Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)
*JPM AFANYA MAKUBWA KWA MIAKA MINNE, ILIKUWA HOTUBA YA KAZI KAZI NA SI AHADI* Naa *Joseph Yona*

*JY-MbagalaZmaHome*

0713802226 yonapavea@yahoo.com

ZIFUATAZO ni nukukuu mbalimbali za aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dkt. John Pombe Magufuli* wakati akilivunja Bunge la 11 mjini Dodoma Leo Juni 16, 2020.

Nukuu hizi ni kielelezo tosha Cha kazi kubwa sana imefanywa na Serikali ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 - 2020.

*FUATANA NAMI*

(1).Wakati tukiingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha, pamoja na matukio ya mauaji kule Kibiti na kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitendo hivyo vilikomeshwa na nipende kusema kuwa nchi yetu kwa sasa ni salama - Rais Magufuli

(2) "Ripoti ya Global Peace Index ya mwaka 2020, imeonyesha Tanzania ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki na ya 7 kwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara kwa kuwa na amani na utulivu." - Rais Magufuli, Bungeni 16/06/2020

(3) "Idadi ya watalii na mapato yameongezeka, 2019 tulipokea watalii zaidi ya Mil 1, mapato yameongezeka kutoka Dola Bil 1.9 2015 hadi Dola Bil 2.6 mwaka 2019, isingekuwa Corona mwaka huu pia idadi ya watalii na mapato yake yangeongezeka maradufu" - JPM

(4) "Tulizidisha mapambano dhidi ya rushwa, uhujumu uchumi na ufisadi, nilianzisha Mahakama ya Uhujumu uchumi ambapo imeshapokea mashauri 407, TAKUKURU imefungua mashauri 2,256 ambapo kati ya mashauri 1,926 yaliyotolewa uamuzi, Serikali imeshinda mashauri 1,013." - JPM, Bungeni Dodoma 16/06/2020

(5) "Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 273.38 zikiwemo fedha walizokuwa wamedhulumiwa wakulima"- Rais Magufuli, Bungeni Dodoma 16/06/2020

(6) “Tumeongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya 1769, zikiwemo zahanati 1198, vituo vya afya 487, Hospitali za Wilaya 71, Hospitali za Mikoa 10, Hospitali za Rufaa za Kanda 3, tumeajiri watumishi wa afya wapya 14,479, wakiwemo Madaktari 1000 walioajiriwa hivi karibuni”-JPM, Bungeni 16/06/2020

(7) "Tumejenga vituo vya afya,kuimarisha upatikanaji wa dawa,kununua magari ya kubebea wagonjwa 117,tumesomesha madaktari bingwa 301 ambapo imepunguza idadi ya rufaa za wagonjwa kutibiwa nje ya nchi pia baadhi ya wagonjwa kutoka nchi zingne wameanza kutibiwa hapa" - JPM

(8) "Tumefanikiwa kusomesha madaktari Bingwa 301 ambao wameongeza huduma katika magonjwa ya moyo, figo, sikio. Vifo vya watoto wachanga chini ya siku 28 vimepungua kutoka 25 hadi 7 kwa vizazi 1,000. Wagonjwa kutoka nje ya nchi wameanza kuja husasani wa moyo." - Rais Magufuli

(9) "Tunaendelea kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa SGR na awamu ya pili imefikia 30% ambapo mradi huu unatumia fedha za Serikali yetu kwa 100%, ujenzi wa sehemu ya Mwanza, Isaka hadi Dodoma ipo kwenye maandalizi, hivi karibuni tutaitangaza ianze kujengwa". - Rais Magufuli

(10) “Kutokana na kuimarishwa kwa matibabu ya kibingwa baadhi ya wagonjwa kutoka mataifa ya jirani wameanza kuja kutibiwa nchini hususani magonjwa ya moyo” - JPM, Bungeni Dodoma 16/06/2020

(11) " Idadi ya Wanafunzi wanaojiunga vyuoni imeongezeka kutoka 65,064 mwaka 2015 hadi 87,813 mwaka 2020. Wanaopata mikopo wameongezeka toka 98,300 2014/15 hadi 130,883 mwaka 2019/20. Nitakuwa sijakosea nikisema kazi kubwa imefanyika kwenye sekta ya elimu" - JPM

(12) "Tumepanua wigo wa upatikanaji wa huduma za Elimu, Afya na Maji. Tumetoa elimu bila malipo; tumeweza kuongeza madawati kutoka zaidi ya milioni 3 hadi zaidi ya milioni 8. Tumeongeza Mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Bilioni 348.7 hadi Bilioni 450." - Rais Magufuli

(13) "Kutokana na jitihada zilizofanyika katika sekta ya maji, upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka kutoka 47% mwaka 2015 hadi 70.1% mwaka 2020, upatikanaji wa maji mijini umeongezeka kutoka 74% mwaka 2015 hadi 84% mwaka 2020" - JPM

(14) "Tunaendelea kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa SGR na awamu ya pili imefikia 30% ambapo mradi huu unatumia fedha za Serikali yetu kwa 100%, ujenzi wa sehemu ya Mwanza, Isaka hadi Dodoma ipo kwenye maandalizi, hivi karibuni tutaitangaza ianze kujengwa". - Rais Magufuli

(15) “hivi sasa tunafanya upanuzi wa Bandari zetu kubwa Mtwara na Tanga. Vilevile tunaboresha ujenzi wa meli zetu. Kwa upande wa Ziwa Victoria kwa mfano tumekamilisha meli tano, na sasa tunaendelea na ujenzi wa Meli Mpya, ‘Hapa Kazi Tu’.” - JPM

(16) "Tumekamilisha ujenzi wa barabara za kiwango cha lami za kiasi cha kilometa 3,500. Tumeanza kujenga flyovers na interchange kwa kuanzia Dar ili kupunguza msongamano." - Rais Magufuli

(17) "Tumefufua ATCL kwa kununua ndege mpya 11 na ambapo 8 zimefika na nyingine zinatengenezwa. Faida nyingine ya ndege tumeiona katika kipindi hiki cha Corona ambapo Watanzania mbalimbali waliokwama ikiwemo India tumewarejesha." - Rais Magufuli

(18) "Ndege zimeanza kuja kutoka nchi za nje kwa ajili ya kubeba samaki wetu, mauzo ya samaki nje ya nchi yameongezeka kutoka wastani wa TZS Bil.379 mwaka 2015 hadi TZS Bil.692 mwaka 2019" - Rais Magufuli

(19) "Tumeimarisha huduma za mawasiliano hususan katika kuboresha usikivu wa simu kutoka 79% mwaka 2015 hadi kufikia 94% mwaka 2019, idadi ya watumiaji wa simu za mkononi pamoja na watumiaji data imeongezeka maradufu "- Rais Magufuli

(20) “Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi pamoja na watumiaji data imeongezeka maradufu na hali hiyo imechangiwa na kupungua gharama za kupiga simu kwa dakika moja toka shilingi 267 mwaka 2015 hadi shilingi 40 tu hivi sasa” - Rais Magufuli, Dodoma Bungeni 16/06/2020

(21) "Tumeboresha upatikanaji wa nishati ya umeme. Ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere Hydropower Station unaendelea ingawa ulipigiwa kelele sana. Pesa zote za ujenzi ni za Watanzania. Umetumia Tsh. 6.5 trilion na unaweza kuzalisha 2,115 MegaWatts." - Rais Magufuli

(22) "Shughuli za Sanaa na Burudani ziliongoza kwa ukuaji 2018 sekta hii ilikuwa kwa 13.7%, na 2019 ilishika nafasi ya 3 kwa ukuaji wa 11.2%, hongereni sana wasanii wetu hususani Bongofleva,Filamu,mpira nk, kazi zenu sio tu zinaburudisha na kuchangia uchuki ila zinaitangaza Nchi”-JPM

(22) "Naipongeza Timu yetu ya Taifa ya Soka ambayo baada ya takribani miaka 39 kupita hatimaye mwaka jana ilifanikiwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la Afrika,nawapongeza wanamichezo mingine waliopeperusha vizuri bendera yetu hususani katika ndondi na riadha”-JPM

(22) "Kutokana na hatua mbalimbali tulizozichukua za kuimarisha sekta mbalimbali kiuchumi, kwa wastani katika miaka mitano iliyopita uchumi wetu umekua kwa 6.9% kutoka 6.2% mwaka 2015" - Rais Magufuli

(24) "Biashara yetu nje imeongezeka kutoka TZS Tril.11.5 mwaka 2014/15 hadi TZS Tril. 16.6 mwaka 2018/19, Tanzania imekua na ulali chanya wa mauzo ya bidhaa kwenye masoko ya nchi ya SADC na EAC" - Rais Magufuli

(25) "Nina imani kubwa Watanzania watanendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuongeza nchi yetu ktk vipindi vingine vijavyo na ninaamini katika misingi ya ukuaji wa uchumi tuliyoieweka, nchi yetu katika miaka 5 ijayo tutafanya makubwa zaidi" - JPM Bungeni Dodoma 16/06/2020

*#T2020JPM*
*0713802226*View attachment 1499173View attachment 1499174View attachment 1499178
Wewe unaona hapo katika picha kuna chochote cha maendeleo ya mkulima? Ni miradi ambayo wafaidika wakubwa ni wale waliochukua tenda, yaani MABEBERU.
 
Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe Rais Magufuli
 
Siasa haijawahi kuwa mchezo msafi, hata siku moja.
 
Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe Rais Magufuli
Alisema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Akasema atamkata mtia nia yeyote kwa kuangalia alivyoamka siku hiyo.

Huyu anaweza kusema lolote.
 
Kuna jamaa kilosa aliambiwa ana kiherehere ndo maana anazabuliwaga makofi na mkewe


Halafu Dodoma hamna joto kunafaa kwa kupiga push ups za haraka haraka zile za Asubuhi.🤣🤣
Mtoto Kama Unampa Uji Na Bado Analia Si Unamzaba Kibao Ili Abugie Uji Vizuri.
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
😀😁😄😏😄😃😃
 
Nimeamua kuyatoa maisha yangu sadaka kwa ajili ya kuwapigania watanzania ikibidi hata nife. Maisha yangu hayatakuwa na thamani kama Rais kwa kuona watanzania wakifa kwa kukosa dawa hospitali, watoto wa masikini wakikosa elimu, hali ya usafiri ikiwa mbaya, halafu mimi niwe sehemu ya wanaoshiriki kuhujumu taifa hili kwa kufukuzana na machinga barabarani huku tukiacha kukusanya kodi kwa wanaokwepa kulipa kodi ya serikali. Nimeamua nchi iende na atakayejaribu kutukwamisha, atakwama yeye mwenyewe Rais Magufuli
Hayo mbona hata Mobutu seseko aliyasema sana. kule kwa Kagame wanaamini yeye ndiye kila kitu. Hahahaa mnajidanganya na vimaneno vya kujitia moyo. Disgrace.
 
Alisema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Akasema atamkata mtia nia yeyote kwa kuangalia alivyoamka siku hiyo.

Huyu anaweza kusema lolote.
Hata shetani alikuwa mbinguni akimwimbia na kumtukuza Mungu.
 
Wajinga ndo watamwani huyu mzee kama ameamua kurisk asipokee mshahara hata sh.100 pia amrudishe Azory Gwanda na Ben-Saanane.
Hahaha jamaa ana maumivu moyoni kwa matendo yake. Anajaribu kutafuta sympathy.
 
Mtoto Kama Unampa Uji Na Bado Analia Si Unamzaba Kibao Ili Abugie Uji Vizuri.
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
😀😁😄😏😄😃😃
Nimemuonya DAS kutembea na wake za watu hasikii Leo tunamalizana Hapahapa...., (Mke mwenyewe mchepuko JHOKATE) ..........lol
 
Alisema atawapiga wapinzani mpaka shangazi zao.

Akasema atamkata mtia nia yeyote kwa kuangalia alivyoamka siku hiyo.

Huyu anaweza kusema lolote.

Kushona barakoa ni rahisi tu, si ipo kama titi? Aah samahani Wazir wa afya
 
Back
Top Bottom