NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Imenichukua 3 weeks na bado hela hazijaingizwa wakati nimetimiza kila kitu. Magomeni branch Dar es salaam mwangalieni sana Joyce wa sehemu za miko
 
aise naomba kujua gharama za kuwa wakala wa nmb pamoja na faida zake
 
Hawa NMB wako ushingishi achaneni nao. Kwani benki ni moja ?
 
Huduma zenuu ovyooooo nimejiunga na NMB mobile lakini sipati chochote kinachoendelea

Miamala kupitia simu inashindikana nimewaeleza Sana lakini Hamna msaada wowote

Hata hili naamini mtapuuzia
 
nyie NMB mnaubia gan na loan board...mwezi uliopita nilienda kurenew nmb mobile password mana nilikua nimesahau cha ajabu si mkapeleka jina langu loan board ghafl nashangaa nakatwa pesa....kwanza aliewaambia mpeleke jina langu nani? acheni usenge maisha yenyewe magumu haya..pumbavu kabisa nyie
 
Mi naomba wimbo wa tangazo la WAJIBU.. nina mdogo wamgu analipenda sana hilo tangazo kwa wimbo wake
 
Hii ni moja ya benki za hivyo nchini. Hivi sasa hivi mikopo hamtoi au!? Manake huku Kwimba hii Benki ina urasimu usio na tija ktk suala la utoaji mikopo mf, rafiki yangu aliomba mkopo miezi mitatu ilopita na alikamilisha taratibu zote alizopaswa kukamilisha lakini wanamzungusha hajui hata kwa nini
duuuuh. . . . NMB jamani mbona mnaniangusha?
 
Naomba kuelimishwa kuhusu riba/interest za kwenye hizi benki zetu Tanzania hasa NMB yaan leo nimejaribu kwenda kurequest mkopo wa 7,500,00 naambiwa ntalipa milioni 13,600,00 wakati huo huo tunaambiwa riba ni 22% ni calculation za uchumi, wizi, unyonyaji au ni kitu gani?
duuuhhh . . . . sasa mkuu makato ya huo mkopo wamekuambia yatadumu kwa muda gani? mikopo hizi benki za Tz duuh . . . pasua kichwa
 
NMB mshirika wetu kwenye kuuza huduma ya umeme na malipo mengi tupo pamoja
 
Tawi la kariakoo mnaboa sana yena mno tena vibaya vibaya......Teller ziko 4 au5 lakini uyakuta Cashier mmoja au wawili mnaboa sana itakuta wanamuacha Wakala ndio tuweke au kutoa .....sehem kama ile inabid mue shap kusiw na folen, si chini ya mala moja nimeghaili folen kubwa
 
Mimi imenitokea mara mbili nikitoa pesa kwenye ATM inatoka pungufu zaidi (wakati mwingine nusu) ya kiasi nilichoingiza wakati wa muamala. Na kama nisingehesabu pesa papo hapo kama wengi wetu tulivyozoea kwa kuziami ATM, ningesingizia uchawi.
Maana hata baada ya kupeleka malalamiko kwenye uongozi wa benki nilitakiwa kujaza fomu halafu nisubiri baada masaa 24 ndipo kiasi cha pesa kilichozuiwa na ATM kitarejeshwa kwenye akaunti.

Sasa maswali:-
Kwanza, je nisingegundua kuwa ilikuwa tatizo la ATM ingekuwaje?
Pili, je, kama ni weekend mfano Jumamosi jioni halafu ninadharura, au ninasafiri ningefanyeje?
Tatu, je, pesa iliyokatwa kwenye ATM hamwezi kuirejesha kwenye akaunti yangu bila kujaza fomu?
Nne, je tatizo hili hamwezi kulitatua? Maana kwa upande wangu limenitokea kwa nyakati mbili tofauti, tena kwenye matawi mawili tofauti.
Tano, nina akaunti kwenye baadhi ya benki pia lakini mbona kwenyewe hakuna risk kama hii?
Duuuuhhh .....kuna siku nilikaa natoa laki 5 ikawa inakataa niliangaika sana baadae namuuliz wa pembeni yangu akaniambia toa laki nne na nusu alafu utoe elfu hamsini ujue nikashangaa sana kwa nini?.....nazan wapat faida c kila ukiw unatoa unakatwa percent ila sikuoenda hata kidogo
 
Ndugu wapendwa ningependa kufaham mambo muhimu/Msingi ya kuzingatia hasa baada ya kufungua hii Fixed Deposit account

Je?
1. Unapewa mkataba baaada ya kuifungua ya kiasi cha pesa ulichoweka Na utakachopata?!

2. Endapo kama ikifika Muda let say 3 monthes after depositing Na hawaja kuongezea io RIBA taratibu ni zipo

Naomba wataalam wanisaidie Na vitu vingine zaidi

NB: kama hujui subiri tuje kujuzwa Na wanaojua kuliko kupost Mambo mengne
 
Back
Top Bottom