Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Nimesema hajitambui badala ya kutumia lile neno baya alilotumia dhidi ya baadhi ya mawazori kwa kuzembea kuchukua hatua. Ni waziri gani asiyemjua Rais na utendaji wake usiotabirika na udhalilishaji dhidi ya wayeule wake?
Naanza na waziri Mwakyembe. Huyu alitoa tamko dhidi ya wasio na vyeti vya ndoa, na akawa mstari wa mbele kusimamia hilo pamoja na kutoa muda maalum wa utekelezaji (mtanisahihisha kama ni vyeti vya ndoa au kuzaliwa). Tulichoshuhudia ni Rais kutengua mamlaka ya waziri wake. Unadhani ni ujumbe gani ulipelekwa kwa wateule wake?
Ishu ya Nape nayo inachanganya. Nape aliporwa uwaziri kisa aliunda tume ya kuchunguza tukio la uvamizi wa kituo cha clouds tv. Kosa la Nape ni lipi? Kwani hakuchukua maamuzi ambayo yalitenguliwa na Rais?
Ishu ya juzi Tanga kusema kuna mawaziri WAPUMBAVU wasiochukua maamuzi kwa wakati. Mwisho tunamuona waziri wa viwanda akiingia kwenye sintofaham na kubakia kuweweseka dhidi ya matamko ya Rais.
Akiwa Morogoro Rais alisimama kusalimiana na wananchi. Ndani ya hotuba yake fupi akagusia viwanda vilivyobinafsishwa na waliopewa, mmoja wapo akiwa ni mbunge wa Moro. Akamtaja na kumpa onyo mbele ya watu wa jimbo lake, kwamba atamnyang'anya hivyo viwanda kisa kashindwa kuendeleza.
Watu wanataka waziri/mawaziri wafanye nini au kuchukua hatua zipi wakati Rais ndiye mwenye kauli ya mwisho? Tena kauli za hadhara na za kufedhehesha. Rais aliwapa mamlaka mawaziri. Sasa asiwape msongo wa mawazo kushindwa kujua ni hatua zipi wachukue ns zipi waache. Asipende tu kuona yale anayotaka yeye yatekelezwe au yaachwe kisa tu ana maslahi nayo.