NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hadi dakika hii bado barua haijaandikwa, yani kitu cha dakika 5 kinachukua siku zote hizi wana maana gani
 
Nature ya kazi yangu napata Ration Allowance kila katikati ya Mwezi. Mwezi uliopita nilikopa Salary Advance kiasi cha sh. 100,000 ajabu ipoingia Allowence walikata mkopo wao. Sasa nachojiuliza nilikopa salary advance au Allowence advance?

Ina maana kumbe ile riba ya 6% ni kwa wiki 2, Hii ina maana Riba ni 12% kwa mwezi....NMB acheni utani na Fedha bana
 
nyie NMB mnaubia gan na loan board...mwezi uliopita nilienda kurenew nmb mobile password mana nilikua nimesahau cha ajabu si mkapeleka jina langu loan board ghafl nashangaa nakatwa pesa....kwanza aliewaambia mpeleke jina langu nani? acheni usenge maisha yenyewe magumu haya..pumbavu kabisa nyie

Ila mkuu kama ulikopeshwa ukasoma kwanini usilipe? Unategemea wengine watasomaje endapo wewe ukigoma kulipa? Chochote kinachoitwa mkopo ni subjected to repayment mkuu
 
Hawajibu chochote
Bora tujibiane wenyewe

Nauliza swali huu mpango wa nmb kununua madeni ya bodi ya mikopo helsb je unawasaidiaje watu au faida zake ni zipi?

Yani nmb wakinunua deni langu Mimi napata unafuu gani?
 
Naomba kujua kama naweza fanya money tranfer from nmb to crdb kwa atm
 
nyie NMB nyie sina hamu na nyie kabisa nlifungua account chap chap baada ya kuambiwa account ya mwanzo imefungiwa sasa namba yangu simu hamjaifuta toka mwezi wa saba mpaka sasa hivi haijafanyiwa chochote na yale mabarua mlionisumbua kuandika
Mimi kwenye ku upgrade kutoka chap chap kwenda Personal savings account, waliniambia ili niweze upgrade inabidi niwapelekee barua za mwenyekiti na mtendaji sijui,

niliwapelekea nikakaa weee naona kimya hamna kilichobadilika!! sasa nilirudi pale Branch nilimzingua yule dada nikamwambia hata sisi pia tuna shughuli nyingi za kufanya sio mnasumbua watu matokeo yake hakuna kinachofanyika!! bac nilikaa two days waliifanyia kazi!!
 
Bora tujibiane wenyewe

Nauliza swali huu mpango wa nmb kununua madeni ya bodi ya mikopo helsb je unawasaidiaje watu au faida zake ni zipi?

Yani nmb wakinunua deni langu Mimi napata unafuu gani?
Faida zake, ukiwa na mkopo wa loan board huwezi kufanya top up kwa hiyo ukihamishia Nmb unakuwa mkopo wa kawaida hivyo unaweza kufanya top up.

Loan board inakata moja kwa moja toka kwenye mshahara wako hivyo inapunguza room ya mkopo, kwa mfano mshahara wako ni 100,000 makato ya loarn board ni 15000 kwa mwezi kwa hiyo ukienda kuomba mkopo watapigia hesabu 85000 na sio laki 1 hivyo kama ulikuwa unaweza kukopa Milioni moja kwa mshahara wa laki 1 kiwango hicho kitapungua.

kwa utaratibu wa loan board mshahara ukiongezeka na makato yanaongezeka ila ukiwa ni mkopo wa kawaida makato yatabaki pale pale.
 
Tawi la kariakoo mnaboa sana yena mno tena vibaya vibaya......Teller ziko 4 au5 lakini uyakuta Cashier mmoja au wawili mnaboa sana itakuta wanamuacha Wakala ndio tuweke au kutoa .....sehem kama ile inabid mue shap kusiw na folen, si chini ya mala moja nimeghaili folen kubwa
Hata Magomeni wanazingua hivyovyo.Jana nimeshinda pale.
 
Bora nyie mnaotokea hapa jukwaani kwa ajili ya kukidhi kiu ya maswali na ushauri kwa wateja wenu
Maana wenzenu NBC wako hoi kitandani na hawana hata habari juu ya yale yanayoandikwa kwenye mitandao juu ya benki yao
Hongereni sana kitengo cha mawasiliano kwa umma NMB kwa mrejesho huu mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya taifa hili
Natamani taasisi zote zikaiga mfano huu
HEKO NMB HEKO TANZANI
 
Nasikia kuna zonal manager mpya amekuja nmb dar zone ameandaa sala maalumu watakayotumia kusali asubuhi madhehebu yote ie wakristo na waislam which sio mbaya, ishu ni kwamba huyo manager analazimisha wafanyakazi waikariri hiyo sala, hapo ndio naona sio sawa, naona kama ni kuingilia imani za watu, hadi wafanyakazi wanafanyishwa test ya sala kuhakikisha kama sala imekaa kichwani, hakuna vitu vya kukariri/kufanya mpaka wakakariri sala za asubuhi? hii imekaaje? @NMBTanzania
 
Maeneo ya tazara kama unakuja mjini unakutana na atm moja eneo la kamata katikati ya mataa njia panda ya veta na ya kamata. Je hili ni sawa katika kutoa huduma kwenu mbona wenzenu wametapakaa njia nzima haswa kwa ma maduka makubwa
 
Hivi nyie watu wa jf haya masuali yenyu huwa mnajibiwa au mnajijibu wenyewe?
 
Maeneo ya tazara kama unakuja mjini unakutana na atm moja eneo la kamata katikati ya mataa njia panda ya veta na ya kamata. Je hili ni sawa katika kutoa huduma kwenu mbona wenzenu wametapakaa njia nzima haswa kwa ma maduka makubwa
Salaam Radavi,
Tunajitahidi kukufikia kwa kuweka huduma mbadala za NMB Wakala na NMB Mobile karibu yako zaidi kuwezesha kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi.
 
Huduma ya salary advance imekataa kufanya kazi kwangu na mshahara wangu unapitia NMB Bank tatizo ni nini ? .

Na ukiangalia kiwango unachostahili kukopa inakuonesha vizuri kabisa
 
Hizi kadi zenu za chapuchapu inapofikia mteja anataka mkopo kwanini lazima aibadilishe wakati ni kadi zenu na mnaendelea kuzitoa?

Na pia masharti ya kuzibalisha kwanini yanakuwa magumu wakati mteja ni yule yule alisajiliwa nayo na taarifa zake mnazo?
 
Back
Top Bottom