Mimi imenitokea mara mbili nikitoa pesa kwenye ATM inatoka pungufu zaidi (wakati mwingine nusu) ya kiasi nilichoingiza wakati wa muamala. Na kama nisingehesabu pesa papo hapo kama wengi wetu tulivyozoea kwa kuziami ATM, ningesingizia uchawi.
Maana hata baada ya kupeleka malalamiko kwenye uongozi wa benki nilitakiwa kujaza fomu halafu nisubiri baada masaa 24 ndipo kiasi cha pesa kilichozuiwa na ATM kitarejeshwa kwenye akaunti.
Sasa maswali:-
Kwanza, je nisingegundua kuwa ilikuwa tatizo la ATM ingekuwaje?
Pili, je, kama ni weekend mfano Jumamosi jioni halafu ninadharura, au ninasafiri ningefanyeje?
Tatu, je, pesa iliyokatwa kwenye ATM hamwezi kuirejesha kwenye akaunti yangu bila kujaza fomu?
Nne, je tatizo hili hamwezi kulitatua? Maana kwa upande wangu limenitokea kwa nyakati mbili tofauti, tena kwenye matawi mawili tofauti.
Tano, nina akaunti kwenye baadhi ya benki pia lakini mbona kwenyewe hakuna risk kama hii?