Kuna haja gani kuanzisha huduma ya kutoa huduma kwa haraka kwa baadhi ya watu? Hamjua kuwa kila Mtanzania ana haki ya kupata huduma ya haraka? Sikieni kama kweli mnataka kuendelea kuwa namba moja Tanzania na Afrika kwa jumla jitahidini kuwa na huduma za haraka kwa kila mteja wenu.
Unaingia benki ya NMB, mfano pale Magomeni unakuta kuna madirisha ya kutoa huduma kama sita hivi, ni moja tu ndilo linalowahudumia wateja wa kawaida wanaotaka kuweka na kutoa fedha hii si sawa. Huwa ninajiuliza kwa nini mmetengeneza madirisha yote hayo?
Pili naomba mpime uwezo wa watoa huduma wenu, wawekeeni hata kamera mahususi mjue kuwa siku wametoa huduma kwa watu wangapi ili litakuza ufanisi wa kazi.