NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hivi hii benk ya nmb ni ya vigogo wa serikali nini. Mbona kila tawi folen sana alafu jitihada za kuipunguza hazipo. Eti kahama nzima nmb ni moja tuu sehem mhimu zenye ela kama isaka hata itm hamna duuu. Maboss wa nmb hampo makini..
 
Nmb ni majanga benki ya wakulima...

Wateja pomoni mpk mnashindw kuwahudumia vijan wanakaa mtaan elimu wanazo mnashindw kuajiri branch inakuw na teller mmoja au wawil mnakaz ya kuandik closed closed bila aibu mkijua watu kazi hawana zaid ya kuja kuwapangia foleni..

Naichukia hii bank kwa moyo wote wafanyakaz nyodo mpk wanakinaisha.
Hamjibu uzi mmeleta wa nn km co vihiyo tu...
 
Jana nilifika benki NMB Mbinga nimesimama katika foleni masaa matatu ATM ni moja nyingine ni mbovu nayo inayofanya kazi inasuasua niliingia kwa teller napo niliganda kwa saa moja jumla ni manne pia ukitumia nmb mobile pesa unatoa leo unaipokea kesho hii ni kwa mpesa mwanzoni huduma zilikuwa safi naomba mboreshe huduma zenu nchi nzima mwezi ujao nitaenda tena tarehe za mwisho wa mwezi kuangalia maboresho yenu hali ikiwa hivi nahamia benki nyingine masaa manne ni mengi sana kwenye foleni naomba badilikeni bora muondoe atm mashine tulipwe kwa teller kama zamani mnaharibu ratiba zetu au mnataka tulale benki.
 
Kwa kweli nmb mnacampaign za uongo kuusu ku topup.Mtu ana topup mnasema mnafuta mkopo wa nyuma lkn unajikuta umeanza upya na riba kubwa zaidi ya asilimia mnazotaja.Mm nina mkopo milioni10 narudisha milioni 15.7.Hii si zaidi ya nusu?.
 
Hivi mtu akitumia humuna ya Nmb mobile mfano ukitoa laki1 unakatwa shilling ngapi?
 
Oya @nmbtanzania inakuwaje mimi nina salio kwenye akaunti halafu nataka kununua salio nmb mobile mnasema salio halitoshi?
 
Kuna haja gani kuanzisha huduma ya kutoa huduma kwa haraka kwa baadhi ya watu? Hamjua kuwa kila Mtanzania ana haki ya kupata huduma ya haraka? Sikieni kama kweli mnataka kuendelea kuwa namba moja Tanzania na Afrika kwa jumla jitahidini kuwa na huduma za haraka kwa kila mteja wenu.

Unaingia benki ya NMB, mfano pale Magomeni unakuta kuna madirisha ya kutoa huduma kama sita hivi, ni moja tu ndilo linalowahudumia wateja wa kawaida wanaotaka kuweka na kutoa fedha hii si sawa. Huwa ninajiuliza kwa nini mmetengeneza madirisha yote hayo?

Pili naomba mpime uwezo wa watoa huduma wenu, wawekeeni hata kamera mahususi mjue kuwa siku wametoa huduma kwa watu wangapi ili litakuza ufanisi wa kazi.
 
Kuna taarifa kuwa kw sasa ku-renew mkopo hadi kufikia miezi 12 badala ya sita kama ilivyokuwa, je ni kweli?
 
kwenye kutop up nmb ni wezi na wanawadanganya walimu wasioelewa mambo yakoje.Pia wanatoa mikopo midogo sana ambao hauwezi kumtoa mtu kimaisha backlays ndo habari ya mjini
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Mna huduma mbovu sana. Sina mpango wa kubaki NMB. Kwanza huduma yenu ya NMB MOBILE sio nzuri kabisa unaweza ukatoa fedha na usizipate kwa wakati. Pili matatizo ya watena yanachukua muda mrefu kutatulisa
 
Eeeeh mie tokea niombe card yapata four weeks hakuna kinacho endelea wizi mtupu.by Marco
 
akaunt inasoma salio 8,524.afu chini kiasi kilichopo ni 5,205.mbn sijawaelewa hapo?
 
Bravoooo
NMB mmethubutu.

Kwa hili nawasifu na nategemea mtapata matokeo chanya ya kuendeleza/kukuza benki yetu.
 
Its the worse bank i never believe it can be will never bank with u no more
 
Mimi niliwahi kukatwa karibu laki 2 kwa makosa. Wenyewe NMB walikiri hilo kosa. Ila mpaka leo (muda wa miaka miwili) sijarudishiwa hiyo hela. Nipo CRBD tu. Hawa wanajua kazi yao.

Halafu kwanini hamleti visa au mastercard? Mtu ukienda nje ya nchi, inakuwaje?

NMB sucks!
 
Back
Top Bottom