Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)
Uzi huu ni spesho kwa kuweka nukuu za mh rais magufuli
(1)twafaaaaa
(2)katerero
(3)nitawafanya matajiri waishi kama mashetani
(4)makonda piga kazi
(5) fomu nilichukua mwenyewe sipangiwi na mtu
(6)msaliti anayewasaliti wanajeshi wenzake wakiwa vitani hatakiwi kuishi
(7)mpaka ifikapo mwaka 2020 kutakuwa hakuna upinzani tanzania
(8)upinzani ni kama nyoka tumemponda nyoka kichwa
(9)
(10)jazia nukuu nyingine

11. ka-ta
12. hawa ni wanaume
13. mayala kwa kikwetu ni njaa
14. wanafunzi wote wanatoka darasani wanakwenda kunyonyesha
 
Naweza nikaamua, hata ndani ya siku mbili nikabadilisha fedha ili wale walioficha kwenye magodoro zikaozee humo humo.
 
1. Nyongeza ya mishahara itakuwa tayari mwezi ujao, kwa sasa tunahakiki watumishi hewa
2. sipo tayari kusomesha wake za watu
 
Zaaneni tu watoto nitasomesha bureeee.

ccm haukuleta tetemeko.
 
Maagizo kwa Supika wa Bunge:

“Kwa wale watakaokuwa wanaropoka ropoka unaenda vizuri, tumia hiyo technique (mbinu) ya kuwafanya wasiropokee bungeni waropokee nje na kule ‘tutadeal’ (tutashughulika) nao vizuri.

“Kwa sababu wanapokuwa ndani wanaweza kutukana chochote. Sasa immunity (kinga) yao wanaoitumia vibaya kainyooshe wewe. Ili wawe wanatoka kule bungeni ukishamfukuza hata mwezi mzima, atakuja kuropokea huku na mimi nakueleza, ‘I will deal with them (nitawashughulikia).."
 
hahahaaaaaaa! mbona rahaa nimeongeza siku zangu za kuishi kwakweli daah
 
Wakikusimamisha na mazao yako wakakuomba tozo waambie na nyie kichwa kama tozo

Tena nasema huu ndio muda wa wakulima kufaidikia kisado kimoja cha mahindi kwa ng`ombe watatu.
 
Sisi kwetu mwanamke huwa hatumsogezi watasema linakutawala (jangwani)
 
*NUKUU ZA MWENYEKITI WA CCM NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO CHA UWT TAIFA*

Desemba 08, 2017.
Dodoma.

1. " Tunataka kuwa na wanachama na viongozi waliopatikana kwa halali, hii nazungumza kwa Chama chote iwe wazazi, UWT ama vijana " - JPM


2. "Kama tumeamua kupingana na rushwa kwenye serikali Lazima tupingane na Rushwa na kwenye chama".- JPM


3. "Mtakavyo kuwa mnachagua leo msiangalie amekupa kiasi gani, amekulipia hoteli kiasi gani, chagueni kiongozi anaye amini kanuni na katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)". JPM

4. "Nataka mchague kiongozi atakaye waweka pamoja wakina mama" JPM

5. "Nasema kwa dhati nawapenda sana wakina mama, naomba mnisaidie yule mtakaye mchagua awe kila siku mtetezi wa wakina mama" JPM

6. "Atambue kiongozi siyo mfalme kiongozi ni kuwatumikia unaowaongoza"JPM

7. "Kiongozi wa UWT ngazi ya taifa siyo jukumu dogo ni jukumu kubwa, jumuia hii ni muhimu sana kwa Chama chetu cha Mapinduzi" JPM

8. "Naomba Ndugu zangu mchague kwa umakini mkubwa siyo kwa ukanda, udini, ukabila na Kamwe msichague mtoa rushwa tukumbuke ahadi namba 3 ya mwanaCCM" JPM

9. "Chama chetu kimefanya mageuzi makubwa na tumelenga kukifanya kuwa chama cha wanachama hivyo UWT lazima iwe ya wanawake wote siyo ya mtu mmoja " JPM

10. "Benki ya wanawake haifanyi vizuri Tangu ianzishwe utendaji kazi wake hairidhishi" JPM

11." Na wakopaji wengi pale ni wanaume na inariba kubwa kweli kwa wanawake". JPM

12. "Tunaipitia vizuri ili benki ya wanawake iwe kwa uhalisia kimbilio la wanawake hasa wale walio pembezoni" JPM

13. "Niwaombe uongozi huu mpya mnaouchagua mkafanye mageuzi kwenye benki ile ya wanawake maana inawanyonya wanawake".JPM

14. "Mimi ninadeni kubwa la kuwatumikia ila ninyi mnadeni kubwa zaidi leo la kuchagua viongozi wanaoweza kuenda na muelekeo wangu" JPM

Imetolewa na:

Idara ya Itikadi na Uenezi
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
404dee2ba72023b2e61a3ed7b676acc4.jpg
 
Back
Top Bottom