Ndugu wana JamiiForums,
Tunachulia kwa uzito
tuhuma zilizotolewa na kuelekezwa kwa baadhi ya wafanyakazi wetu kwani zina lengo zuri la kuifanya benki kuendelea kuwa namba moja kwenye kusimamia maadili.
Ndugu wana jukwaa, NMB tunajipambanua kwa kusimamia maadili mojawapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wetu pamoja na kuwa na sera kali dhidi ya rushwa na upendeleo wa aina yoyote katika kutoa ajira.
Wafanyakazi wasio waadilifu na wanaoendesha mambo yaliyo kinyume cha utaratibu na sera za benki, hawavumiliki na hatua kali zitachukiliwa kwa atakayedhibitika kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za nchi juu ya rushwa.
NMB pia tunapenda kuwahakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba tutaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
" HAKUVUMILIKA AISEE!"