NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kwann nmb msiwezeshe local fundi wanaojenga mashule na mahosipital kwa force acount
Maana malipo mnafanya conectin na almashauri malipo yanapitia kwenu mmakata pesa zenu hii imekaaje
 
NMB

KWANINI MNACHELEWA KUTOA KADI TULIZOLETA MZIFANYIE REPLACEMENT AU MNAFURAHI KUONA TUNACHUKULIA DILISHANI HUKU MAKATO YAKIWA MAKUBWA

TUNAOMBA MUONGEZE SPEED KWENYE UTENDAJI AU KWAKUWA MAGUFULI HAYUPO TENA NDIYO MUMEAMUA KUPUNGUZA SPEED
ACHENI USANII NA UKILITIMBA.
 
Kureplace kadi mnachukua mwezi mzima mbona wakati Rais Magufuli yupo hai hamkua lazy kiasi hiki au ndiyo paka akiondoka panya hutawala. Huyu manager wa tawi la Magomeni atumbuliwe haiwezekani watu wachini yake washindwe kuwajibika ingali yeye yupo.

Najua mnafanya hivyo ili tuendelee kutolea Dirishani au kwa wakala ili muendelee kufyeka pakubwa, jamani mishahara yetu yakuungaunga msitake tugawane hela zote yaani mnataka tutoke pasu wakati nyie wenzetu mnalipwa mamilioni.

Naomba mama samia amtumbue huyu manager wa tawi la Magomeni naona hajui kilichompeleka kazini maana tangu Mzee atutoke wanafanya kazi kimazoea Sana, ukiwapigia simu wanasema bado tunashughulikia halafu kadi zenu hazina uimara kabisa ukikaa nayo week moja inabanduka maganda au ukiikalia kidodo inajikunja yaani hadi equity wamewapiku kwa uimala wa kadi,sis wengine hatujazoe kuhamahama mabank Tunaomba muwajibike pia niwavivu Sana kupokea simu na kumsikiliza mteja, najua mnapage humu jf lakini hamjibu maoni ya wateja au nitapeli alifungua ile page nakuitelekeza.

Nawasalimu kwajina la jamhuri ya muungano.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Kwanini suala la bima ni ngumu sana kupata haki yako
 
Bora nyie mnaotokea hapa jukwaani kwa ajili ya kukidhi kiu ya maswali na ushauri kwa wateja wenu
Maana wenzenu NBC wako hoi kitandani na hawana hata habari juu ya yale yanayoandikwa kwenye mitandao juu ya benki yao
Hongereni sana kitengo cha mawasiliano kwa umma NMB kwa mrejesho huu mnautupatia, Hakika nyinyi ni wadau wa kweli katika maendeleo ya taifa hili
Natamani taasisi zote zikaiga mfano huu
HEKO NMB HEKO TANZANI
Hazina wameongezeka muda wa mkopo kwa wastaafu hadi miaka nane. Kwa nini mnachelewa kuongea na taasisi nyingine kama PSSSF na NSSF nao waongeze muda wa kukopesha hadi miaka nane kama walivyofanya Hazina kwa wastaafu wao.
 
mnatutumia sms kuhusu tozo za serikali bila kutwambia mtakata asilimia ngapi ya kila muhamala hamuoni hilo ni tatizo kwa wateja wenu
 
Nyie nmb nyie,mnakurupuka tu,ooh tunakusanya tozo za serikali kwenye akaunti yako.
Mkataba tumefunga Mimi na nyie,lini mlinitaarifu kuwa mtakusanya tozo toka akaunti yangu?
Hivi nchi hii hakuna wanasheria wa kuwaahitaki nyie nmb[emoji15][emoji15][emoji15]
 
NMB,hii siyo sawa kwa sisi wastasfu wenye mkopo..nilichukua mkopo wa Benki kwa mkataba wa kukatwa kila mwezi pensheni inapoingia.ajabu tarehe 18 mwezi huu nimeingiziwa fedha toka mahali ikskatwa ilhali nilikuwa safari nikiitegemea kwa nauli.

Benki NMB,tawi Kaitaba
Account 32608000725
 
NMB,hii siyo sawa kwa sisi wastasfu wenye mkopo..nilichukua mkopo wa Benki kwa mkataba wa kukatwa kila mwezi pensheni inapoingia.ajabu tarehe 18 mwezi huu nimeingiziwa fedha toka mahali ikskatwa ilhali nilikuwa safari nikiitegemea kwa nauli.

Benki NMB,tawi Kaitaba
Account 32608000725
Haya mambo kukatwa hela bila taarifa ni upumbavu na ujinga

Hata voda wanafanya hio michezo

Wapuuzi sana
 
Nyie NMB muna mambo ya ajabu Sana,mumetukata pesa kwenye account ni za kwenu? Wengine tumedipositi marejaesho munakakata tuu munavyojisikia ,na hatujui tozo zinahusika na nini?

Kama ni makato mbona tunakatwa pesa nyingi sana tukitoa pesa!
Mfano leo nimetoa sh 100,000/= kwenda M-PESA mumenikata zaidi ya sh 5,000/= STOP STOP STOP tozo!
 
Mimi nimeingiziwa 100000 juzi, Jana naangalia salio nakuta kuta 87000 kweli mnatukomesha aisee,wezi wakubwa nyie.
 
Ninapenda kutoa Pongezi kwa Benki namba moja nchini Tanzania, NMB.

Kwa huduma yenu ya Advance Salary.
Ni msaada mkubwa sana kwa Wafanyakazi wa nchi hii na wadau wa NMB kwa ujumla.

Asanteni sana Management na Washika dau wote wa
NMB Bank.
 
[emoji16]
JamiiForums2040959967.jpg
 
Kasoro za NMB Bank.
1. ATM ambazo hazipo kwenye tawi la Benki muda mwingi hazina pesa.

2. Kila tarehe za Mshahara ATM nyingi huwa hazifanyi kazi. Hata zilizopo katika matawi ya Benki. {wateja wanahisi wanalazimishwa kuchukua pesa zao kaunta ili wakatwe pesa nyingi za service charge}

3. Ni kawaida kukuta cashier wasio zidi wawili katika madirisha yote ya kuchukulia pesa ingwa madirisha ni mengi (hata kukiwa na msululu mrefu wa wateja hakuna hatua zinazochukuliwa, jambo ambali linawachosha wateja wengine wanaamua kuahirisha zoezi la kuchukua pesa)

4. Baadhi ya matawi ya benki hayana wahudumu wa kuwaelekeza wateja jinsi ya kutumia huduma mbali mbali za Kibenki mfano jinsi ya kutumia ATM, NMB App nk.

kwa wateja wenye ufamu mdogo.
Utakuta kuna walinzi tu nje na ndani ya Benki au Vituo vya ATM ambao hawasemi chochote ukuwauliza jambo lolote.

5. ATM nyingi hazitoi huduma ya kutoa pesa. Na zikitoa zinatoa kwa muda mchache na kuishiwa pesa.

5. NMB punguzeni Riba za mikopo ili kuvutia wakopaji.
 
NMB bana
Baada ya kuomba mkopo inachukua muda gani kuupata huo mkopo?
 
Back
Top Bottom