NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu wapendwa ningependa kufaham mambo muhimu/Msingi ya kuzingatia hasa baada ya kufungua hii Fixed Deposit account

Je?
1. Unapewa mkataba baaada ya kuifungua ya kiasi cha pesa ulichoweka Na utakachopata?!

2. Endapo kama ikifika Muda let say 3 monthes after depositing Na hawaja kuongezea io RIBA taratibu ni zipo

Naomba wataalam wanisaidie Na vitu vingine zaidi

NB: kama hujui subiri tuje kujuzwa Na wanaojua kuliko kupost Mambo mengne

IKo hivi, unatakiwa kwanza uwe na akaunti ya kawaida (personal account ) ,kisha unaweka pesa kwenye hiyo akaunti.

Baada ya hapo unaingia mkataba wa fixed account, mkataba huo unakuonyesha kiasi unachoweka kwenye Fixed account na muda ya kukomaa(maturity ) wa pesa yako na kiwango utakachopata baada ya kodi.

Hela itaatolewa toka kwenye account ya kawaida na kwenda kwenye akaunti ya fixed na baada ya muda wa kukomaa kufika pesa hiyo pamoja na faida itarudishwa kwenye akaunti yako ya personal /binafsi
 
Nimeshangaa sana, mwipwa wangu ana mkopo NMB sasa CRDB waliomba barua ya NNB ikionyesha mkopo anao daiwa cha ajabu sasa ni siku ya 5 leo (siku za kazi) wanamzungusha tu, sasa najiuliza inamaana hawataki awahame au wanaleta usumbufu ili wengine wajifunze kuwa kununua mkopo sio rahisi au. huu sio ungwana, maamuzi ya kuchukua mkopo ni maamuzi ya mtu binafsi haihitaji ushawishi na isitoshe sio lazima mtu abaki kwenye benki flan akihitaji kupata huduma flani.

NMB baada ya mahesabu walimwambia ku top up mkopo watamps sh mil 2.9 ila CRDB baada ya hesabu wanampa mil 5. saas kwanini asihame? bishara ni ushindani sio kuwakomoa watena.

Ujumbe huu uwafikie nafahamu wamo humu wanausoma kesho barua isipotoka tutawaanika mengine ya huduma zisizo ridhisha halafu waje waseme ni wivu.

MESSAGE DELIVERED
 
kumbe hela yenyewe ya MKOPO; ? yaani unahamisha Deni? Huko unakopeleka kuna mufilisi mubaya sana hiyo 5 utaja lipa 8 !
 
eti mtu anakuja mnamwambia eti sisi tunatoa mikopo mizuri lazima mtarudi tu hapa kweli mbona mmeshindwa kuwapa watu pesa nyingi kwa kiwango cha makato yaleyale ila wengine wanatoa hela nzuri kwa makato yale yale. lazima wateja wa mikopo wapungue
 
kumbe hela yenyewe ya MKOPO; ? yaani unahamisha Deni? Huko unakopeleka kuna mufilisi mubaya sana hiyo 5 utaja lipa 8 !
sasa akilipa Mil. 8 kuna tatizo gani? Hakuna anayepata maendeleo bila mikopo. hata akina Mengi wana mikopo ya mabilioni ya fedha katika taasisi za fedha. Sasa kama wewe hutaki kadundulize vi laki moja moja yako then uone zitakuja kutosha kujenga baada ya miaka mingapi.
 
Ungeandika tawi la wapi wamefanya hayo ingesaidia kwa haraka mabadiliko. Hizi bank bila ya rushwa makisio ni hafifu.
 
Ungeandika tawi la wapi wamefanya hayo ingesaidia kwa haraka mabadiliko. Hizi bank bila ya rushwa makisio ni hafifu.
swala sio tawi swala ni Benki wana utaratibu ambao ni mmoja kama wamepokea barua ya maombi ni benki zote lazima ziwe na mfumo mmoja tu, tawi hili haliwezi kufanya kinyume na tawi lingine maana sio makampuni tofauti na yanayo shindana ni kampuni moja na bosi wao mkuu ni mmosha
 
NMB nao waige kwa crdb,kuwepo na mikopo hadi wa miaka sana (miezi 84)
 
Hizi bank bila ya rushwa makisio ni hafifu.
Nenda kachukue mkopo kwenye matawi flan hivi ya NMB halafu umwambie ukitoka haraka ntakupa laki 2 au laki uone kama hutaambiwa mkopo umejibiwa kesho, niliwahi ambiwa eti kuna foleni inabidi nisubiri watu ni wengi wanaoomba nikasubiri sipati jibu mwisho wa siku nikamwambia utakata laki yako humo mbona sikukaa siku 1 nikaitwa eti tayari umepitishwa ahaha NMB hiyo hiyo sio nyingine. sasa inabidi niwatolee uvivu maana mwipwa wangu amechoka kusubiri, hata leo amesema ataenda kuulizia mchana tena kama barua tayari na isipotoka naweka laivu tena mambo yao ya hovyo
 
NMB nao waige kwa crdb,kuwepo na mikopo hadi wa miaka sana (miezi 84)
wataweza, toka lini wakaenda na wakati hujui wao ndio ZANTEL walioanza na ZPESA wakashindwa kuendelea wengine wakachukua nafasi hiyo leo wako mbali. acha walale tu halafu utasikia benki zinapitia hali ngumu kumbe wanashindwa kuingia kwenye mfumo wa ushindani ambao unahitaji kuwa fasta sio kulala. nadhani/ nahisi sina uhakika ila ilnaweza ikawa hivyo Marketing Manager wao na anayehusika na ku design product wana hongwa sana ili wasiende na kasi
 
wataweza, toka lini wakaenda na wakati hujui wao ndio ZANTEL walioanza na ZPESA wakashindwa kuendelea wengine wakachukua nafasi hiyo leo wako mbali. acha walale tu halafu utasikia benki zinapitia hali ngumu kumbe wanashindwa kuingia kwenye mfumo wa ushindani ambao unahitaji kuwa fasta sio kulala. nadhani/ nahisi sina uhakika ila ilnaweza ikawa hivyo Marketing Manager wao na anayehusika na ku design product wana hongwa sana ili wasiende na kasi

Inabidi wachunguzwe,wasije ua benki ya walalahoi
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.


Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

NMB
Kutokana na trend ya mikopo kwa watumishi inavyoenda,tunaomba muongeze miezi ya kukopa kama benki nyingine ifikie miezi 84,ili kutupunguzia adha ya kuhamisha madeni kwa taasisi zingine.

Pia riba mshushe pungufu zaidi yao,au mlingane. Hali ni mbaya ya maisha. Msiwe na mioyo migumu.
Mteja wenu wa tangu mnaaza.
 
Back
Top Bottom