NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hiv malalamiko tunayotoa mnayafanyia kazi au unatizama tu Na kuacha kama ilivyo kama unayafanyia kazi mbona hatuoni mrejesho.Hii inaziilisha kuwa huduma zenu mbovu hata kujibu humu unaitaji kujiandaa

Wayafanyie kazi kwa lipi?
Ushaina hata admin wao akijibu hata msg moja hapa? Mshahara wanaopata kwn bank ya baba yao hiyo,
Wewe unafanya kazi kazura mimba halafu unaleta nyodo, sana sana watakufungia ki acc chako cha tgs d na mikopo ya Bayport ya kutosha ufuate mshahara kigoma mjini ndio akili itakuingia.

Chezea bank za bongo wwe!
 
Swali langu ni kwamba kuna dhuluma au wizi mnaufanya nyie nmb iko hivi nikitaka kuangalia mathalani salio kupitia nmb mobile mnaniletea ujumbe kuwa huduma hii kwa sasa haipatikani jaribu tena baadaye lakini vocha yangu ya kwenye laini imekatwa na kupungua.

Sasa huu si wizi wa hila,iweje sikuhudumiwa lakini pesa yangu ikatwe?
 
Tawi lenu la Ngarenaro Arusha Huduma ni hafifu haswa...haiwezekani tellar 2 ndo wanafanya kazi ....meneja uko wapi
 
Nawapongeza NMB kwa huduma na kazi yenu njema,mnayoifanya.
Naomba kutoa ushauri juu ya tawi lenu la mlimani city.

kumekuwepo matukio mbali mbali ya wateja wanaochukua fedha
nyingi kufuatwa na kufanyiwa uharifu, na hata wengine kuuawa
na kuporwa fedha, naomba nieleweke kuwa silaumu mtu kwani.

sina ushahidi wa wazi kwamba wizi huo unaasisiwa na wafanyakazi.

Ushauri wangu ni huu ili kurudisha imani kwa wateja ambao hudhani kwamba ni mbinu zinasukwa na watoa huduma.

sina uhakika kama kuna sheria inayombana mtoa huduma
kutotumia simu awapo ndani ya benki kama inavyotubana sisi wateja.
kama hiyo sheria ipo basi izingatiwe kwa msisitizo,kwani simu ni hatari kwa mteja.

anayetoka na fedha nyingi bila escort ya polisi.

Pia wasimamizi wa kamera za usalama wa benki,waangaliwe
kwa jicho la tatu,sehemu nyingi kamera huwekwa.

kila sehemu nyeti ikiwepo kaunta ambapo ndipo wateja huchukulia fedha.
msimamizi wa kamera kama siyo mwaminifu ni rahisi kuangalia
ni nani kachukua kiasi kikubwa cha fedha na kufanya mawasiliano
na wenzake wasiowaaminifu ili kufanya uhalifu.
Ombi langu ni kwamba kwa kuwa walinzi hawa hawako busy sana kama ilivyo watu wa kaunta
wanaweza kuutumia mwanya huo kufanya uhalifu,na pindi malalamiko yanapo
tokea wao huonekana hawahusiki kwani ni rahisi kuwasahau kwamba nao wana nafasi
kubwa ya kumuona mteja aliyechukua fedha nyingi,sawa na mhudumu aliyemhudumia huyo mteja.
Naomba idara hiyo ya kamera isimamiwe na kuwekewa sera madhubuti ili kupunguza
uwezekano wa wateja kuibiwa na kuharibu heshima ya benki.
asanteni.
 
Nimekumbana na Tatizo pale NMB tawi la University , Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Nimeenda kuchukua hela kwa Cashier Laki sita, akanihesabia kwa Mashine, Kwa kumuamini sikuhesabu kwa mkono, Nilivyofika nje katika transactions nyingine nikakuta Haikukamilika, Imepungua Elfu Ishirini.

Waonyeni Macashier wenu Wasidokoe pesa za Wateja, Tukiwakamata huo Mtiti watajuta Kuzaliwa!
 
Usiamini cashier yoyote wa bank yoyote
Wamekuwa waizi vibaya sana,
Na mabenk yao wametulia kimya!
 
Mashine za ATM Mbagala hazitoi pesa kwa siku nzima ya jana 29 Jun 2015 bila taarifa kwa wateja kulikoni? Kama NMB inafilisika mseme tuondoke mapema
 
Hata Mbezi Mwisho (Mbezi ya Kimara) wangeweka ATM aisee


Wameweka ATM katikati ya kimara mwisho Na korogwe, kwenye kituo cha mafuta.

Tatizo sijawahi kukuta inafanya kazi halafu poor location Ni bora wahamishie kimara mwisho itahudumia watu wengi Na kwa urahisi.
 
Wameweka ATM katikati ya kimara mwisho Na korogwe, kwenye kituo cha mafuta. Tatizo sijawahi kukuta inafanya kazi halafu poor location Ni bora wahamishie kimara mwisho itahudumia watu wengi Na kwa urahisi.
Ile ATM ya Resort kwa kweli inatia uvivu ni bora ingekuwa Kimara mwisho. Sijui na pale kama upo na gari sharti uwe unaelekea mbezi tu na sio mjini,na kama upo kwa mguu pale sio safe kwa usiku
 
Binafsi sijawahi kuombwa hongo ila nna rafiki zangu wapo ruangwa-lindi wanamlalamikia sana afisa mikopo kuwa yupo corrupt mmmmnoooo.
 
Nimekumbana na Tatizo pale NMB tawi la University , Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Nimeenda kuchukua hela kwa Cashier Laki sita, akanihesabia kwa Mashine, Kwa kumuamini sikuhesabu kwa mkono, Nilivyofika nje katika transactions nyingine nikakuta Haikukamilika, Imepungua Elfu Ishirini.

Waonyeni Macashier wenu Wasidokoe pesa za Wateja, Tukiwakamata huo Mtiti watajuta Kuzaliwa!

Ni yule jamaa white??? Imeshanitokea tawi hilo pia, nilichukua 1.5milion ikapungu kama elfu30 hivi
 
Bunda idara ya mikopo tunasumbuliwa sana na maombi ya hela ya chai! Uongozi mara ya pili hii naandika ili mtatue tatizo hili ,kwa nini linaendelea?

Huyu bwana mweupe mrefu hela ya chai kaifanya kama mshahara wake!
 
Kadi zetu zikíisha muda tunaomba mfanye haraka tunapojaza form ya kad nyingine sana sana kwa sie ambao hatujafungulia branch hyo au wenye maisha ya kuhama hama
 
Nmb sina hamu nao japo mm ni mteja wao na yote hii ni kwakua sina namna nyingne. Kuna siku nimetoa mil 5 nikaondoka kufka home kuhesabu ili niwalipe waliokuwa wananidai nikakuta 120000 haipo iliniuma sana ila sikuwa na jinsi
 
Nmb sina hamu nao japo mm ni mteja wao na yote hii ni kwakua sina namna nyingne. Kuna siku nimetoa mil 5 nikaondoka kufka home kuhesabu ili niwalipe waliokuwa wananidai nikakuta 120000 haipo iliniuma sana ila sikuwa na jinsi

Ni uzembe wako kwann msihesabu hpo hpo
 
Nimejiunga na Nmb mobile .

Sasa kila nikipiga *150*66# kwa ajili kufanya mualama from my nmb account to my mpesa naambiwa" you have not enough funds to do this transactions .

Sielewi elewi na mbaya zaidi nipo mbali kutoka kwenye branch niliyofungulia account yaani nipo porini kabisa.
 
Back
Top Bottom