NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Mimi nauliza, hivi nalipishwa shillingi ngapi kwa siku kwa kumiliki NMB ACCOUNT?

MAANA niliweka Akiba yangu she 36000/= BAADA ya miezi 3 nilpewa Salio LA sh 1300/=
AMBAPO hiyo hela Mimi sikuitumia kabisa
 
Ndugu WA Nmb naomba Maelezo AU ushauri.

Nliweka akiba sh 38000/= NMB. Baada ya miezi 3 kuuliza Salio naambiwa Salio lako ni sh 1369.00 kwa kipjndi chote Hicho nemewahi Nunua muda wa maongezi sh 1000/=tu.

Swali langu ni kumiliki Accounts MMB UNALIPIA SH NGAPI KWA SIKU KUTUNZIWA HIYO ACCOUNT?
 
Salaam Radavi,
Tunajitahidi kukufikia kwa kuweka huduma mbadala za NMB Wakala na NMB Mobile karibu yako zaidi kuwezesha kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi.
Naomba kujua kama kuna gharama zozote kujisajili na NMB mobile.

Na gharama yake kwa mwezi mnakata shs ngapi kuwa kwenye hiyo huduma
 
Naomba kujua kama kuna gharama zozote kujisajili na NMB mobile.
Na gharama yake kwa mwezi mnakata shs ngapi kuwa kwenye hiyo huduma
Salaam,
Hakuna gharama za kujiunga na NMB Mobile na pia haina makato kuwa kwenye hiyo huduma. Karibu sana.
 
Huduma ya salary advance imekataa kufanya kazi kwangu na mshahara wangu unapitia NMB Bank tatizo ni nini ? .

Na ukiangalia kiwango unachostahili kukopa inakuonesha vizuri kabisa
Pole sana, una akaunti ya aina gani? na ni mara ngapi unaomba huduma hii. Tunaweza kukusaidia zaidi kupitia PM, karibu sana
 
Nimeipenda sana huduma yenu ya Advance Salary.

Tafadhari msiiondoe, inatusaidia sana sisi wa kipato cha chini.
 
Salaam NMB,. Vipi huduma ya mikopo ya vikundi mmeshaanza ?
 
Nauliza kadi yangu iliisha muda wake miaka3 sasa na sikuweza kwenda kuichukua kutokana na umbali. Je naweza kwenda kuchukua kadi mpya au kwa muda huu Itakuwa imezuiliwa
 
Naomba kuelezwa kigezo cha salary advance,,mm ni mwajiriwa mpya na nna miez nane 8 kazin mshahara wangu unapitia NMB je nipo eligible kupata salary advance???
 
Nmb Bank Zipo Popote
Wewe Unatakiwa Ufanyiwe Kazi Kwenye Mtandao
 
Habari za majukumu wakuu..

Niende moja kwa moja kwenye mada.. Naomba kwa mwenye kufanya kazi nmb au mwenye mtu anaefanya kazi kwenye hiyo bank ani PM maelezo yote nitampa huko na akiweza kunifanyia kazi yangu nitampa chochote. Nawakilisha...
"Rushiwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushiwa" Hii ilikuwa ahadi ya Mwana TANU
 
Tafadhali naomba kufahamu Je tofauti na makato ya miamala kama kuangalia salio, kuhamisha fedha nk, akaunti ya NMB inamakato ya kila mwezi?
Kuna mteja wenu analalamika kila akiingiziwa fedha katika account yake lazima akatwe 2000.
 
Last edited:
Back
Top Bottom