NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

afu imekaa kama kibiashara...maana ukiwa na tatzo wanakwambia uwajulishe katika emails zao...cyo kuimwaga hapa na kuitolea ufafanuzi ka wafanyavyo vodacom...
Matumaini yangu Mods wataona haya mapungufu na kuifutilia mbali..

Watakuwa walikuwa wanapima upepo. Sasa aliyeileta atakuwa ameona ina mtafuna mwenyewe.
 
mbona garama za makato ya kwa mwezi yanazidi kupanda? pia nakutoa pesa kwa ATM pia ziko juu sana?
 
NMB mpo local sana tunaomba muingie kwenye mfumo wa VISA na MASTER card ili angalau ukiwa nje ya nchi uweze kuendelea kupata huduma.

I am waiting this ili nifunge viaccount vyangu vyote benki nyingine.
Nimeshafunga NBC TAYARI.

Mi ni mteja wenu tangu 2003.

Shida yenu NMB NI RUSHWA KWENYE MIKOPO.
Badirikeni hapo mpambane na CRDB MAANA NDIYE KIBOKO YA MABENKI YOTE TANZANIA KWA HUDUMA NZURI.

PIA PUNGUZENI GHARAMA ZA KUPATA KADI MPYA KWA WATEJA WALIO NJE YA TAWI WALILOFUNGULIA AKAUNTI, 15,000/- NI NYINGI SANA JAMANI.

AHSANTENI
 
Kwa wakazi wa mbezi kimara, kuna tatizo la huduma ya ATM, Nawashauri mfungue maeneo hayo kwani usumbufu ni mkubwa.

Inalazimisha mtu uende kibaha au ubungo. Jitahidini msogeze huduma ikiwezekana hata kufungua branch, CRDB wamefungua na wateja ni wengi sana.

Nawapongeza watendaji wa Muhimbili branch, huduma ni nzuri sana. Kuna siku nimekaa nasubiri kuhudumiwa, meneja akaja kuniuliza kama nimehudumiwa, muda tena akaja afisa mwingine kuniuliza hilo hilo.

Ila tatizo ni huyo mdada wa mikopo, ana dharau sana nakujisikia. Miaka ya nyuma alinihudumia akiwa teller pale muhimbili, nilifunga account wiki hiyo hiyo. Nimefungua accouny bank house, mwaka jana tu, na ni kwa sababu ya shughuli zangu, ila huduma za mikopo sithubutu kwenda Muhimbili, maana huyo dada maringo mengi na customer care sifuri.
 
Wakazi wa mbezi-louis na kimara mmewasahau kihuduma..,hakuna tawi wala ATM..nashauri mfungue tawi japo mbezi mwisho, itasaidia watu wa kibamba na kimara kupata huduma kwa urahisi
 
mbona garama za makato ya kwa mwezi yanazidi kupanda? pia nakutoa pesa kwa ATM pia ziko juu sana?

mambo ya C.C.M na uchaguzi haya..
Money transafer zote zimeongezwa gharama, M pesa, Tigo Pesa, Atms ,Monthly chargers..
 
Moderators TOA Huu upuuzi! Maana watu wanatoa hoja mleta mada hajibu kitu?.
 
NMB ! NMB !!!!
najuta kua mteja wenu wafanyakazi wenu ni wanadharau kama banki ni ya baba yao hawana adabu wala ethics hata kidogo

mfano mimi sasa nipo sengerema ila kuna hao wafanyakazi nkifika pale bank nkiwakuta NMB sengerema bora nirudi manake unaeza piga mtu kuna mdada ni teller pale weupe ivi jaman uyo nguvu ya kua na dharau na majvuno katika kutoa huduma sijui kapata wapi ukiona kwenye foleni mpo wengi ndo kwanza anatoka anaensa ndani na bora ivo muda mwingne anatoa wanja anapaka anasubiri matajiri wa sengerema waje ndo utaona anaanza kutuhudumia ivi hiii banki ni ya matajiri kama ndio mtuambie tuhamishe vijisenti vyetu yote tisa kumi uyo mkaka m1 mwembamba mrefu ni anatukana hadi wateja kama huwezi tumia ATM mashine ucje bank yani kunasiku nimemkuta customer service pale anamju mama m1 mzee amepoteza kadi yake nilitaman mchabanga makofi nikapuuzi hakuna mfano
 
yote tisa njooo huko mjini mwanza matawi ya kenyatta na lile la PPF du haiseee banki wameweka watu wasio na uchungu wala utashi wa kutuhudumiaa mfano nilikua Mwanza mjn mwanzon mwa ile promotion yao ya weka na ushinde nkawa cjaelewa pikipiki na bajaji mle ppf plaza ndan ya banki zinafanya nini nkajua zinakopeshwa nkaenda kwa uyo LOAN officer yule mkaka kijana ivi nilijihc mjnga kwan nilimuuliza izo pikipiki na bajaji ni za nini mnakopesha au??? alichonijibu ni kakope pikipiki kinshen uku akizunguka kwenye kiti na kubonya simu hakujbu tena mpka alipokuja mwenzake ndo akanielekeza .
Toka siku hyo banki za mjn naziogopa kama majbu ndo yalikua yale kenyatta ndo usiseme mlinzi tu anakufokea helpdesk ndo usihata songee wanaangalia sura na mavazi.......
yani isingekua mishahara hili libank ngewaachia
 
Mimi pia nilitaka kufungua account katika tawi lenu la sengerema lakini nilikutana na mzee anaitwa gadagada majibu aliyonipa nikabaki kuchukizwa na kuondoka tu.

hivi ndio mnawafundisha wafanyakazi wenu mbinu za kuwahudumia wateja kweli.na anatoa wapi kiburi cha kuwajibu wateja atakavyo.kumbukeni crdb yuko pembeni pale atachukua wateja mkabaki na wafanyakazi wa serikali tu..
 
NMB Tanzania hongera sana kwaa kuja jf!
_Hakuna bank yenye huduma nzuri za mikopo nzuri hapa Tanzania kama NMB nishakopa bank nyingi sijaona kama NMB!
__Tatizo moja tu rushwa rushwa idara ya mikopo..
mi niko mwanza nshakopa mara nyingi na hakuna wakati sijatoa rushwa tena afisa analazimisha kama tumefanya naye biashara

Mtaje huyo afisa na kiasi ulichotoa kila ulipopata mkopo.
 
Last edited by a moderator:
Sisi waalimu na mapolisi tunataka ATM special kwa ajili yetu.foleni zinatupa vigimbi
 
😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Mbona sisi Wateja wa Nmb tawi la Ngudu tumesitishiwa Huduma ya mikopo bila sababu maalum tunaomba tufahamu lini Huduma hii itarejeshwa hapa ngudu
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe Siri)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Mnatuumiza sana, makato yenu ya mikopo kwa wafanyakazi ni makubwa mno. Awali kwa baadhi ya viwango mlikuwa mnakata 140, 155 bado hamkulidhika mkaano wateje wenu wanafaidi mno mmeongeza mnakata kalibu172,000. Mshahara wenyewe kiduchu,huyu mtu abakiwe na nini, hivi hamuoni huruma, hivi ni kweli mkipunguza mnapata hasara au ni uroho wa kutotosheka na pesa? pesa mnazo tena mnachezea lakini bado mnaumiza watu. Kwenye ATM ukiingiza tu kile kikadi mmekata 600 na kuendelea.

Hivi ni kweli mnatoa huduma kwa watu au mpo kujinufaisha? Hatukatai msitafute fedha lakini angalieni na wenzenu.

Walisema hii ni benki ya masikini, masikini gani mnaowasaidia au niji wenyewe benki ndio mmegeuka kuwa masikini? Waoneeni huruma watu. Naacheni majibu ya kisiasa yenye dharau ndani yake.
 
Nilichukua mkopo NMB Temeke 2009 -2012 nikamaliza.

Miezi mawili baadae wakaanza kunikata tena kiwango tofauti kwa awamu mbili nikaenda kuwasilisha malalamiko yangu pamoja salary slips zangu karibu zote kuonyesha jinsi nilivyokatwa na kumaliza mkopo, imechukua zaidi ya mwaka bila mafanikio yeyote pamoja na kupeleka malalamiko kwa meneja wa tawi mwisho nika give up , ila nikaapa kutofanya huduma zozote za mkopo na NMB naogopa usumbufu kwenye mshahara ila kama ingewezekana hata a/c ya mshahara ningehamisha.
 
pelekeni ATM udom school of humanity watu wanapata tabu mno mpaka waende social science
 
Back
Top Bottom