Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo prepaid haipokei pesa mkuu, ukitaka kudeposit unaenda tawini. NMB ni benki ya ajabu mnowakuu mambo vip,naombeni kujulishwa jinsi yakuweka pesa kwenye NMB PREPAID CARD kupitia airtel money ...maan account namba naiona ina namba na heruf
Naomba hyo namba ya customer careMimi Ni mteja wenu kwa miaka. sasa,na nimekuwa nikiwajulisha kuwa mnatakiwa kufanya marekebisho kwenye mfumo wenu wa namba ya simu huduma kwa wateja ,maana ukipiga simu na unashida ya haraka Ni vigumu kupata msaada,mfano juzi nilipoteza kadi yangu hivyo ikanibidi niwapigie ili kadi yangu ifungwe,Cha kushangaza nilikutana na matangazo mengi tu bila kupata kitufe Cha kuongea na mtoa huduma,hivi kwa uelewa wenu mtu makini anaweza piga simu kwenu ili asikilize matangazo?,ilinuchukua dakika 20 kuwapata ,ikiwa kadi yangu ingekuwa kwa mikono isiyo salama tayari nilikuwa nimeshaibiwa pesa zangu.
Mwaka Jana nilipiga simu nikawaambia,fanyeni kuweka namba ya kubofya ili kuongea na mtoa huduma? Nasio matangazo,,yaani iwe hivi bonyeza moja kuongea na mtoa huduma,na baada ya hapo ndo yafuate hayo ya kwenu.
Ninyi mna dhamana kubwa ya kutunza pesa zetu,sitegemei mtu apige simu kwenu theni akutane na blah blah ! Na kitu kingine watoa huduma hata ukiwabahatisha wanachelewa Sana kuunganishwa nao au kukuhudumia,badilikeni.
Mimi nilikuwa nimejipanga kuwashitaki ikiwa tu pesa zangu zingeondolewa kwenye account yangu kwa uzembe wenu.
Mwisho nakazia Tena,kwenye menu yenu ya huduma kwa wateja kwa njia ya simu wekeni kipengele Cha " kuongea na mtoa huduma bonyeza eidha sifuri,moja ,mbili nk.
NMB Tanzania
0800002002Naomba hyo namba ya customer care
Shukrani mkuu0800002002
Mimi nataka kumfungulia mwanangu account ila Hana cheti Cha kuzaliwa je inawezekana kufungua ?Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom