Kasome tena historia vizuri hakuna mzungu aliyefukuzwa.
Hao wahindi na waarabu unaowaona toka ukoloni walikuwa wafanya biashara na ndio walijenga hayo majengo posta mengi ni wao.
Wazungu wao walikuwa ni gvt officers kwa hiyo baada ya uhuru wengi walisepa kwao maana kilichowaweka hapa hakikuwepo.
Ukweli mchungu tanganyika chini ya ukoloni ilikuwa sawa na mapori tu sehemu kubwa Nyerere chini ya Tanu amefanya kazi ya ziada na kizalendo kuunganisha viclan vidogovidogo kuwa makabila isee sio poa, viwanda, elimu imagine unakabidhiwa nchi na maengineer 3 tu. Madaktari hawafiki 100 walimu hawazidi 500..rami ni njia za mashamba makubwa tu we sio mchezo iliitaji uzalendo wa hali ya juu..
makosa yaliyofanyika ni kwa sababu ya kukosa experience ila mimi nampongeza yeye na viongozi wote wa awamu ile ya kwanza walifanya sehemu yao na walifanya vizuri sana.
Makosa makubwa sana ambayo tunayafanya sasa ni planning ya miji yetu ni ya ovyooo sana na itatucost pesa nyingi sana huko mbeleni maana ni lazima miji ije kupangwa upya kwa gharama za serikali hili haliepukiki.