NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

nafikiri jamaa waliofungua huu uzi wamesimamishwa kazi...si unajua msemaji ni mzungu!!!
hali imechafuka
 
NMB MOBILE Ni majanga! mbona gharama za kutuma pesa ziko juu? nimetuma juzi tsh 22,000 nimekatwa elfu tatu? kweli hii ni halali?
 
Ninaswali moja la kuuliza na ushauri pia. Nikianza na swali, ni hivi, nilifungua account ya mke wangu 2012 au 2013 katika tawi moja hivi hapa nchini, katika kipindi cha kusubiria card (ATM) usumbufu ukajitokeza hadi mke wangu akaanza kuwa mkali kwa wahudumu maana ahadi zilizidi sana ikabidi ni mtulize kumwambia awe mvumilivu.

Ilishindikana kabisa kuipata tukaambiwa tuanze upya kufanya utaratibu wa kuomba card kisa document hazionekani. tukajitahidi kuwaletea document walizohitaji ile karatasi unayopewa mara ya kwanza kama temporary lipo na linatumika kuchukua hela dirishani, ikatokea tumesafiri kwenda mkoa mwingine lile karatasi wakalikataa kuchukua hela, tukaamua kuachana nao ila hela ilibaki kidogo kama 70,000/-, je, naweza kupata hizo hela?

Ushauri wangu kwenu ni kuhusu bank statement kwenye NMB mobile, ipo shallow sana mistari mitatu minne halafu maelezo hayajitoshelezi, naomba ionyeshe fedha iliyoingia toka wapi na tarehe gani. kwa leo ni hayo machache.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe “Siri”)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Pesa fasta majanga meseji za confirmation code haziji na muda mwingie unataka kutuma pesa unaambiwa externa application down na hayo matatizo hayatatuliwi kwa wakato
 
Huyo dada namfahamu ni bonge la mpuuzi, sijui anajiskia ili iweje.
 
nmb hamjali walemavu, wajawazito na wazee. Utakuta mmojawapo wa niliowataja jasho linamtoka yuko kwenye foleni ya kuweka pesa mpaka anatia huruma. Na kwa sababu ya foleni kila mtu kajikausha hakuna wakumhurumia.

CRDB morogoro kwa mfano wakiona aidha mlemavu, mzee au mjamzito ameingia atapokelewa kwa upendo na kushikwa mkono mpaka dirishani na atapewa huduma baada ya mteja aliyemkuta anahudumiwa. Hilo tu lilinifanya nikatua CRDB.
 
jamaa anapiga kazi mpaka raha
yaani mchangamfu kwa mweli mwasandube hongera sana
mi nkifika yaani nkimkuta naenjoy sana the guy mzuri mnoo very responsible
ila mlokole yule anapiga maji kidogo

Alafu Mshikaji ana kasi nzuri sn. Bora nipange foleni kwa Mwasandube mwenye watu 10 kuliko kwa mwengine mwenye watu 4
 
Nataka Mkopo wa Mshaara Formula ipi inayotumika. Hii itanisaidia kuweza kujua kiwango kipi Niombe
 
kwa msomi hakuna kitu kinachohangaisha kama kufanya utafiti ili kupata ufumbuzi wa jambo fulani! itashangaza nmb kufanya utafiti eti kujua matatizo yao! nenda tawi lo lote tz utagundua tatizo lao kubwa ni kukosa ubunifu! njoo tbr ujionee vituko! ni mwisho au mwanzo wa mwezi, watu wamejaa, counter zipo nyingi lakini wahudumu ni wawili au watatu!

ukiingia benk saa 3 kutoka ukiwahi ni saa 8!joto ndani kali lakini hata kuwasha feni mpaka wakumbushwe! nawashauri nmb muweke migahawa na grocery kwenye matawi yenu, mtauza sana!
 
nmb mnajitahidi ila kero moja mnayo, NMB MOBILE NA ATM ZENU MWISHO WA MWEZI NI KERO TUUUUUUPU, HERI UENDE UKUTE FOLENI LAKINI SIO KUKAA FOLENI MWUSHONI UNAKOSA HELA... JIREKEBISHENI
 
Tatizo kubwa na lililo sugu kwenu ni Rushwa hasa Loan officers wenu, toa chochote ili update mkopo mapema, naongea kwa sababu nimefanya utafiti , Hongeleni kwa hii thread
 
mwajitahidikufika kila halmashauri lakini mwajua idadi ya wateja na kipindi gani wanafurika (mwisho wa mwezi) ila bado hamuandai mkakati wa kuwahudumia kwa haraka, wakuta tellers zimefungwa na hata huyo mmoja aliyefungua anasogoa tu na mwenzie aliye dirisha la pili! foleni rekebisheni
 
hongereni. nmb ni benki yetu watanzania tulio wengi hasa wa vijijini. kero kubwa kwangu ni mashine za kutoa zenyewe(ATM) kukosa pesa au baadhi yake kutokufanya pesa. jitahidini kuhahakisha kuwa mashine zote zinakuwa na pesa muda wote na zinafanya kazi.
 
Kadi ikiexpire wakti mteja yupo mbali na tawi alilofungulia akaunti anaweza kusubiri mwaka mzima bila kupata kadi yake. Yani mnaboa sana. Yamenikuta mara mbili sasa.
 
Huu ni mfano wa kuigwa. Taasisi zenye uongozi imara ziko hivi. Nakupendeni sana NMB. Nina akaunti kwenu (japo mimi si mwalimu) mwaka wa saba sasa. Na sijawahi kujuta.
Kwani nani kakwambia kuwa watu wenye account NMB ni walimu peke yao?
 
Hongereni Nmb bank shida kubwa bank yetu ya Kasulu baadhi ya watumishi wanaibia Wateja hela kwa visingiziombalimbali mf.ukienda kuchukua pesa ukawaamin usihesabu wanakuibia au nyakati za kuweka na jambo lingine punguzeni riba
 
Foleni imezidi na watu kujazana bank bila sababu watu wanatapeliwa ndani ya bank bila wasiwasi.
 
Back
Top Bottom