Nyerere alikosea sana alipokumbatia wahindi/warabu na kuwafukuza wazungu

Nyerere alikosea sana alipokumbatia wahindi/warabu na kuwafukuza wazungu

Kasome tena historia vizuri hakuna mzungu aliyefukuzwa.

Hao wahindi na waarabu unaowaona toka ukoloni walikuwa wafanya biashara na ndio walijenga hayo majengo posta mengi ni wao.

Wazungu wao walikuwa ni gvt officers kwa hiyo baada ya uhuru wengi walisepa kwao maana kilichowaweka hapa hakikuwepo.

Ukweli mchungu tanganyika chini ya ukoloni ilikuwa sawa na mapori tu sehemu kubwa Nyerere chini ya Tanu amefanya kazi ya ziada na kizalendo kuunganisha viclan vidogovidogo kuwa makabila isee sio poa, viwanda, elimu imagine unakabidhiwa nchi na maengineer 3 tu. Madaktari hawafiki 100 walimu hawazidi 500..rami ni njia za mashamba makubwa tu we sio mchezo iliitaji uzalendo wa hali ya juu..

makosa yaliyofanyika ni kwa sababu ya kukosa experience ila mimi nampongeza yeye na viongozi wote wa awamu ile ya kwanza walifanya sehemu yao na walifanya vizuri sana.

Makosa makubwa sana ambayo tunayafanya sasa ni planning ya miji yetu ni ya ovyooo sana na itatucost pesa nyingi sana huko mbeleni maana ni lazima miji ije kupangwa upya kwa gharama za serikali hili haliepukiki.
Kama huna experience una weka wataalamu wa kukushauri na sio waganga wa kienyeji
 
Kipindi Cha azimio la Arusha wazungu wengi walifukuzwa Ila Cha ajabu wakabaki wahindi Leo hii wahindi na wakifuatiwa na warabu ndo wamekamata biashara kubwa na Wana ukwasi Mkubwa

Maajabu ya mhindi/mwarabu hata nyumba ajengi Yuko tayari kuishi kwenye nyumba za NHC au kupanga kule kariakoo au upanga na kamwe hawez fanya uwekezaji wa maana hapa Tanzania
Wewe hufai hata kujiita mtanzania maana hata hiyo historia ya nchi yako huijui wala huna hamu ya kutaka kujua. Unalojua wewe ni ubaguzi wa rangi tu. Hivi hata huwezi kufikiria kuwa zile nyumba za maeneo ya Upanga ni za wahindi kiasili?

Nyerere hakubagua watu lakini ni sisi wenyewe wabantu tusiokuwa na uwezo wala ujuzi wa kuendeleza biashara ndiyo tumekwama hapa tulipo mpaka leo hii. Tumeshindwa nini kuendeleza kilimo na sisi tukawa wakulima wakubwa kama wenzetu Kenya? Idi Amini wa Uganda aliwapora wahindi biashara na viwanda na kuwapa Waafrika na matokeo yake uchumi ulianguka na hakukuwa na lolote lililofanyika.

Nyinyi kaeni na roho zenu mbaya hamutaendelea maana kila siku munawaza kurudisha nyuma wengine kimaendeleo badala ya kufikiria jinsi ya kujikwamua wewe mwenyewe ukasonga mbele.
 
Hili ni kosa zito mno Hayati Nyerere alilolifanya. Kuiga sera za kikomunisti na ujamaa ndo kama aliua nchi.
 
Back
Top Bottom