NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

USIRI KATIKA MANUNUZI (ZABUNI) MAANA YAKE NI NINI HAPA TANZANIA?
1. Mchakato haukuwa huru, haki na wenye nia njema.
2. Sheria, kanuni na taratibu zilikiukwa ili kufikia lengo.
3. Kuna harufu ya upigaji wa kiwango cha kutisha.
4. Wahusika ni vigogo ndani ya serikali wakishirikiana na wageni.
5. Mwisho wa siku itakuwa ni skendo yenye kutesa watu na taifa.

USHAURI WANGU.
Katika zama hizi, hakuna siri itakayobakia kuwa siri siku zote, kadri jambo lenye maslahi kwa umma linapofanywa kuwa siri ndivyo huzaa kashfa, uharibifu na uzushi mwingi kwenye jamii. Tusiwalaumu wanasiasa wa upinzani wakianza kulitolea ufafanuzi (kulikosoa) uuzwaji huo kwa kuwa tumewapa rasmi jukwaa la kulisemea. Binadamu ni kiumbe anayependa kusikia na kusikilkzishwa mambo ya sirini. Wahusika mtoke sasa hadharani sasa kuweka wazi kila kitu (hata kama ni kibaya au kichungu) ili muwe huru.
 
Kwa hyo tuseme TANZANIA [emoji1241] KUNA PESA NYINGI TU DU HIVYO KUMBE MAAANA WATU WANACHOTA MAPESA NA BADO YAPO
 
Huenda mnunuzi ni mtumishi wa umma chini ya joka la kijañi
 
Kama kuna mtu amenunua mradi kwa bei kubwa kiasi hicho tena ukiwa haujakamilika Ina maana wazo la uwekezaji na mpango huo ulikuwa ni mzuri na wenye faida baadae.

Hili ni tofauti na wale wakurupukaji waliouponda..... Hongera corporate man, Dr Dau.
 
Hatari thana...
AIP01SBV0DQ Imethibitishwa.Umepokea Tsh50.00 kutoka 219777 - M-PESA FAIDA tarehe 25/9/23 saa 12:39 AM Salio lako ni M-Pesa ni Tsh70.30.
Hongera sana mkuu mimi wananitumiaga Sh 16. Tena walivyokuwa wenu wanatuma saa 6 usiku
AIN5ARMXM7J Confirmed.You have received Tsh16.00 from 219777 - M-PESA FAIDA on 23/9/23 at 2:47 AM New M-Pesa balance is Tsh63,848.75.
 
Akili inaniambia aliyenunua ni mwarabu....ndio maana mnunuzi kafichwa maana angesemwa ingezidisha maneno mtaani....ndio maana mwarabu anatetewa sana maana kanunua vingi...tuendelee mtori nyama zinaanza kuonekana...SASA KILICHOBAKI KILICHOPO MBELE NI BUNGE KUPITISHA SHERIA YA ARDHI ILI WAMILIKI KABISA IWE YAO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…