check CRDB growth mimi ni mchumi, kwa hiyo chukua tanzania nzima, igawe kwa wilaya kwa miaka 5 nyuma hadi leo, halafu kwa kila mkoa weka Nmb walikuwa na Matawi Mangapi kwa kila willaya kwa miaka yote mitano, na CRDB walikuwa wana matawi mangapi kwa kila mwaka kwa kila wiaya.

Nadhani utaona jinsi wanavyokua kwa kasi. Unaweza ku delve deeper ukaangalia kwa customers , collections services etc. itakuja picha . Well done
 
Nmb inachosha unapo peleka hundi unapanga foleni ya kuweka hunditu unapohitaji fedha cash lazimaupange foleninyingine huuni usumbufu usio natija badilikeni
 
Nina account NMB na sifurahishwi na huduma zenu.
Moja ya kero kubwa ni FOLENI, NMB ni moja ya benki inayotumiwa sana na watumishi wengi wa serikali. Hivi huwa mnaajiri tellers wachache maksudi au ni kiburi tu cha hao tellers wenu? Unakuta kuna madirisha ya tellers sita ndani ya benki LAKINI yanayofanya kazi ni mawili au matatu tu! Tellers wengine mnawapelekaga wapi?? Au ni utoro tu? Na km ni watoro iweje msiwafatilie?

Kero nyingine ni Matumizi ya muda (Time management). Wafanyakazi wenu hawazingatii kabisa matumizi sahihi ya muda. Wengi wao wapo slow sana kuhudumia watu. Nawashukuru kwa sasa mmegawa wateja wanaolipa kwa hundi kubwa kuwa na dirisha lao lakini mbona bado foleni ni kubwa kwa madirisha ya kawaida? Vile vile ikifika saa nne asubuhi utakuta tellers wengi wanaondoka eti kwenda kunywa chai na kuanza madirisha yakiwa na vibao vilivyoandikwa: "Temporary closed". Utakuta saa nzima inapita teller hajarudi, chai gani ya kunywa saa nzima?

Kero nyingine ni mchakato wa ATM cards zinazokwisha muda wake. Kadi ya ATM ikiisha muda wake na bahati mbaya ukawa mbali na tawi ulilofungulia account inakuwa shida sana kuipata. Kwa mfano mimi binafsi nilifungulia account mkoa wa Iringa lakini baadaye nikahamia mkoa wa Tanga na baada ya muda kadi yangu ilikwisha matumizi yake na kunilazimu ku-renew. Nilipowaambia wahudum wa hilo tawi la Tanga walinambia nitatozwa gharama ya utumaji wa hiyo kadi ambayo ni shilingi elfu kumi na tano (15,000/=) ndipo watanitumia. Nilisubiri hadi miezi sita lakini sikufanikiwa kupata kadi yangu mpya hadi nilipoamua kwenda mkoa wenye tawi nilikofungulia ndipo nikapewa kadi mpya.

Tatizo lingine ni uchache wa ATM machines. Kwanini hamuweki ATM mchines nyingi hasa kwenye Mahoteli, Supermarkets, kwenye Sheli, na kwny vyuo km wenzenu CRDB? Nina uhakika mkifanya hivyo mtapunguza msongamano mkubwa hasa kipindi cha mwisho wa mwezi ambapo ndipo foleni hutia fora.

Kero nyingine ni huduma ya NMB MOBILE; Mara nyingine unakuta unachukua hela kwenye ATM machine lakin unapata ujumbe wa kuwa umetoa pesa baada ya dakika kumi au kumi na tano.
 
Benki yenu haibadiliki ipo ipo tu kwanini msiwe wabunifu ? Watu wanatafuta hela kwa shida kwenda kutunza hela zao na kuchukua pia wapate shida ? You have to be creatives and avoid conservatism.

Mtu kafanya kazi NMB miaka 7, lakini hana hata chembe ya ufanisi!! and you call him/her a manager? bull shit that Manager! unafreeze account ya mtu bila kumpa taarifa yet mnaazo katika kablasha zenu! mbu you had announced that in the medias, do you think each person listens to clouds and the so called blah blah medias?

Come one men, wapatieni vijana opportunities ili muwe sawa na dunia!
 
hawa nmb hapa naona wahuni 2, maana hawajibu maswali ya watu, nini maana ya kuomba maoni? acheni ubabaishi wa maofsin hadi humu ndani?
 
Back
Top Bottom