NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB MPWAPWA NI ZAIDI YA MAJANGA, WAPO MIUNGU WATU PALE, UNATAKA MKOPO UNAZUNGUSHWA ASUBUHI MPAKA JIONI BILA JIBU LA MAANA HUKU NINA SIFA ZOTE ZA MKOPO NA MSHAHARA NAPITISHIA KWAO, NIMEENDA CRDB FASTER ACCOUNT NDAni ya dakika tu NA KUMALIZA KUJAZA FOMU ZOTE ZA MKOPO SASA TULI NASUBIRIA ANKARA.!
 
Jamani NMB zingatieni huduma ya kuhamisha pesa toka kwenye bank account kwenda mitandao ya simu (M-pesa, Tigo-pesa) kwakutumia NMB mobile inachukua muda mrefu mno. Kwa mfano mwezi wa tano nikiwa Mbeya nilikwenda ATM zenu nikakuta foleni kubwa.

Nika amua kuhamishia pesa kwenda account ya Mpesa ilichukua siku tatu pesa kuingia ktk simu. Hebu rekebisheni hilo ni usumbufu mkubwa kwa wateja wenu.

Pia tunahitaji huduma za VISA. Otherwise tukutane ktk kazi. Tchaoooo
 
ATM inazingua, inakata hela bila kuzitoa usiporipoti ujue Imekula kwako na ukiripoti subiri siku kadhaa yaani km una emergency utalia.wenzao crdb inarudi automatic tena fasta tu.

Mi imenitokea Jana pale ATM za mwenge TRA na nimejaza fomu. nasubiri kuona watatumia miezi mingapi kunirudishia
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Nashukuru kwa kuitikia wito hapa Jamvini.
Nadhani hili limekuja baada ya kutoa kero kwenye huu uzi
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=751714
Tunaomba mfanyie kazi malalamiko yetu,siyo mnakuja kutupooza na Herufi tu hapa jf.

Wafanyaki wenu Nmb mbalizi road branch hawajali wateja, wana lugha ya kuudhi sana kwa wateja hasa kitengo cha mikopo.

Kama inawezekana wafanyakazi wenu wawe wanavaa vitambulisho vyenye majina yao kama CRDB ili tuwatambue kwa majina tunapotoa malalamiko kwa huduma MBOVU.
 
NMB sina hamu na ninyu tena kwani kwa hapa Dodoma nawakomoa
wateja waliohamia kiba Benki (mkidhani wanamfuata meneja wenu wa zamani) wakirudi tu mnawalima faini.

Nina Current a/c (cheque book) nikapata matatizo binafsi ya mahakamani kwa hiyo mihangaiko sikuweza ihudunia hiyo a/c yangu zaidi ya mwaka na nusu siku naingiza cheque ya ndugu yangu aliyedhamiria kuninyanyua mkanilima 320,000/=

kama ada ya kuoperate hiyo a/c na bado mkanilazimisha kununua kitabu kingine.

Nilipotaka kumuona Meneja wa Tawi hilo la Dodoma Bw K nikajibiwa vivyo hivyo kuwa wataendeshaje a/c bila kukata pesa @10,000/= service charge nk?
Kilichonishangaza Mwenzangu mfanyabiashara ni mpaka leo hakatwi hizo gharama na anaweza maliza hata miezi 6 na aendapo NMB hakatwi chochote

rani zenu wa CRDB hawana adhabu hizo EQUIT Benki hawachaji gharama zozote kwa anayeweka feda huko AKIBA ndio kabisa hawakati ila kiwango chao cha chini ni 20,000/=

Adhabu hizo punguzeni kwani najua ndio Benki inayotumiwa zaidi na Serikali Kuu na Serikali za mitaa lakini ipo siku tutwakimbia kwani biashara ni huria na si lazma kufanya na serikali.
 
Jambo la kwanza, nawashauri mkaangalia crdb tawi la mlimani city namna wanavyowahudumia wateja wao.

Pili wafanyakazi wenu wanadharau sana kwa wateja wao. Hasa nmb tmk ambapo nimepata kushuhudia maneno machafu ya wafanyakazi wenu. Hawana good will kwa wateja. Tatu boresheni huduma katka ATM zenu.

Maana kuna baadhi ya ATM kukuta zina pesa ni nadra. Kama ubungo stand
 
Mmefanya vizuri kampuni za simu pia mnatakiwa mje humu kuna shutuma nyingi sana zinatukera mje na nyie kama hawa NMB walivofanya

Ya simu majambazi hayawezi kuja tutayashinda tu. Wezi wakubwa wale
 
Idara ya mikopo pamoja na managerment kujitutumua kudhibiti RUSHWa bado hamjafanikiwa kudhibiti urasmu huo dhidi ya wakopaji. NMB KITENGO CHA MIKOPO SHIDA IKO.

Idara za mikopo wanapenda rushwa. Akukopeshe hela ulipe wewe na ugawane nae huo mkopo. Wakati ukishindwa kurejesha cha moto unaona
 
Idara za mikopo wanapenda rushwa. Akukopeshe hela ulipe wewe na ugawane nae huo mkopo. Wakati ukishindwa kurejesha cha moto unaona

Aliyetoa na kupokea rushwa wote chupa moja. Mi nilichogundua sisi wateja ndo tunapenda kutoa rushwa sababu yakimuhemuhe chakutaka pesa kwa njia ya mkato.

Ila kubwa hebu tarehe za mishahara rekebisheni machine zenu zinalemewa na mara nyingi pesa kutokuwepo hii kwa Iringa Manispaa kwingine sijui ikoje
 
afu imekaa kama kibiashara...maana ukiwa na tatzo wanakwambia uwajulishe katika emails zao...cyo kuimwaga hapa na kuitolea ufafanuzi ka wafanyavyo vodacom.

Matumaini yangu Mods wataona haya mapungufu na kuifutilia mbali..
 
Back
Top Bottom