NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Juzi akaunti yangu ya NMB nilikuwa na tshs 72,000/=kwenda kutoa nakuta tshs54,000/=tu naambiwa ni makato ya kodi,bado sijaelewa hiyo kodi ni %? Kiasi kwamba 70,000/= kodi iwe tsh16,000/=?
Naomba majibu tafadhali.

Hee sss mim mwenye 4m+ si watakua wamekata 400000[emoji15][emoji15]
Nhoj nkaangalie leo
 
Elezeeni kuhusu mwalimu spesho.

Alafu kuna haja gani kurusha habari ndogo inayohusu kundi dogo ktk vyombo vya habari.Mbona mengine huwa mnawajulisha kwa sms tu?
Au vipeperushi si vinatosha?
NMB Tanzania
 
Wakala wa nmb mtaani kila ikifika usiku mtandao unazingua ni suala la mashine yake au ni Hadi huko makao makuu mtandao unazingua
 
Juzi akaunti yangu ya NMB nilikuwa na tshs 72,000/=kwenda kutoa nakuta tshs54,000/=tu naambiwa ni makato ya kodi,bado sijaelewa hiyo kodi ni %? Kiasi kwamba 70,000/= kodi iwe tsh16,000/=?
Naomba majibu tafadhali.
Acha kbs Mimi CRDB nilitoa pesa nikakuta 22,000 imekatwa.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
BANK YA NMB WILAYA YA NEWALA HAKUNA VYOO VYA WATEJA.
MIMI NI MTEJA NIMEULIZA KWA ASKARI / MENEJA HAPA NMB WAMENIJIBU HAKUNA VYOO VYA WATEJA. WATU TUNAKUJA KUPATA HUDUMA KUWEKA NA KUTOA WAKATI MWINGINE FOLENI TUNAJISAIDIA WAPI?
WAHUSIKA LIFUATILIENI HILO.
 
Mbona huduma za nmb app hazipatikan Leo na hamjatoa taarifa? Au nanyi mmeamua kuwa Kama tanesco na dawasa wanaositisha huduma Kwa wateja bila taarifa?
 
Nahitaji mkopo kiasi Cha tshs 40mil,dhamana ni nyumba iko DSM wilaya ya ilala kata ya kitunda,utaratibu wa bank yenu NMB uko vp?
 
Benki yenu haibadiliki ipo ipo tu kwanini msiwe wabunifu ? Watu wanatafuta hela kwa shida kwenda kutunza hela zao na kuchukua pia wapate shida?

You have to be creatives and avoid conservatism.
Sijaona kama wamejibu hapa ni kwamba kuna siku kadi yangu imepata shida kuchukua hela dirishani niliingia saa tano asubuhi nilitoka saa nane mchana,remind you nilikua nachukua hela niendelee na mihangaiko kwaio hata kunywa chai si kunywa, unasimama hadi unapepesuka, watu foleni ya mita karibu 20 wanahudumiwa na teller mmoja. Badilikeni NMB. recruit vijana wapo wengi sana hawana ajira kuliko kila mwaka kuingiza mifaida yenye malalamiko.
 
Nikiwa mdau wa benki hii natoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa benki Dr. Edwin Mhede - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi na Prof. Ruth Zaipuna (Mrs)- Mkurugenzi Mtendaji kwa kitendo cha kuyapokea maoni na ushauri na hatimaye kufanikisha kumwadabisha Lilian Komwihangiro (Advocate) aliyekuwa katibu wa benki na mkuu wa idara ya sheria.

Sina budi kuwapa pongezi za dhati kwani kitendo cha kusimama katika ukweli na haki bila ya kuficha maovu yake kinazidi kuiweka taasisi katika hali nzuri kuelekea kwenye mafanikio zaidi.

Hivyo basi msiache kufanyia kazi maoni na ushauri mwingine mtakaoupata ili kuendelea kuboresha benki hii imara hapa nchini.

Nashauri kwa uwazi na ukweli kwa kuwa hiyo nafasi ni nyeti na kiungo kati ya wadau, uongozi tendaji na uongozi wa bodi, nafasi hiyo itangazwe ndani ya benki na nje ili apatikane mtu POTENTIAL ambaye ataweza kusimamia maslahi ya kila upande, kwani kitendo cha kuendelea kuiacha wazi kinaweza kudhorotesha na kupunguza ufanisi wa benki kwa ujumla na mapana yake.

Nawasilisha.
 
Hongera tena kwa Uongozi wa Taasisi hii kwa kufanya makuu, sasa hiyo nafasi moja waigawa kutengeneza nafasi mbili yaani Mkuu wa Idara ya Sheria & Katibu wa Benki na hizo fursa zimetangazwa ndani ya Taasisi wasiwasi wangu nikiwa mdau mkubwa ni:

1. Wajaribu kuficha ili umma na wateja wasitambue kuwa mtu yule she is no longer.
2. Hao mabinti wanaokaimu hizo nafasi ni zao la uozo toka kwa mtu yule.
3. Hizo nafasi yamkini zinahitaji mtu/watu toka nje ili waje na vitu vipya wala sio kuendeleza uozo uliopo.
4. Kwa mantiki ya uwazi na ukweli zitangazwe nje na kampuni kama Delloite na pia Ernest & Young wapewe tenda ya kutafuta right candidates ili hao wanaokaimu nao washindanishwe haswa.
5. Hili sio geni kwani viongozi wengi top management wamepatikana hivyo.

Namaliza kwa kuwashukuru na kupokea maoni chanya hivyo hivyo kuwa wasikivu kwa maslahi mapana ya taasisi kwa ujumla wake.

Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
NA KAZI IENDELEE.
 
Nimehamisha hela kutoka Nmb mobile kwenda Airtel Money na sijazipata toka juzi
 
Nikiwa mdau wa benki hii natoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa benki Dr. Edwin Mhede - Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi na Prof. Ruth Zaipuna (Mrs)- Mkurugenzi Mtendaji kwa kitendo cha kuyapokea maoni na ushauri na hatimaye kufanikisha kumwadabisha Lilian Komwihangiro (Advocate) aliyekuwa katibu wa benki na mkuu wa idara ya sheria.

Sina budi kuwapa pongezi za dhati kwani kitendo cha kusimama katika ukweli na haki bila ya kuficha maovu yake kinazidi kuiweka taasisi katika hali nzuri kuelekea kwenye mafanikio zaidi.

Hivyo basi msiache kufanyia kazi maoni na ushauri mwingine mtakaoupata ili kuendelea kuboresha benki hii imara hapa nchini.

Nashauri kwa uwazi na ukweli kwa kuwa hiyo nafasi ni nyeti na kiungo kati ya wadau, uongozi tendaji na uongozi wa bodi, nafasi hiyo itangazwe ndani ya benki na nje ili apatikane mtu POTENTIAL ambaye ataweza kusimamia maslahi ya kila upande, kwani kitendo cha kuendelea kuiacha wazi kinaweza kudhorotesha na kupunguza ufanisi wa benki kwa ujumla na mapana yake.

Nawasilisha.
Mkuu unaweza kutoa dokezo ya uovu alioufanya yule Bi Mkubwa,maana nilisikia kung'oka kwake ni kwa kustaafu,kumbe behind the scene kuna mazito ,toa dokezo tafadhali...
 
Mkuu unaweza kutoa dokezo ya uovu alioufanya yule Bi Mkubwa,maana nilisikia kung'oka kwake ni kwa kustaafu,kumbe behind the scene kuna mazito ,toa dokezo tafadhali...
Balozi (Ambassador_🙂

Hakuna kitu kibaya kama kuficha ukweli! inakuwaje mtu asimamishwe kazi! maana yake kuna tuhuma bila ya kificho! pili umri wa kustaafu upo wazi huenda kwa hiari ni 55 au lazima ni 60 sasa yeye alitimiza ipi kati ya hiyo!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunachulia kwa uzito tuhuma zilizotolewa na kuelekezwa kwa baadhi ya wafanyakazi wetu kwani zina lengo zuri la kuifanya benki kuendelea kuwa namba moja kwenye kusimamia maadili.

Ndugu wana jukwaa, NMB tunajipambanua kwa kusimamia maadili mojawapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wetu pamoja na kuwa na sera kali dhidi ya rushwa na upendeleo wa aina yoyote katika kutoa ajira.

Wafanyakazi wasio waadilifu na wanaoendesha mambo yaliyo kinyume cha utaratibu na sera za benki, hawavumiliki na hatua kali zitachukiliwa kwa atakayedhibitika kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za nchi juu ya rushwa.

NMB pia tunapenda kuwahakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba tutaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

" HAKUVUMILIKA AISEE!"
 
@Msemakweli TZ mwaga maneno kama jina lako watu waujue uozo,pengine inaweza kuchochea kufichuliwa kwa maovu mengi zaidi kwenye Taasisi husika..
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunachulia kwa uzito tuhuma zilizotolewa na kuelekezwa kwa baadhi ya wafanyakazi wetu kwani zina lengo zuri la kuifanya benki kuendelea kuwa namba moja kwenye kusimamia maadili.

Ndugu wana jukwaa, NMB tunajipambanua kwa kusimamia maadili mojawapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wetu pamoja na kuwa na sera kali dhidi ya rushwa na upendeleo wa aina yoyote katika kutoa ajira.

Wafanyakazi wasio waadilifu na wanaoendesha mambo yaliyo kinyume cha utaratibu na sera za benki, hawavumiliki na hatua kali zitachukiliwa kwa atakayedhibitika kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za nchi juu ya rushwa.

NMB pia tunapenda kuwahakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba tutaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

" HAKUVUMILIKA AISEE!"
Alaf na ile position si ni contract based,sio kwamba na mkataba wake uliisha?
 
Yule mwanamama alikuwa ndio defacto CEO

1. Aliweza kuweka ndugu zake katika nafasi nzito nzito tuu na hata alidiriki kutaka mdogo wake wa kuzaliwa asiye na vyeti kuwa CEO kwa kumfitini ndugu mmoja aliyekuwa anaandaliwa na watasha kuongoza shirika.
2. Kampuni zote zilizokuwa na mikataba na benki huenda zilikuwa zake 100% au aliingia nazo mikataba fichi.
3. Alikuwa na Kuogofya na Uongozi wa Bodi hata na wafanayakazi wadogo tuu ikiwemo walinzi na hata wafagizi.
4. Hata huyo mwanamama mwenzake Mrs. Prof Zaipuna alikuwa anamwogopa mno.
5. Kuhusu kazi yake yeye alikuwa na mkataba wa kudumu, ila kwa sasa nafasi imevunjwa vunjwa mara dufu na kutengeneza (i) Head of Legal and (ii) Company Secretary.

Je kama Benki hii huwa inatoa taarifa za Financial Position kuwa ni za ukweli kwanini wanadanganya umma kuwa huyu mwanamama alishaafu wakati alifukuzwa kwa Aibu Tele!

Je tutawaamini kwa lipi hawa waungwana!

Nakushukuru mno Ambasador kwa kufuatilia na kutaka kujua ukweli na kadri nitakapozidi kupata muda niyakuwa nauweka ukweli hapa hapa kama wao wana majibu mengine nao waje watoe ufafanuzi wa kina!
 
Back
Top Bottom