NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania ni kwanini mmeacha kutuma electronic bank statement za kila mwezi kwenye email.

Kuna uhusiano wowote na huu utaratibu mpya wa kukata tsh 5300 bila maelezo yoyote?
Account ikikuwa 70000 baada ya siku mbili bila kutoa pesa ikabaki 23000 sijui mpaka leo hiyo pesa wameipeleka hakika NMB Mungu anawaona
 
Kindly....naomba kujua je inachukua muda gani ..KUTUMIWA ID password ya NMB wakala kutoka Makao makuu baada ya taratibu zote kukamilika katika Branch....maana ni karibu mwezi sasa hatujatumiwa !
 
Wakuu msaada tafadhali kwa wahusika kuna shida gani upande wa salary advance?Huduma inanigomea changamoto ni nini!!
 
Jambo hili limeleta kero kubwa.
Mtu unataka kununua salio la simu au kununua umeme lakini unatakiwa kuweka salio kwanza.
Una pesa kwenye akaunti lakini unalazimishwa utembee kwenda dukani kununua vocha y kukwangua ya sh.500/=.
Huku ni kuturejesha kwenye analogi.
Ndio! NMB wakishirikiana na makampuni ya simu wangeweka utaratibu wa kuondoa hii kero kwa kuingiza gharama hizi kwenye salio LA mteja (I mean hiyo tozo ya sh. 100 ikatwe kwenye salio .je ikiwa nitahitaji huduma hii nikiwa eneo ambalo halina duka LA vocha itakuwaje?Kweli jamani?
 
BANK YA NMB WILAYA YA NEWALA HAKUNA VYOO VYA WATEJA.
MIMI NI MTEJA NIMEULIZA KWA ASKARI / MENEJA HAPA NMB WAMENIJIBU HAKUNA VYOO VYA WATEJA. WATU TUNAKUJA KUPATA HUDUMA KUWEKA NA KUTOA WAKATI MWINGINE FOLENI TUNAJISAIDIA WAPI?
WAHUSIKA LIFUATILIENI HILO.
Hiyo ni siri ya benki, vyoo vipo ila ili wateja waruhusiwe kuingia huko vyooni ni lazima waongeze askari badala ya kuwa wa 2 lazima wawe wa 3, unadhani benki iko tayari kuongeza hizo gharama? Benki ni wachumi sana, je ulishawahi kuona mtumishi wa benki anaenda kununua mahitaji ya benki? Mfano karatasi, peni, toilet paper, wino nk. Je ulishawahi kuona afsa ugavi wa benki hapo ulipo?
 
Leo acha na mimi niweke kisa changu.
NMB mkononi app ni upigaji kama upigaji mwingine tu.!
Poor customer service halafu wanaboa kinoma.
Iko hivi;
Mnamo miezi kadhaa iliyopita nikiwa kama mtumiaji wa app yao ya NMB mkononi ambayo mara nyingi naitumia kununua umeme na wakati mwingine salio sasa siku hiyo kama kawaida nikaingia kununua muda wa hewani wa tsh kadhaa sasa baada ya kumaliza kununua na kuconfirm kama ninavyofanya siku zote cha ajabu sikupata salio wala sms ya kuonyesha nimefanikiwa kununua muda wa hewani ingawa nikiangalia salio kwenye account inaonyesha pesa imekatwa!
Nikaona isiwe tabu nikarudia mara ya pili kimya, mpaka nilirudia mara tano hapo nikiangalia salio kwenye account pesa imekatwa mara tano lakini sipati vocha wala sms ikabidi nilale mpaka kesho yake lakini bado sikupata vocha ikabidi niwapigie mtandao wa simu wakaangalia wakasema salio halijaingia kwenye simu yangu hivyo itakuwa ni ishu ya watu wa bank!
Nikawapigia NMB huduma kwa wateja ambapo waliangalia kwenye system zao na kukiri kwamba kweli kulikuwa na shida kwenye system zao hivyo pesa yangu yote itarudishwa kwenye account yangu ndani ya 24hrs lakini cha ajabu suala langu limechukua miezi zaidi ya mitatu ambapo kila baada ya siku kadhaa huwa nawapigia lakini majibu ni yale yale kwamba wanashughulikia watanirudishia pesa yangu soon.
Sikuridhika nikaamua kuibuka kwenye tawi la bank husika ambapo pia walicheck na kukiri kwamba kulikuwa na shida hivyo wakanipa form maalum nijaze nikaijaza wakasema wanatuma makao makuu then pesa itarudishwa lakini mpaka leo ni miezi kadhaa sijawahi kurudishiwa hiyo pesa kabisa na nikipiga customer service majibu yao ni hayo hayo tena sometimes huwa ni wakali wanaona kama nawasumbua kila siku!
Sasa najiuliza swali hili: inawezekana vipi mimi kama mteja nikatwe pesa yangu kwenye account kwa makosa ya mtandao wao halafu mpaka leo hii miezi wamekaa na hela yangu ambayo haina majibu sahihi mpaka leo?
Je kwa hali hii kama pesa ndogo tu isiyofika hala laki imekuwa ngumu kuirudisha je siku mteja afanye mwamala hata wa laki tano halafu wamfanyie kamchezo haka itakuwaje?
Ukweli niliipenda sana NMB ila kwa huu mchezo naelekea kuifunga account yangu na kuhamia bank nyingine pia ntafanya hivyo kwa account za wanangu na watu wangu wa karibu ambao nawamudu!
Endeleeni na upigaji wenu hamjui watu tunapata pesa kwa taabu hasa mimi muuza majeneza ambaye kipato changu ni kidogo!
 
NMB Handeni Tanga kuna kadada flani keusi nywele hakaja suka kamepaka dawa kanaringa sana ukifika akuhudumie unatakiwa kila kitu uwe unakielewa ukimuuliza atakupa jibu baya na hana time na wewe kiufupi anadharau sana kila nikifika handeni nikihitaji huduma ya ndani naishiwa nguvu kabisa nikimfikiria yeye nabaki kuomba Mungu nisogee sogee atleast Korogwe ila kwa handen bado mna kazi kubwa sana ya kufanya
 
Hello...
Kwa yeyote mwenye ufahamu, je, ninaweza kuunga akaunti zaidi ya moja kwenye application ya nmb mkononi?
Msaada tafadhali.
 
Habari zenu wapendwa?

Naomba kuuliza kuhusu matumizi ya App ya NMB Tanzania yanakuwaje kwa sababu kila ninapojaribu kuuliza kuangalia salio langu kupitia NMB App nakuta salio limepungua kwenye Account yangu.

Tena makato sio ya kitoto ni makubwa sana najiuliza hii ni kwangu tu au kwa watumiaji wote wa NMB App. Msaada Tafadhali.

Pia naomba kufahamu kwa yeyote anaefahamu kuhusu Mambo haya,ni benki gani cheep zaidi katika swala zima la makato lipokuja swala la kutoa pesa au mikopo na riba zao? Msaada Tafadhali.
 
Back
Top Bottom