NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Napenda kujua hivi ukichukua mkopo kupitia mshahara na umefanya marejesho zaidi ya manne unaruhusiwa kutop up mkopo yaani kuongeza mda wa kukopa tena
 
Msisina JANA NILIWAFATA WANIPE MKOPO WA 6M, WANAULIZA NINA LESENI,TIN,OFISI,TRA CLEARNCE FORM
nikajibu hivyo vyote Sina Ila
Nina dhamana isiyohamishika na wadhamini wapo na Nina uwezo wa kurejesha hiyo pesa.WAKASEMA SIWEZ KUKOPESHWA NIKASEMA ok NIKASEPA.
Daah hatari
 
NMB wana kamtandao kao flani wa matapeli wanaowadhulumu watu nyumba haswa kwenye mikopo. Wanasema hao maofisa wanacheza sana na wanunuzi au court brokers mwisho wa siku wanapotezwa.

Nina kaka yangu anakaa maeneo flani hivi sitaki kutaja jina, wamezika jirani yao juzi kwa michezo hiyo. Kuna maofisa wa bank walitafuta mtu wa kununua nyumba ya mnada wakazuga zuga kwa kutumia court brokers wakapindisha taratibu ile nyumba ikapigwa mnada wakadhulumiwa. Yule waliemdhulumu alisema ameonewa kila akifungua kesi mahakamani wanampindishia.

Trailer likaanza mmoja wa afisa wa nmb aliewachorea ramani hao matapeli alizama na boti na akanusurika kufa tanga hata miaka miwili haijaisha, mwengine alizika mtoto, akafata mzazi wake na mke aliugua sijui kama kapona, mwengine alieshiriki alivunjika miguu.

Naambiwa huyu alienunua nyumba amezika ndugu mmoja aliewahi kukaa kwenye hiyo nyumba na kila siku matatizo hayaishi humo ndani. Ndo juzi kaka ananiambia walipokua msibani minong’ono ni mingi.

Nikasema kama bank wanacheza michezo ya kudhulumu watu basi wataisha aisee. NMB fatilieni sana maafisa wenu
 
NMB taasisi maarufu sana kwa ulipaji wa mishahara ya civil servants wengi mnhini. Mnapokuea hamjapokea malipo hayo lawama huwa mnatupiwa. Vipi Hilo huwa mnalichukuliaje?
 
NMB mnachelewesha mshahara wa January 2021 wengine washapewa ila sisi bado. Sio vizuri.
 
NMB rekebisheni hichi kitu kwa wenye akaunti za dola kunashida moja kubwa ukitaka hela lazima uingie kwa teller ndani ndio utatoa hela kwa rate ya dola inayoonekana kwa siku hiyo mfano 2306 lakini ukitumia kadi kutoa kwenye ATM unapewa rate ya 2237,hiki kitu kimekuwa ni kero kubwa sana ukitaka kutohela usiku kama ni nyingi unapata loss kubwa kwasababu utatoa kwa rate ya 2237 sio 2300 naa, kwanini ATM hazitoi sawa na rate mnayoinesha?

hii ni kero na inasababisha wateja kufikiria kuhamisha account zao kwenda bank nyingine zinazotoa rates sawa kwenye ATM na kwa teller
 
Bank zenu hazitoi shilingi elfu 5, hivyo ikitokea una uhitaji wa elfu 45 au 55 huwezi kupata...! Boresheni hilo tafadhali
 
Lini mtaondoa gari la Mobile Banking pale Mji wa Nanyamba Mkoani Mtwara?. Huduma za ATM kwenye lile gari haziridhishi mara nyingi inakuwa imeharibika na kuleta usumbufu kwa wateja wenu.
 
Habari Njia gani nyingine ya kutoa fedha kwenye account ya nmb bonus account bila kupanga foleni ndan ya benki?
 
Punguzeni Riba ktk mikopo kwa watumishi wa umma ili wajikwamue kiuchumi.
wapeni mikopo mahsusi kwa ajili ya biashara na kununua vyombo vya moto, mtakuwa mmewasaidia kuwakwamua kichumi.
 
NMB wana kamtandao kao flani wa matapeli wanaowadhulumu watu nyumba haswa kwenye mikopo. Wanasema hao maofisa wanacheza sana na wanunuzi au court brokers mwisho wa siku wanapotezwa. Nina kaka yangu anakaa maeneo flani hivi sitaki kutaja jina, wamezika jirani yao juzi kwa michezo hiyo. Kuna maofisa wa bank walitafuta mtu wa kununua nyumba ya mnada wakazuga zuga kwa kutumia court brokers wakapindisha taratibu ile nyumba ikapigwa mnada wakadhulumiwa. Yule waliemdhulumu alisema ameonewa kila akifungua kesi mahakamani wanampindishia. Trailer likaanza mmoja wa afisa wa nmb aliewachorea ramani hao matapeli alizama na boti na akanusurika kufa tanga hata miaka miwili haijaisha, mwengine alizika mtoto, akafata mzazi wake na mke aliugua sijui kama kapona, mwengine alieshiriki alivunjika miguu. Naambiwa huyu alienunua nyumba amezika ndugu mmoja aliewahi kukaa kwenye hiyo nyumba na kila siku matatizo hayaishi humo ndani. Ndo juzi kaka ananiambia walipokua msibani minong’ono ni mingi. Nikasema kama bank wanacheza michezo ya kudhulumu watu basi wataisha aisee. NMB fatilieni sana maafisa wenu
Duh hatari sana hii mkuu. Lakini na sisi wakopaji tusilete janja janja sana. Tulipe tu mikopo ya benki.

Na nyie maafisa wa benki msijifanye kimbele front kama hele zenu.

Sie tukipanick tunawaroga tu. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

cc: mshana Jr.
 
Back
Top Bottom