Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana. NMB siku hizi kila penye tawi lenu CRDB wanakuja kwa kazi na ni kipenzi cha watu wengi wakiwemo wafanyabiashara. mm niko Bunda mkoani Mara ambapo CRDB wanajenga tawi kwa kasi. naomba pale customer care kuna wasichana wawili ukiacha yule dada anayeitwa Agnes. wale wawili ni wapuuzi sana kiasi cha mimi kushindwa kufanya shughuli zangu pale. wanajiona kama miungu watu. hawajui thamani yetu na pesa zetu. walahi msipokuwa makini CRDB ikianza kazi mtatukisa wengi. castomer care ni weledi na si kila mtu anatakiwa kuwa pale. waondoeni wale wasichana au wapewe elimu na Agnes namna ya kusikiliza na kuhudumia wateja. Inauma sana kuweka watu wanaoangalia sura za watu ndo wawahudumie. ni hayo tu na nategemea mabadiliko NMB Bunda mkoani Mara.
...nmb sometims unabore saaana...nlifunguaga akaunt moshi..nelson mandela branch yr 2008...den after shule nlihamia dsm as kikaz zaid...atm yangu ili x pire....nlifuatilia nipewe ingine via ilala branch ila mnazingua miez mitatu ikaisha et atm mpya ipo moshi....kuileta imekuwa issue.....badiliken maana mpaka leo kimnya...mnaringa mtadhan bank n yenu pekeenu...nlishahama na nahamasisha wengine wahame hamna msaada kwa sisi jamii ya kawaida.......
Admins Fungeni hii thread haina maana, kama wamefngua humu dawati la huduma kwa mteja halafu wanashndwa kufuatlia na kutoa majibu kwa maswali wanayouliza inaonesha huduma zao ni mbovu tu!
Ninaweza kupata salary loan topup,mar ya mwisho nilikopa february mwaka jana?Kwenye web yenu inaonyesha unaweza fanya topup baada ya miezi sita,but hapa singida nmb wakasema hadi mwaka.Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom