NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nmb nyie ni miyeyusho sana badilikeni huduma kwa wateja department is useless
 
wakuu mambo vip,naombeni kujulishwa jinsi yakuweka pesa kwenye NMB PREPAID CARD kupitia airtel money ...maan account namba naiona ina namba na heruf
 
Hivi imeshawahi kutokea hii Benki ya NMB au benki yoyote kuweza kujibu maswali ama manung'uniko ya wateja wake hapa JF? Mie sijawahi kuona, na huwa nafuatilia sana maana kero hizi zinazozungumziwa pia huwa nazipata, kwa hiyo nakuja humu kuona kama kuna majibu yeyote.

Ila naambulia patupu. Nilidhani uzi huu ulianzishwa na benki wenyewe ili waweze kuwahudumia wananchi kwa ukaribu na kutatua kero. Au ndivyo sivyo?
 
NMB mmenizulumu pesa yangu, nililinew mkopo deni likakatwa nikachukua changu na benki wakachukua Chao, lkn mkaendelea kukata kwenye mkopo wa Zaman badaye mmekuja kuanza kukata kwenye deni jipya na pesa ya makato ya mwanzo ambalo deni lake lililipwa, nilimfuata aliyeshughulikia mkopo wangu akaniambia hayo mambo hufanyika makao makuu hata yeye hajui chochote, nataka ifike miezi 5 kama hawajanilipa nawapeleka mahakamani wakanipe na riba kabisa
 
wakuu mambo vip,naombeni kujulishwa jinsi yakuweka pesa kwenye NMB PREPAID CARD kupitia airtel money ...maan account namba naiona ina namba na heruf
Hiyo prepaid haipokei pesa mkuu, ukitaka kudeposit unaenda tawini. NMB ni benki ya ajabu mno
 
Tunaziomba benki katika kusherekea miaka 60 ya uhuru wetu zikae chini na kuwezesha uanzishwaji wa ATM CENTER. Kwa maana ya kwamba sehemu ambao itakuwa na upatikanaji wa ATM za benki zote.

Mfano; ukishuka airport ya jiji la NAIROBI kwa wale mliobahatika kufika pale mtakuwa manaelewa nini najaribu kumanisha. Na hii inarahisisha upatikanaji wa huduma.

Kwa Tanzania sehemu kama kariakoo kwa mzunguko wa fedha uliopo pale na idadi ya watu sio ya kukosa ATM CENTER.
 
NMB naomba mtufanyie favour moja. Piga chini ATM zote hapa Azikiwe street opposite Benjamini Mkapa Tower. Yaani fungeni zote muziondoe maana zimebaki kama takataka tu tangu muue hili tawi. Kweli ATM zote mchecheto! Fungilia mbali huo uozo.
 
Mimi Ni mteja wenu kwa miaka. sasa,na nimekuwa nikiwajulisha kuwa mnatakiwa kufanya marekebisho kwenye mfumo wenu wa namba ya simu huduma kwa wateja ,maana ukipiga simu na unashida ya haraka Ni vigumu kupata msaada,mfano juzi nilipoteza kadi yangu hivyo ikanibidi niwapigie ili kadi yangu ifungwe,Cha kushangaza nilikutana na matangazo mengi tu bila kupata kitufe Cha kuongea na mtoa huduma,hivi kwa uelewa wenu mtu makini anaweza piga simu kwenu ili asikilize matangazo?,ilinuchukua dakika 20 kuwapata ,ikiwa kadi yangu ingekuwa kwa mikono isiyo salama tayari nilikuwa nimeshaibiwa pesa zangu.

Mwaka Jana nilipiga simu nikawaambia,fanyeni kuweka namba ya kubofya ili kuongea na mtoa huduma? Nasio matangazo,,yaani iwe hivi bonyeza moja kuongea na mtoa huduma,na baada ya hapo ndo yafuate hayo ya kwenu.

Ninyi mna dhamana kubwa ya kutunza pesa zetu,sitegemei mtu apige simu kwenu theni akutane na blah blah ! Na kitu kingine watoa huduma hata ukiwabahatisha wanachelewa Sana kuunganishwa nao au kukuhudumia,badilikeni.

Mimi nilikuwa nimejipanga kuwashitaki ikiwa tu pesa zangu zingeondolewa kwenye account yangu kwa uzembe wenu.

Mwisho nakazia Tena,kwenye menu yenu ya huduma kwa wateja kwa njia ya simu wekeni kipengele Cha " kuongea na mtoa huduma bonyeza eidha sifuri,moja ,mbili nk.

NMB Tanzania
 
Naomba hyo namba ya customer care
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Mimi nataka kumfungulia mwanangu account ila Hana cheti Cha kuzaliwa je inawezekana kufungua ?
 
Hii app yenu mbona sielewi?
Screenshot_20211230-091305.jpg
 
NMB naomba ufafanuzi wa wateja wenu ambao walichukua mkopo wa kilimo(pembejeo) wakashindwa kulipa kutokana na sababu mbalimbali ambapo riba yake inapaa kwa kasi ya supersonic mfano mwenye deni la M4 kwa sasa anandaiwa M7. kwanii kwa mikopo ya kilimo iwe hivyo wakati mikopo ya biashara riba haipandi kiasi hicho? Je mna mpango gani wa kuwerejeshe wakulima ambao tayari wamelipa riba UMIZA hiyo? mfano mteja wa milioni 3 aliyelipa M6?
 
Kwa nini NMB hawatoi Mikopo kwa Wastaafu wa NSSF, ambao wanaweza kutumia pensheni yao ya kila Mwezi,inaweza kutumika kulipa deni.Lakini Wastaafu wanalipwa pensheni kupitia Hazina na PSSSF wanakopeshwa na wanaruhusiwa kukatwa kwa miaka 5.

Ushauri
1.Ni vema NMB ikatoa mikopo kwa Wastaafu wa NSSF ili na wao wamalizie ujenzi wa vibanda vyao
2.NMB na NSSF kaeni chini muyajenge
 
Hongereni sana NMB kwa huduma yenu nzuri ya kututunzia pesa zetu.

Natoa pongezi pia kwa huduma yenu nzuri ya mikopo kwa wafanyakazi na hasa huduma ya Afvanve Salary.

Mosi
tatizo kubwa ninaloliona binafsi ni kutopokewa simu kwa wakati za huduma kwa wateja.
Pesa ndio kila kitu katika maisha ya sasa.
Mteja akipata tatizo na kuwapigia simu ni lazima asikilizwe kwa haraka sana.
Kachelewa sana isizidi dakika kuweza kujibiwa ili aeleze tatizo lake.
Wateja hatutaki matangazo yenu simu iite mteja aseme shida yake basi.
Na sio unapiga simu unaanza kuulizwa maswali na viroboti

(eti ukitaka huduma za feza za kigeni bonyeza mbili)

Pili
Siku za mishahara ATM huwa hazifanyi kazi yaani zinakosa Network.
Inawezekana hii ni mbinu yenu ya kutaka wateja waende kuchukua feza zao ndani ya Benki ili kuongeza faida ya benki inayotokana na makato makubwa ya huduma hiyo.
Basi hata humo ndani kwenye Benki kuweko na Cashiers wa kutosha.
Unakuta siku za mishahara kuna mtoa huduma mmoja na hawazidi wawili. Foleni ndefu mteja anasimama hadi anataka kudondoka.
Na watoa huduma hawatulii dirishani mara watoke kidogo warudi baada ya muda na kurudiarudia.
Jambo hili ni kama mnatoa adhabu kwa wajeja wenu.
Watu wengine ni wagonjwa au Wazee au tutakuta mama kabeba mtoto.
Hata mimi mzima nakerwa sana na huo usumbufu.

Jirekebisheni.
 
Back
Top Bottom