Unayo matatizo kichwani.
Benki na huyo mama walishamalizana na huyo mama kuhusu mkopo. Benki hawajatoa hiyo hati kumrudishia mwenyewe mwenye hati (mama).
Mama anakwenda Benki kuulizia hati yake, anaambiwa arudi nyumbani atapigiwa simu; lakini simu hata moja hapoki toka benki, miaka mitano sasa!
Kwa hiyo hati iko benki, na kuna wachangiaji wengine humu wameeleza kuwa inawezekana matapeli wa benki wameitumia kuchukua mkopo, ndiyo maana wanashindwa kuirudisha kwa mwenyewe, badala yake wanatumia mbinu za kumzungusha, miaka mitano mfululizo.
Kuna wachangiaji wengi tu wameshauri huyo mama alipeleke swala lake mahakamani; na adai fidia ya usumbufu wa muda mrefu. Wakili apatikane wa kumsaidia huyo mama. Gharama za huyo wakili zitatokana na fidia itakayodaiwa.
Wewe hapo ukaingia kwa gia nyingine kabisa, kwamba mama adai hati imepotea, kwa hiyo aende kuomba nyingine. Mwanzo nilidhani ni wazo lakutaka kuchekesha watu tu, kumbe sivyo. Nikakueleza huko nako kuna 'process' atakazotakiwa kuzifuata huyo mama, kama kwenda kutoa ripoti polisi kuwa kapotelewa na Hati (huku ikiwa ni uongo). Hili pekee linakufanya wewe uonekane kuwa kichaa, tena tapeli lisilokuwa na akili.
Sihangaiki tena na wewe.