Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
Hizi ni baadhi ya nukuu za Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti madini:
-Kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu anaposikia ripoti kama hii lazima apate uchungu
-Nafahamu wapo watu walitaka kuhatarisha maisha yenu, lakini walishindwa kwa sababu ya ulinzi imara
-Tanzania tuna karibu madini yote, unaweza ukayataja mpaka ukasahau.
-Watanzania tuna mali nyingi lakini tunazichezea mpaka shetani anatucheka huko aliko
-Tanzania siyo siri wapo watu wanakufa kwa kukosa madawa, wapo wakulima wanakosa hata pembejeo wakati mali tunazo.
-Inashangaza sana kampuni ya madini inafanyakazi nchini kunyume na sheria tena biashara ya matrilioni ya fedha.
-Ukiwa na mchungaji wako anasema ng’ombe wanatoa lita 1 tu kwa siku ukienda kuhakikisha kama ni ukweli, ni vibaya?
-Sisi viongozi tujiulize ni mara ngapi tunawadhalilisha wafanyabiashara wadogo wa Kitanzania wakiwa hawajasajiliwa?
-Nani atakayepewa ripoti kama hii akacelebrate? Wakati watoto wa maskini wanakufa.
-Siwezi kusimama pale mbele halafu naona haya yanafanyika nikae kimya, siwezi, nitaulizwa siku moja na Mungu wangu.
-Kuna mpiga kelele mmoja, tuli trac simu yake tukaona anatuma meseji anasema naomba data hii, naomba data hii.
-Hizi fedha zikienda hospitalini hawatatibiwa CCM tu hata CHADEMA watatibiwa.
-Kwenye ripoti ya kwanza, Kafumu amehangaika kutafuta data ili afanye mabadiliko ni ujinga mtupu
-Dkt. Kafumu alienda kumbembeleza Prof. Mruma ili afanye forgery ya Ripoti ya Kamati ya Kwanza
-Mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati hii nayapokea na nimeyakubali kwa asilimia 100
-Kuna Dkt mwingine wa Muhimbili tulimkamata Dodoma anataka kuishawishi kamati ibadili ripoti, tukamrudisha akatibu.
-Ukiwa msoma sio unakuwa mzalendo, unaweza ukasoma ukawa hata Profesa lakini usiwe mzalendo
-Hii kampuni inayoitwa Acacia waitwe kwanza walipe pesa zetu,Wakikubali na kutubu ndipo wafanyiwe registration
-Wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti hii vyombo vya dola viwahoji na kubaini ukweli juu ya jambo hili
-Kazi hii ni ngumu, ni ngumu kweli kweli, lakini kama Mungu amenipa kuifanya i will do it
-Sawa sisi viongozi hawaturuhusu kuingia migodini, hata viongozi wa dini basi waruhusiwe kwenda kuombea hayo madini
-Naomba Sheria ya gesi ipitiwe, hata tukichelewa ni sawa lakini tuwe na sheria nzuri
-Hii nchi tumelogwa na nani? Basi viongozi wa dini tuombeeni mapepo yatoke
-Mtu unakuta ni Mbunge na Jimbo lake ni masikini lakini anakuja kutetea huu ujinga
-Spika nikakuletea hii mizigo, kwa wale watakaokuwa wanaropoka unaenda vizuri, ili wakiropoka nje mimi ntadili nao
-Spika, kwa wale watakaokuwa wanaropoka ropoka, watoe nje. Na wakiropokea nje i will deal with them, Ila siwatishi
-Prof. Oroso umetimiza wajibu wako hapa duniani, Mungu atakubariki sana.